vendredi 3 avril 2009

Waliomuua Lucky Dube wafungwa maisha


Jaji wa Afrika Kusini amewahukumu watu watatu kifungo cha maisha jela baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua mwanamuziki maarufu wa reggae Lucky Dube mwaka 2007. Lucky Dube aliyekuwa na umri wa miaka 43, alipigwa risasi na watu hao watatu katika jaribio la kumuibia gari lake katika kitongoji kimoja cha mjini Johannesburg, tukio lililoleta hofu kwa taifa hilo. Jamaa wa Lucky Dube walitokwa machozi na baadae wakashangilia baada ya kutolewa hukumu hiyo. wanamuziki pamoja na mashabiki walikusanyika nje ya mahakama hiyo kuonesha mshikamano wao. Mahakama hiyo ilielezwa kuwa washtakiwa hao watatu, walifikiria mtu waliyekuwa wakimpora gari alikuwa raia wa Nigeria na kamwe hawakufahamu waliyemuua alikuwa Lucky Dube hadi waliposoma magazetini siku iliyofuatatu hao watatu. Moja ya mabango nje ya mahakama hiyo lilikuwa likisomeka "Lucky Dube hafanani na Mnigeria; bali yeye ni Mwafrika." Mahakama hiyo pia imewahukumu Sifiso Mhlanga, Julius Gxowa, na Mbuti Mabe kifungo cha miaka 15 kila mmoja kwa kufanya jaribio la kupora gari la Lucky Dube.

1 commentaire:

EWL a dit…

Hello from Penang Island, Malaysia.

I am missing 28 countries to complete my worldwide collection of postcards and one of the missing countries is Burundi.

You can see my postcard quest at http://smspostcard.blogspot.com/

Hope to hear from you. Thank you.