vendredi 9 octobre 2009

HALI YA PURUKUSHANI BAINA YA POLISI NA WAKIMBIZI HUKO GIHINGA

kumetokea hali ya mvutano kati ya Polisi wa uslama wa raia nchini Burundi na wakimbizi wa congo wa kabila la Banyamulenge. Tukio hilo limetokeya ktk kambi ya Gihinga iliyo mkoani Mwaro kati kati mwa Bdi umbali wa kilometa 70 hivi na mji mkuu Bujumbura, ambako askari polisi wamewafiatuliya risase wakimbizi banyamulenge na wawili miongoni mwao kujeruhiwa, huku wengine watatu wakizirayi kutokana na miliyo ya risase kambini hapo Gihinga. Kambi hiyo ya Gihinga ilikuwa imewapa hifadhi wakimbizi Banyamulenge 2317 kutoka nchi jirani ya RDC. Septemba 21 ndipo Shirika la UM linalo wahudumiya wakimbizi UNHCR liliamuru kusitisha huduma zake zote kwa wakimbizi hao, baada ya wakimbizi hao kupinga kuhamishiwa ktk kambi ya bwagiriza iliyo ktk mkoa wa Ruyigi mashariki mwa Bdi kwenye mpaka na Tanzania. Septemba 30 shirika la UNHCR lilitangaza kuwa kambi ya Gihinga imefungwa licha ya wakimbizi hao kusaliya kambini huku miongoni mwao 264 wakikubali kuhamishiwa bwagiriza mkoani Ruyigi. Hatua hiyo ilipelekeya wakimbizi hao kuchukuwa uwamuzi wa kurudi kwa mguu nchini kwao RDC, hatua ambayo imeanza kutekelezwa jumanne hii.

samedi 12 septembre 2009

WANASIASA NCHINI BURUNDI WATOFAUTIANA KUHUSU SHERIA YA UCHAGUZI

BUJUMBURA: Kumekuwa na hisia tofauti baina ya wanasiasa nchini Burundi kuhusiana na sheria ya uchaguzi iliopasishwa bungeni usiku wa alhamis kuamkia ijumaa septemba 11, 2009. Chama Sahwanya FRODEBU kimesema kufurahishwa na hatuwa hiyo ya kupasisha sheria ya uchaguzi bungeni, lakini hata hivo mwenyekiti wa chama SAHWANYA FRODEBU Leonce Ngendakumana amesema kuwa na wasiwasi hasa kwamba kadi moja ya uchaguzi iliokuwa ikitetewa na chama hicho haikupasishwa kaika muswada huo. upande wake msemaji wa chama FNL Bosco HAVYARIMANA amesema kuwa wabunge wamekwenda kinyume kabisa na maafikiano waliokuwa wamekubaliana siku za nyuma. kiongozi huyo amesema kuwa kiwango cha dhamana kinacho takiwa kwa wagombe viti mbalimbali vya uchaguzi hakina sababu za kuwepo. upande wake mwenyekiti wa chama CNDDLéonard Nyangoma amesema ni aibukubwa sana kwa taifa la Burundi. upane wake amesema sheria hiyo ya uchaguzi inakuja kurejesha nyuma hatuwa za demokrasia nchini Burundi ukilinganisha na sheria.

BAADA YA MVUTANO WA SIKU NZIMA, HATIMAE WABUNGE WAMEPASISHA SHERIA ZA UCHAGUZI SAA TISA USIKU

BUJUMBURA le 11.9.2009:Hatimae wabunge nchuini Burundi wamepasisha muswada wa sheria uhusuo uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Tangu saa tatu asubuhi alhamis Septemba 2009, wabunge walitakiwa kujadili na kupasisha muswada wa sheria uhusuo sheria za uchaguzi nchini Burundi. Kutokana na utata uliokuwemo katika sheria hizo, ilikuwa vigumu kupatikana muafaka, hadi saa tisa usiku wa kuamlia ijumaa septemba 11, wabunge walifikia muafaka na kusaini sheria zihusuzo uchaguzi wa 2010. miongoni mwa walioafikiana ni pamoja na mpangilio wa uchaguzi utaoanzia kwa viongozi wa madiwani na baadae kufuatia uchaguzi wa rais, utaofuatiwa na na wa bunge na seneti na kuhitimishwa kwa ule wa viongozi wa ngazi za china. Ama kuhusu kadi ya uchaguzi, wanasiasa hao wameafiki kutumia kadi tofauti na vijisanduku 2. kimoja kitapokea kadi iliopiga kura na nyingine itayo tupwa katika kijisanduku maalum kitachokuwa kimeandaliwa. Ili kuepusha wizi na udanganyifu, kadi zote zitahesabiwa, zile zilizo chaguliwa na zile zilizo tupwa sehemu kutakokutikana na udanganyifu sehemu hiyi uchaguzi utafutwa na baadae kuandaliwe mwingine katika kipindi kisichozidi siku 5. kuhusiana na dhamana anayo takiwa kutowa mgombea kiti cha urais imesalia kuwa franka za Burundi millioni 15, pesa hizo zitarejeshwa iwapo mgombea hatofikisha asilimia 5 ya kura zitazopigwa nchi nzima. Mgombea kiti cha ubunge atalipa dhamana inyo lingana na franka za Burundi laki 5 huku , mgombea kiti cha uanaseneta akilipa franka za Burundi laki 4. Pesa hizo zitarejeshwa iwapo wagombea hao hawatofikisha asilimia 2 ya kura zitazopigwa kote nchini. Wabunge walikubaliana pia kuhusu kufutwa ubunge kwa mbunge ataekuwa amekitoroka chama chake na kujiunga na chama kingine swala ambalo lililo zusha utata, hatimae wabunge wamekubalina na swala hilo.

mercredi 9 septembre 2009

KUKOSEKANA KWA SHERIA JUU YA UCHAGUZI NCHINI BURUNDI KWA CHELEWESHA SHUGHULI ZA TUME HURU YA UCHAGUZI CENI.

Bunge nchini Burundi limeahirisha kwa mara ya tena kikao cha dharura kilichoititishwa na rais wa jamuhuri tangu jumatatu iliopita. Wabunge walitakiwa kujadili jumatano hii muswada wa sheria uhusuo sheria za uchaguzi wa 2010 unaosubiriwa na wengi nchini Burundi. Spika wa Bunge Pie Ntavyohanyuma ameskika akisema kuwa kuna umuhimu wa kuahirisha muswada huo wa sheria ukizingatia kuwa hakujapatikana muafaka kuhusu baadhi ya vipengee. Baadhi ya yanayo leta utata na kupelekea wanasiasa kutoelewana ni pamoja na orodha ya utaratibu mzima wa uchaguzi utavyo fanyika. Chama tawala CNDD-FDD kinataka uchaguzi uanzie juu, yaani uchaguzi wa rais, huku vyama vingine vikitupilia mbali pendekezo hilo. Pia, kadi ya uchaguzi, wanasiasa wanaomba iwe moja kwa vyama vyote vitavyo jikita katika mlolongo wa uchaguzi wakati ambapo chama tawala CNDD-FDD kikiomba pawepo na kadi tofauti kwa kila chama. Swala la dhamana pia linazusha utata ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2005 mgombea kiti cha urais alitakiwa kilipa franka za Burundi milioni 3, lakini mwaka huu wa 2010 mgombea kiti cha urais anatakiwa kulipa franka za Burundi milioni 15. Swala la msamaha wa muda uliotolewa miaka ya nyuma kwa viongozi waliohusika kwa njia moja ama nyingine na machafuko nchini Burundi linazuia pia tafrani. Kukosekana kwa sheria juu a uchaguzi kunachelewesha shughuli za tume ya uchguzi CENI kuanza kazi zake. Wabunge wamepanga kukutana tena alhamis septemba 10/9/2009 kujaribu kutafuta muafaka kuhusu sheria juu ya uchaguzi.

MAZOEZI YA PAMOJA YA KIJESHI YA NCHI ZA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI YA ZINDULIWA NCHINI TANZANIA

Rais wa Tanzania Jakaya Mrishio kikwete amezindua rasmi mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya nchi za jumiya ya Afrika mashariki huko Monduli, Mkoani Arusha jumanne 8.9.2009 asubuhi. Baadhi ya makamanda waandamizi wa majeshi ya nchi za Afrika Mashariki wanashiriki katika mazoezi hayo ya pamoja kutoka katika kilima cha Nodosoito huko monduli mkoani Arusha. Burundi, Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya ni nchi wanachama wa jumuia hiyo ya Afrika mashariki. Kama unavyo ona kwenye picha ma kamanada wa kijeshi kutoka nchi hizo wakimuonyesha rais Jakaya Mrisho Kikwete sehemu kutako endeshewa mafunzo hayo.

POLISI YA USALAMA WA RAIA HAIJA FAULU KUWAKAMATA MAJAMBAZI WALIOJARIBU KUMMALIZIA MAISHA MSANII JOHN CHRIS


Hadi sasa polisi haijafaulu kuwakamata watu waliojaribu kummalizia maisha msanii John Chris wakati wa likizo yake mjini Bujumbura. John Chris alinusurika katika tukio lililo endeshwa na watu ambao hawajajulikana katika usiku wa kuamkia jumanne Septemba Mosi mwaka huu. Kama alivyo eleza mwenyewe kwenye Vyombo vya habari Msani huyo mwenye asili ya Burundi ambae sasa anaishi Mjini Bruxels Ubelgiji alikuwa pamoja na familia katika sherehe za kuagana kwa kuwa alikuwa amehitimisha likizo yake mjini Bujumbura, wakati alipo toka akiwa na walinzi wake 2, alijieleza sehemu kujisaidia, alipo rudi ndipo akakuwa watu 2 waliokuwa na bastola tayari kuziweka kichwani kwa walinzi aho ambao walikuwa ni askari polisi waliovalia nguo za kiraia. Alipo fika nae akawekwa bastola kichwani na kuambiwa aondowe kila kilicho mfukoni mwake, hakusita kufanya hivo kama alivyo eleza. Lakini mmoja kati ya walinzi wake alijaribu kujiokowa kwa kuridi nyuma ili apate jinsi ya kutowa bastola ambayo aliokuwa nayo ili awashambulie majambazi hao, huku mwengine akimsukuma msanii huyo kama kumponyesha. Mmoja kati ya majambazi hao alirusha rusase zikampata mmoja kati ya walinzi kwenye mbavu. Majamabazi hao walitimka baada ya kuona kwamba mambo yamekuwa magumu. Askari polisi huyo afya yake sio mbaya anaendelea kupata matibabu kwenye Hospitali mojawapo jijini Bujumbura.

jeudi 27 août 2009

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHINI BURUNDI APIGA MARUFUKU KWA MA GAVANA KUTOWA VIBALI VYA KUTEMBELA WAKATI ZINAPO FANYIKA SHUGHULI ZA USANIFISHAJI

Waziri wa mambo ya ndani amewapigia maarufu magavana kutoa ruhusa jumamosi wakati wa shughuli za usafi. Waziri Edouard Nduwimana ameiambia idhaa hii kwamba hatua yake imetokana na wananchi wengi kuomba ruhusa za udhuru wa kusafiri jumamossi na hivo shughuli za usafi kuonekana zikipuuziwa. Amewashauri wananchi hasa wasafiri badala ya kun’gan’gania kuomba ruhusa za jumamossi waandae mikakati ya safari zao mapema kuhakikisha kwamba wamefika katika maeneo wanakokwenda kabla au baada ya shughuli za usafi za jumamossi asubuhi. Aidha waziri huyo wa mambo ya ndani amesema kwamba iwapo udhuru wa kuomba idhni utaonekana una umuhimu mkubwa kama shughuli za musba au safari za ndege, basi wakuu wa mikoa watajadili hilo na kumpa ruhusa muhitaji.

VIONGOZI NCHINI BURUNDI WAMESHSREHEKEA MIAKA 4 KITITI WAKIWA KWENYE UTAWALA

Jana Agosti 26 viongozi walioteuliwa kwa misingi ya kidemokrasia nchini Burundi walitimiza miaka 4 kititi wakiwa kwenye utawala, baada ya uchaguzi wa mwaka 2005. Rais wa jamuhuri Pierre Nkurunziza nae pia ametimiza miaka 4 akiwa kwenye usukani wa kuiongoza Burundi. Rais Nkurunziza alizungumzia katika hutba yake jana kuhusu mustakabali mzima wa kuiongoza nchi na matatizo anayo kumbana nayo pia na mipango ijayo. Miongoni mwa yaliotekelezwa na serikali yake ni pamoja na mpango wa kudumisha amani nchini Burundi ambapo wakati huu nchini Burundi hakuna tena makundi ya uasi. Katika mipango ijayo Rais Nkurunziza amefahamsiha kuwa uchaguzi utafanyika kama ilivyo pangwa na katiba ya Burundi ameahidi kuwa uchaguzi utafanyika katika hali tulivu na ya muafaka, ameomba wale wanaopendelea kufuatilia shughuli za uchaguzi wa Burundi wangeanza mapema wakati huu. Kuhusu secta ya Afya na jamii rais Nkurunziza alitangaza mpango wa kutowa tiba kwa akinamama kuanzia mwanzo wa ujauzito hadi wanajifungua na baadae. Rais Nkurunziza ametumia fursa hiyo kukemea baadhi ya ma dactari na wauguzi ambao wamekuwa wakitowa kauli mbaya kutokana na mpango huo wa kutowa tiba pasina malipo.

mardi 18 août 2009

BEI YA MAFUTA YA GARI YAPANDA KWA MARA YA TENA

Serikali ya Burundi imechukuwa hatuwa ya kupandisha bei ya mafuta ya gari. Mafuta aina ya essence imepanda kutoka franka 1650 hadi 1700 lita moja huku mafuta aina ya Mazout ikipanda kutoka franka 1600 hadi 1650. hatuwa hii imechukuliwa wiki mbili baada ya kuchukuwa uamuzi kama huo, hali ambayo iliopelekea bei ya nauli za usafuri kwa abiria wanaosafiri kutoka katika tarafa mbalimbali na hata mikoani kupanda. Shirika linalo tetea haki za wanunuzi ABUCO limeihimiza serikali kufuatiliya kwa karibu bei ya mafuta ya petroli na kukomesha kuongeza bei ya mafuta hayo kwani husababisha ongezeko pia la bei ya bidha nyingine mahitajio.

ALEXIS SINDUHIJE MWENYEKITI WA CHAMA MSD ATAKIWA KUTOWA USHAHIDI DHIDI YA MATAMSHI YAKE


Mkuu wa chama MSD Alexis Sinduhije Jumanne Agosti 18 ameripoti mbelele ya hakimu mkuu wa jamuhuri katika jiji la Bujumbura akitakiwa kutowa ushahidi juu ya matamshi yake kuhusiana na kuwepo na njama ya kuunda kundi la vijana wa kabila la kitutsi lenye lengo la kuwamaliziya maisha baadhi ya watu nchini wakiwemo viongozi, ili baadae wavikwe dhamana wafuasi wa chama MSD. Na kwamba mpango huo umekuwa ukiandaliwa na idara ya upelelezi.

POLISI MKOANI MURAMVYA YAFAULU KUKAMATA NOTI ZA MAGENDO ELFU 30 ZA ELF 5

Noti za magendo 30 za elfu 5 zilikamatwa Bugarama katika mkoa wa Muramvya. Noti hizo zilikamatwa zikiwa na bwana jean Minani aliekamatwa na askari polisi, na kudai kuwa pesa hizo alizipata baada ya kuuza ngombe. Lakini majirani wa mtu huyo wamekanusha kuwa hajawahi kuuza ngombe wala kufuga, na kwamba mtu huyo amekuwa akitowa noti hizo za elfu 5 bandiya ili kununuwa pombe. bwana huyo amewekwa kizuizinii mkoani hapo Murambya.
Viongozi tawala Mkoani hapo Muramvya wamewatolea mwito wananchi kuwa makini sana wanapo pokea noti.

vendredi 14 août 2009

MIAKA 5 IMEMALIZIKA TANGU YATOKEE MAUAJI YA WATU ZAIDI YA 160.

Wakimbizi Banyamulenge kutoka RDC alhamis hii Agost 13 wameadhimisha mwaka 5 tangu kuuawa kikatili wakimbizi 161 katika kambi ya Gatumba waliko kuwa wamepewa hifadhi , ilikuwa Agosti 13 mwaka wa 2004. Walionusurika katika mauwaji hayo wameitaka serikali ya Bdi na jamii ya kimataifa kufahamisha matokeo ya uchuguzi uliofanyika ili sheria iweze kufuata mkondo wake., amebaini hayo David BaNoGe msemaji ya walionusurika katika mauwaji hayo ya Gatumba. sherehe za kuweka mashada ya mauwa kwenye kaburi la pamoja waliko zikwa wahanga wa mauwaji hayo, zimeanfayika ambapo baadae hutba mbalimbali zilitolewa.
Itakumbukwa kuwa wapiganaji zamani wa FNL walithibitisha kuhusika na mauaji hayo na kusema kwamba walikuwa wakipambana na majeshi ya Burundi, na baadae wakaaza kushambuliwa na makombora kutoka katika kambi hiyo, hivo kujibu, na baadae kukuta kulikuwepo makundi ya wanajeshi waliokuwa na nia ya kuendesha mashambulizi mjini Uvira. Msemaji wa FNL zama hizo Pasteur Habimana alithibitisha hilo na kubaini kuwa kulikuwepo na vifaa vinavyo tumiwa kwa kuunguza majumba aina ya unga, ambavyo vilivyo sababisha watu hao wasiokuwa na hatia kuteketea. Serikali ya Burundio zama hizo ilikanusha madai hayo na kushutumu moja kwa moja makundi ya wa wapiganaji wa Rwanda wa FDLR na Mai Mai kuhusika na mauaji hayo. Miaka 5 sasa imemalizika hakuna ukweli wowote kuhusu mauaji hayo. Jamii ya kimataifa na serikali za Burundi na DRC kwa nini zimesalia kimya ? Nani aulizwe ao nani alaumiwe ?

BUNGE LA BURUNDI LAIDHINISHA MUSWADA WA SHERIA UNAOPIGA VITA MATUMIZI YA SILAHA ZA MAANGAMIZI

Bunge la Burundi limeidhinisha alhamis hii Agost 13 muswada wa sheria ya kimataifa inayo piga marufuku matumizi ya silaha za maangamizi makubwa na makombora mengine madogo madogo yanayo weza kuripuka pindi mtu anapo yasogeleya. Silaha hizo zinao uzito wa kilo 20, na zaweza pia kuripuka kabla ya kuwasili pale yalipo elekezwa. Waziri wa ulinzi wa Burundi Germain Niyoyankana alikuwa mgeni wa heshma bungeni kufafanuwa mswada huo wa sheria. Wabunge wamemuuliza umuhimu wa usainiwaji sheria hiyo kwa Bdi, waziri wa ulinzi amejibu ya kuwa sheria hiyo ni muhimu ktk lengo la kujikinga na kujihami pindi Bdi ipo kuwa imeshambuliwa. Jumla ya wabunge 98 waliohudhuria kikao hicho cha bunge, wabunge 98 wameipasisha huku mmoja akisaliya pasina kubaini msimamo wake.

mercredi 17 juin 2009

RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA AREJEA NYUMBANI BAADA YA KUSHIRIKI MAMOBOLEZO YA KIFO CHA MAREHEMU OMAR BONGO ONDIMBA


Rais wa jamuhiri Pierre Nkurunziza amerejea nyumbani hii leo akitokea mjini Libreville nchini Gabon ambako alikuwa amekwenda kutowa heshimwa zake za mwisho kwa marehemu Elhadji Omar Bongo rais wa Gabon aliefariki huko Barcelona Hispania wiki zilizopita. Rais Nkurunziza kama vile ma rais wengine 15 wa bara la Afrika walishiriki jana katika shughuli za kuomboleza kifo cha rais huyo Mkongwe wa ma rais wa Afrika. Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa jijini Bujumbura rais Nkurunziza amesema nchi ya Gabon ilionyehsa utawala bora katika kipindi cha muda mrefu, hasa marehemu Omar Bongo Ondimba alisaidia sana katika kuyasogeza makundi yaliokuwa yakigomba nchini Burundi kwa kuwashawishi wakae kwenye meza ya majadiliano. Ameendelea kuwa mbali na Burundi Marehemu Omar Bongo Ondimba alichangia pia katika kusuluhisha mizozo mingi barani Afrika. Pierre Nkurunziza amesema kutokana na uongozi wake bora marehemu Bongo alipendwa sana na wananchi wake ambao wameshuhudiwa wakistika kifo cha rasi wao, hivo rais Omar Bongo atasalia kuwa mfano wa kuigwa na viongozi wa bara hili la Afrika.

mercredi 20 mai 2009

KWA MARA YA TENA BARAZA LA SENETI LAONYESHA NIDHAMU NA UZALENDO


Baraza la Seneti limeidhisha majina yaliopendekezwa na rais wa jamuhuri Pierre Nkurunziza kwenye nyadhifa mbalimbali. Waziri wa ulinzi meja jenerali Germain Niyoyankana aliwasilisha kikaoni jina la Brigadia jenerali Ndegeya diomède ambae alipendekezwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwa kaimu mkuu wa majeshi ya Burundi. Brigadia jenerali Ndegeya Diomede aliidhinishwa kuwa kaimu mkuu wa majeshi ya Burundi. Upande mwigine, waziri wa mambo ya ndani Edourd Nduwimana aliwasilisha majina ya walipendekezwa na rais kuiwakilisha Burundi ugenini. Nibizi Isidore na Bashimiyubusa Denis kutoka chama FNL wamepasishwa kuiwakilisha Burundi ugenini. Elias Buregure wa chama CNDD-FDD ambae aliwahi kuwa mea wa jiji la Bujumbura kabla ya kuwa waziri mdogo wa kazi za serikali amekataliwa na wanaseneti kuiwakilisha Burundi ugenini kwa kushtumiwa katika kesi mbalimbali za ubadhilifu mali ya umma. kulingana na habari kutoka kwa wanaseneti Elias Buregure alijihusisha na rishwa katika utowaji viwanja vya ujenzi wakati alipokuwa waziri mdogo wa kazi za serikali ambae alipingana na waziri mkuu kwenye wizara hiyo katika kuchukuwa maamuzi. Baraza la seneti limeidhinisha pia majina ya ma gavana wa Mikoa ya Mwaro, Makamba na Cibitoke. Nahayo Fredine ataongoza Mkoa wa Mwaro ni kutoka chama FNL, Ntahitaja Térence ataongoza Mkoa wa Makamba ni kutoka chama CNDD–FDD, huku Bizimungu Simon akiidhishwa kuongoza Mkoa wa Cibitoke, akiwa ni mwanachama wa FNL.

KESI YA MAUAJI YA ALBINOS YASIKILIZWA NA MAHAKAMA KUU MKOANI RUYIGI.


Kesi ya watu 11 wanaoshukiwa kuendesha mauaji ya Albinos ilisikilizwa jumanne na mahakama kuu ya mjini Ruyigi. Kulingana na muandishi habari wa kituo cha Burundi cha kutawanyia ABP habari Mkoani Ruyigi Maurice Bukuru, kesi hiyo ilianza kusikilizwa tangu saa nne mchana ambapo halaiki ya watu walikuwa wamemiminika mahakamani kusilikiza kesi hiyo. Awamu ya kwanza ya kesi hiyo iliwahusisha watu 8 walioshutumiwa kuwamalizia maisha binti mmoja albinos aliejulikana kwa jina la Harerimana Violette alieuawa Septemba 8 mwaka jana, pamoja na mtoto mwgine alieuawa katika kijiji cha Kinyinya na bwana mmoja albinos alieuawa Bweru. Washukiwa wengine wanashutumiwa kuhuika na jaribio la mauaji ya Albinos. Washukiwa hao walitajwa na wafungwa ambao walikatiwa kifungo cha maisha jela ambao wanazuiliwa katika jela kuu la Ruyigi. Wafungwa hao wanaozuiliwa jela walihusika na mauaji ya binti mmoja Albinos na kuuza viungo vya mwili mtu ajulikanae kwa jina Richard Adelin wa tarafa ya Cendajuru Mkoani Cankuzo ambae yuu huru hadi sasa. Katika kesi hiyo Nyabenda Elie maharufu Bihoro alikiri kuhusika katika mauaji hayo huku wengine wakikana kuhusika moja kwa moja. Hakimu mkuu wa jamuhuri Mkoani Ruyigi Nicodème Gahimbare aliwakamata kinaga ubaga mwezi march iliopita watu 11 wakiwa na viongo vya Albinos. Mkoa wa Ruyigi ndio ambao ulioorodhesha idadi kubwa ya mauaji ya Albinos waliouawa tangu kuanzishwa kwa visa vya mauaji ya Albinos vilivyo anzia nchini Tanzania na kutanda hadi nchini Burundi. Tangu kukamatwa kwa mtandao huo wa wahalivu wa mauaji ya Albinos Mkoani Ruyigi mwezi march hakuna kitendo kiovu kama hicho ambacho kimekwisha ripotiwa hadi leo.

mardi 21 avril 2009

VITISHO DHIDI YA MWENYEKITI WA SHIRIKA LA KIRAIA LA OLUCOME NCHINI BURUNDI.

Gabriel Rufyiri mkuu wa shirika linalo jihusisha na upigaji vita rushwa na uporaji mali ya umma nchini Burundi OLUCOME ameviambia vyombo vya habari nchini Burundi kwamba siku zote hizi za nyuma amekuwa akipokea simu za watu asio wafahamu ambao wamekuwa wakimtisha na kumtia hofu. Kiongozi huyo amesema tayari amefikisha ripoti kwa hakimu mkuu wa jamuhuri jijini Bujumbura, hadi sasa amesema hajapata jibu lolote. Upande wa polisi kupitia msemaji wake Chanel Ntarabaganyi ameomba Rufyiri atowe namba za simu wanazo tumia watu hao wanaomtia hofu ili waendeshe uchunguzi. Kuhusu uchunguzi wa mauaji ya kifo cha aliekuwa naibu kiongozi wa shirika la OLUCOME Ernest MANIRUMVA alieuawa kikatili siku zilizopita na watu siojulikana bado, msemaji wa jeshi la Polisi nchini Burundi Pierre Chanel NTARABAGANYI amesema kuwa hadi sasa tume ya uchunguzi ilioundwa inaendeleza shughuli zake, na tayari imeomba msaada wa kikosi cha polisi kutoka ugenini itayo saidia katika kuendesha uchunguzi wakitumia ujuzi wa hali ya juu.

lundi 20 avril 2009

SAMAHANI NDUGU WASOMAJI

Tuna tanguliza samahani kwa wapenzi wetu wasomaji wa blog hii kwa habari tulioindika kuhusu kufunguwa mashtaka kwa kiongozi zamani wa uasi nchini DRC Laurent Nkunda ambapo tulisema kuwa ni kiongozi wa kundi la FDLR, tulijidanganya kidogo, Laurent Nkunda hakuwa kiongozi wa FDLR bali alikuwa kiongozi zamani wa kundi la CNDP. natumaikuwa tumesameheka

samedi 18 avril 2009

KIONGOZI ZAMANI WA KUNDI LA UASI LA FDLR LAURENT NKUNDA AIFUNGULIA MASHTAKA SERIKALI YA RWANDA


Kiongozi wa waasi wa FDLR aliyekamatwa nchini Rwanda Laurent Nkunda ameishtaki serikali ya Rwanda kwa kumzuilia kinyume cha sheria. Katibu wa Idara ya habari ya Rais nchini Rwanda Yoland Makolo amesema kuwa, kesi ya Jenerali Nkunda dhidi ya serikali ya Kigali imesikizwa ijumaa April 17 lakini akasita kueleza uamuzi uliotolewa. Makolo ameongeza kuwa, Nkunda atarejeshwa nchini Congo anakotakiwa kujibu mashtaka ya ubakaji, utekaji nyara, kuwashirikisha watoto wadogo vitani pamoja na jinai zinginezo. Jenerali nkunda yuko chini ya kifungo cha nyumbani tangu mwezi Januari mwaka huu anakozuiliwa na serikali ya Rwanda. Mataifa ya Congo na Rwanda yamekuwa yakinyoosheana kidole cha lawama kuhusiana na suala la waasi lakini kuzuiliwa kwa Nkunda na serikali ya Rais Paul Kagame wa Rwanda ni dhihirisho tosha kuwa nchi hizo mbili ziko tayari kubadilisha mkondo wa uhusiano wao, wamesema weledi wa mambo.

BDI-MWENYEKITI WA FNL AGATHON RWASA AREJEA KATIKA MAISHA YA KIRAIA.



Kiongozi wa kundi la uasi zamani la FNL Agathon Rwasa amerejeshwa katika maisha ya kiraia jumamosi hii April 18.2009. Shughuli rasmi zimefanyika katika kambi walimo kusanywa wapiganaji wa FNL ya Rubira. Hii ikiwa ni iashara ya kwamba amani nchini Burundi inapiga hatuwa ya kuridhisha.

Msuluhishi katika mgogoro wa FNL na serikali ya Burundi Charles Nquakula aliteuwa tume iitwayo Task Team ambayo yatakiwa kuharakisha utekelezwaji kivitendo makubaliano ya FNL na serikali ya Burundi, tume hiyo ilipanga kwamba Tarehe 21 mwezi April watarejeshwa katika maisha ya kiraia wapiganaji wa FNL na ndipo chama hicho kitasajilia rasmi kuwa chama cha kisiasa nchini Burundi ambacho kitakuwa cha 42. tarehe 22 mwezi April ndipo yataanza mafunzo ya kuwanoa bongo wapiganaji zamani wataojiunga na jeshi la taifa wapatao 2100, mafunzo ambayo yamepangwa kufanyika Mkoani Bururi huku wale wataojiunga na jeshi la paolisi wapatao 1400 wakipewa mafunzo katika vituo vya Gatumba na Rubira huko Mkoani Bubanza. Hata hivo wanajeshi wapatao 390 wakiwemo wanajeshi wa taifa na wa FNL ndio ambao watalinda usalama wa vituo mbalimbali baada ya wanajaeshi wa Umoja wa Afrika kurejea nyumbani kwao. Askari hao wataendesha shughuli hizo baada ya mafunzo ya myezi 6. wapiganaji elf 10 na wanawake 100 watapewa viinuwa mgongo na badae warejea nyumbani kwao ambapo watasaidiwa katika miradi yao ya kujiendeleza. Watoto 340 watatenganishwa na wengine wapiganaji. Ifikapo juni 30 ndio itakuwa tarehe ya mwisho, mwisho kabisa wa shughuli za kuwarejesha katika maisha ya kiraia wapiganaji zamani wa FNL. Serikali ya Burundi imetakiwa kuwaacha huri wafungwa wa FNL ambao hadi sasa wapmesalia katika jela mbalimbali. Kuhusu nyadhifa 32 zilizo takiwa kutolewa na serikali, rais wa jamuhuri Pierre Nkurunziza na mwenyekiti wa FNL tayari waliteuwa tume ambayo inafuatilia kwa karibu swala hilo na kulitafutia ufumbuzi.

vendredi 17 avril 2009

WANASENETI WA BURUNDI WAYAKATAA MAJINA KADHAA YALIOPENDEKEZWA NA RAIS KWENYE NYADHIFA TOFAUTI KARENGA RAMADHAN AKIWEMO.


Baraza la seneti nchini Burundi limejadili alhamisi hii April 16 majina ya watu waliopendekezwa na rais wa jamuhuri ya Burundi kwenye nyadhifa mbalimbali , ikiwa ni kwenye uongozi wa Mikoa kadhaa ya Burundi, aidha uwakilishi wa Burundi ugenini pomoja na kwenye uongozi wa jeshi la taifa.
Waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana alikuwa amewasilisha majina ya watu waliopendekezwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuongoza mikoa ya Makamba, Ruyigi na Kayanza.
Reverien Ndikuriyo alikuwa amependekezwa kuongoza Mkoa wa Makamba.
Fenele Nduwimana alipendekezwa kuongoza Mkoa wa Kayanza.na Syriaque Nshimirimana alipendekezwa kuwa gavana wa Mkoa wa Ruyigi. Majina ya waliopendekezwa kuwa wanabalozi wa Burundi ugenini ni , ni pamoja na Karenga Ramadhani aliewahi kuwa mkuu wa itifaki kwenye ofisi ya rais wa jamuhuri kabla ya kuwa waziri wa habari na msemaji wa serikali na hatimaye waziri anaye husika na uhusiano wa kikanda.
Mwingine ni Angel Niyuhire ambaye ni mbunge kutoka chama Uprona pamoja na Gahutu zacharie. Wakati huo waziri wa ulinzi meja jenerali Jermain Niyoyankana aliwasilisha majina ya Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye ni Naibu mkuu wa majeshi, alipendekezwa kuwa mkuu wa majeshi ya Burundi kuchukuwa nafasi ya Brigadia jeneral Samuel Gahiro alieteuliwa ku afisa wa kijeshi kwenye ubalozi wa Burundi mjini Tripoli. Mwingine ni meja jenerali Niyoyunguruza Juvenal aliependekezwa kuwa kaimi mkuu wa majeshi.
Miongoni mwa majina hayo, Juvenal Niyoyunguruza amekataliwa na wanaseneti kuwa naibu mkuu wa majeshi wakimtuhumu ya kwamba hayati Melchior Ndadaye rais wa kwanza wa Burundi kuchaguliwa chini misingi ya kidemokrasia aliuawa katika kambi ambayo alikuwa kamanda bila kuzuia mauaji hayo. Mwingine aliekataliwa ni Karenga Ramadhani, kuiwakilisha Burundi ugenini wanaseneti wakimtuhumu kwa matamshi aliyoyatowa wakati alipokuwa waziri wa habari na msemaji wa serikali kuhusu mkasa wa mauzo ya ndege ya rais Falcon 50, Naye Reverien Ndikuriyo amekataliwa kuongoza Mkoa wa Makamba baada ya jina lake kutajwa katika mkasa wa shirika la IDC lililo walaghai wananchi katika mikoa na kuwapora pesa .

vendredi 3 avril 2009

Waliomuua Lucky Dube wafungwa maisha


Jaji wa Afrika Kusini amewahukumu watu watatu kifungo cha maisha jela baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua mwanamuziki maarufu wa reggae Lucky Dube mwaka 2007. Lucky Dube aliyekuwa na umri wa miaka 43, alipigwa risasi na watu hao watatu katika jaribio la kumuibia gari lake katika kitongoji kimoja cha mjini Johannesburg, tukio lililoleta hofu kwa taifa hilo. Jamaa wa Lucky Dube walitokwa machozi na baadae wakashangilia baada ya kutolewa hukumu hiyo. wanamuziki pamoja na mashabiki walikusanyika nje ya mahakama hiyo kuonesha mshikamano wao. Mahakama hiyo ilielezwa kuwa washtakiwa hao watatu, walifikiria mtu waliyekuwa wakimpora gari alikuwa raia wa Nigeria na kamwe hawakufahamu waliyemuua alikuwa Lucky Dube hadi waliposoma magazetini siku iliyofuatatu hao watatu. Moja ya mabango nje ya mahakama hiyo lilikuwa likisomeka "Lucky Dube hafanani na Mnigeria; bali yeye ni Mwafrika." Mahakama hiyo pia imewahukumu Sifiso Mhlanga, Julius Gxowa, na Mbuti Mabe kifungo cha miaka 15 kila mmoja kwa kufanya jaribio la kupora gari la Lucky Dube.

mercredi 18 février 2009

VIONGOZI WA KANISA WAFIA MADARAKA MBELE YA WAUMINI WAO

Hali ya kutoelewana imekuwa ikijitokeza mnamosiku zote hizi za nyuma baina ya viongozi wa kanisa la kimethodist unies katika sehemu mbalimbalia za Burundi.Tukio la karibuni ni la Hivi majuzi Mkoani Gitega viongozi wa kanisa hilo walitwangana ngumi na kuzusha vurumai na hivo kuvuruga usalama wa raia katika Mkoa huowa Gitega, pindi walifikia hali ya kuvurumishiana mawe. Kulingana na waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana amesema kuwa inaskitishwa kuona watu ambao wangelipooza nyoyo za waumini kwa kuwahutubia neno la Mungu na kuleta maendeleo, sasa ndio ambao wanavuruga usalama. Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema kuwa walichukuwa hatuwa ya kufunga kanisa hilo baada yakutokea vurumai hizo hadi pale juhudi za upatanishi zitafikia tamati, waliopigana nao waliwekwa nguvuni na vyombo vya uslama kabla ya kufunguliwa faili na vyombo vya sheria. Waziri Edourd Nduwayo ameomba viongozi wa makanisa kuheshimu sheria zao na watakumbwa na sheria ya mwaka 1992 inamaanisha kwamba watachukuliwa hatuwa kama mashirika mengine. Amesisitizia viongozi hao wa makanisa kuheshimu sheria na kuweka mbele maendeleo na marisdhiano ya wananchi badala ya kutia mbele vyeo. Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema kuwa kwa sasa watu wamekuwa wakishangazwa na kujiuliza vipi wahubiri sasa ndio wafia vyeo wakati cheo ni dhamana. Amesema wamo mbioni kuendesha mikutano na viongozi mbalimbali wa makanisa ili wawahamasishe kuhusu kutia mbele maridhiano badala ya kufarakiana na ilihali ni viongozi.

VIONGOZI WA KANISA WAFIA MADARAKA MBELE YA WAUMINI WAO

Hali ya kutoelewana imekuwa ikijitokeza mnamosiku zote hizi za nyuma baina ya viongozi wa kanisa la kimethodist unies katika sehemu mbalimbalia za Burundi.Tukio la karibuni ni la Hivi majuzi Mkoani Gitega viongozi wa kanisa hilo walitwangana ngumi na kuzusha vurumai na hivo kuvuruga usalama wa raia katika Mkoa huowa Gitega, pindi walifikia hali ya kuvurumishiana mawe. Kulingana na waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana amesema kuwa inaskitishwa kuona watu ambao wangelipooza nyoyo za waumini kwa kuwahutubia neno la Mungu na kuleta maendeleo, sasa ndio ambao wanavuruga usalama. Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema kuwa walichukuwa hatuwa ya kufunga kanisa hilo baada yakutokea vurumai hizo hadi pale juhudi za upatanishi zitafikia tamati, waliopigana nao waliwekwa nguvuni na vyombo vya uslama kabla ya kufunguliwa faili na vyombo vya sheria. Waziri Edourd Nduwayo ameomba viongozi wa makanisa kuheshimu sheria zao na watakumbwa na sheria ya mwaka 1992 inamaanisha kwamba watachukuliwa hatuwa kama mashirika mengine. Amesisitizia viongozi hao wa makanisa kuheshimu sheria na kuweka mbele maendeleo na marisdhiano ya wananchi badala ya kutia mbele vyeo. Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema kuwa kwa sasa watu wamekuwa wakishangazwa na kujiuliza vipi wahubiri sasa ndio wafia vyeo wakati cheo ni dhamana. Amesema wamo mbioni kuendesha mikutano na viongozi mbalimbali wa makanisa ili wawahamasishe kuhusu kutia mbele maridhiano badala ya kufarakiana na ilihali ni viongozi.

vendredi 13 février 2009

WIZI WA KUTUMIA SILAHA WAKITIHIRI KUSINI MWA BURUNDI

Usalama mdogo unaripotiwa katika kiji cha Canda tarafani kayogoro katika mkoa wa kusini wa Makamba .Duru tawala zinasema wizi wa kutumia silaha na mitego ya kuvizia magari vimeibuka katika sehemu hiyo. Gavana wa mkoa wa makamba Pasteur BUCUMI ameiambia idhaa hii kuwa hivi majuzi polisi imefaulu kukamata guruneti , silaha moja na sare za kijeshi kwenye msako uliofanyika tarafani hapo Kayogoro. Ameongeza kuwa uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa wahalifu wanatokea katika mkoa jirani wa Bujumbura vijijini.
jirani ya hapo tarafani Rumonge mkoani Bururi, Raia mmoja mfanyabiashara kwa jina Amissi Mpitabakana ameporwa kitita cha pesa zinazokadiriwa miloni 5 na laki 3 za shillingi , sarafu ya Tanzania. Kulingana na muandishi wa habari wa shirika la Burundi la habari ABP sehemu hiyo, mfanyabiashara huyo alikuwa anajiandaa kusafiri na kitita hicho hadi Tanzania kwenda kulangua bidhaa za kuuza.

MASHIRIKA YA KICHINA YAZIDI KUJIZATITI NCHINI BURUNDI

Machimbo ya Nishati ya Nickel ya Musongati kusini mwa nchi yamekabidhiwa shirika lipya la SAMANCOR kutoka Uchina. Serikali ya Burundi ndio tu imetoa kwa shirika hilo kibali cha utafiti na shughuli za machimbo zimepangwa kuanza mnamo kipindi cha miaka miwili ijayo.
Hayo yamefahamishwa na waziri wa BDI wa nishati na madini Samuel Ndayiragije. Waziri huyo amesema uwanja huo wa machimbo ya madini ya Nickel ulikuwa wazi baada ya serikali ya Burundi kuvunja kandarasi ya shirika la Andover tangu mwaka 2007.

WAALIMU WA BUTERERE WAANZISHA MGOMO

Waalimu wa shule za msingi na upili tarafani Buterere kaskazini mwa jiji la Bujumbura wameanzisha mgomo wa kususia kutoa visomo wakidai wapewe kwanza viwanja vya ujenzi walivyoahidiwa na serikali. Waalimu hao wanaojumuika kwenye mashirika ya waalimu ya STEB na CONAPES wanaonyeshea hasa kidole Baraza la madiwani tarafa hapo ,kugawa viwanja hivyo kwa watu binafsi badala ya kuwapatishia waalimu. Mwenzangu Karim Nkeshimana amezungumza na Jean Bosco Ndarusanze , mwalimu wa shule la upili wa Buterere. Pamoja na mgomo huo , kazi ya dharura imekuwa inafanywa ikiwa ni pamoja na kutoa visomo kwa wanafunzi wa madarasa ya sita na ya kumi yanayotahiniwa kitaifa. Tumejaaribu kuwasiliana na wakuu wa tarafa ya Buterere kutoa muanga zaidi kuhusiana na hali hiyo pasina mafaanikio.

WAGANGA NA WAUGUZI WATISHIA KUREJEA MGOMONI

Vyama vya wauguzi na waganga vimetishia kuanzisha tena mgomo kuanzia jumatatu ijayo,.Mkuu wa chama cha madakatari Pierre Claver Hajayandi amesema kwamba mapatano yaliofikiwa kati yao na serikali hayakutekelezwa .Nae mmoja wa wapatanishi kwenye ugomvi kati ya serikali na mashirika hayo ya waganga, Rais wa zamani wa Burundi Sylvestre Ntibantunganya ameahidi kutoa muanga zaidi kuhusiana na mzozo huo jumamosi Februari 14.

USALAMA BADO WAYUMBISHWA RUYIGI

Gari ya hospital ya mkoa wa cankuzo imeanguka jana jioni alhamisi 12.2.209 kwenye mtego wa watu wenye silaha tarafani bweru katika mkoa wa mashariki wa Ruyigi. Kulingana na muandishi wa shirika la Burundi la habari sehemu hiyo watu waliokuwa wanavalia sare za kijeshi wamepora fedha inayokadiriwa laki sita na mtambo wa kemikali unaokadiriwa kuwa na thamani ya franka milioni 5.

dimanche 18 janvier 2009

MAANDAMANO YA WAISLAM NCHINI BURUNDI YAPIGWA MKASI NA MEA WA JIJI

Waislam nchini Burundi walikuwa wamepanga kuendesha maandamano makubwa mjini Bujumbura kwa ajili ya kuwaunga mkono raia wa Palestina wanaokumbwa na matatizo wakati huu ya kuawawa kinyama huko Gaza na majeshi ya Israel. kama ilivyokuwa kawaida katika sheria na kanuni za kuendesha maandamano mea wa jiji ndie hutowa ruhusa ya kuendesha maandamano. Ombi la waislam kuendesha maandamano lilikataliwa na mea wa jij la Bujumbura Evrar GISWASWA ambae hata hivo hakutowa sababu yoyote. ilikuwa kero kubwa kwa waumini wa dini ya kiislam kukataliwa kwa maandamano hayo ambayo walikuwa wamepanga kuyanednesha katika hali baridi na tulivu. walichukuwa uamuzi wa kuendesha maandamamano hayo ndani ya majengo ya muskiti mkuu jijini Bujumbura, na baadae kugeuza uamuzi huo. haieleweki kwa nini waislam wa Burundi ndio wakataliwe kuendesha maandamano ya kupinga mashambulizi dhidi ya wayahudi dhidi ya wa Palestina, wakati ambapo ulimwengu mzima kumekuwa kukishuhudiwa maandamano ya aina hiyo ikiwemo Marekani na hata Israel kwenyewe.

jeudi 1 janvier 2009

WAFUNGWA WA PALIPEHUTU-FNL WATAACHIWA HURU HIVI KARIBUNI

Tarehe 31 Desemba mwaka 2008 ilikuwa imetolewa kama tarehe ya mwisho kwa pande zinazo jadiliana, yaani serikali ya Burundi na palipehutu FNL wawe wamemaliza mjadala. Uongozi wa kisiasa unaohusika na kufuatilia kwa karibu utekelezwaji wa makubaliano ya tarehe 4 Desemba baina ya serikali ya Burundi na palipehutu-FNL unaoongozwa na balozi wa afrika kusini nchini Burundi Kingsley Mamabolo umetowa tamko ambamo umesema kuendelea vema kwa majadiliano baina ya pande 2 ilikuondowa vizingiti vyote vinavyo zuia utekelzwaji kivitendo mkataba baina ya palipehutu FNL na serikali ya Burundi. Taarifa hiyo imefahamisha kwamba Kampeni ya palipehutu FNL kwa wanachama wake ili kufasiria juhudi za kubadili jina zitafanyika januari 3. juhudi za ujenzi wa kituo kingine cha kuwakusanya wapiganji wa palipehutu FNL cha Rubira zinaendelea kufanyika, na wapiganajiwa palipehutu FNL wataachiwa huru hivi karibuni. Uongozi huo wa kisiasa unaofuatilia kwa karibu utekelezwaji kivitendo mkataba wa tarehe 4 Desemba umezitaka pande mbili yaani seriklai ya Burundi na paliephutu FNL kuendelea kuonyesha utashi wa kutekeleza kivitendo mkataba huo. Kwa mujibu wa kanali Lazare Nduwayo wa tume inayo fuatilia kwa karibu utekelezwaji mkataba wa kusistisha mapigano MCVS amefahamisha kuwa hatuwa ya kuwaacha huru wafungwa wa kisisasa wa palipehutu FNL ilisainiwa jana. Sheria hiyo itapelekea kuachwa huru kwa wafungwa 246 wa palipehutu FNL