samedi 12 septembre 2009

WANASIASA NCHINI BURUNDI WATOFAUTIANA KUHUSU SHERIA YA UCHAGUZI

BUJUMBURA: Kumekuwa na hisia tofauti baina ya wanasiasa nchini Burundi kuhusiana na sheria ya uchaguzi iliopasishwa bungeni usiku wa alhamis kuamkia ijumaa septemba 11, 2009. Chama Sahwanya FRODEBU kimesema kufurahishwa na hatuwa hiyo ya kupasisha sheria ya uchaguzi bungeni, lakini hata hivo mwenyekiti wa chama SAHWANYA FRODEBU Leonce Ngendakumana amesema kuwa na wasiwasi hasa kwamba kadi moja ya uchaguzi iliokuwa ikitetewa na chama hicho haikupasishwa kaika muswada huo. upande wake msemaji wa chama FNL Bosco HAVYARIMANA amesema kuwa wabunge wamekwenda kinyume kabisa na maafikiano waliokuwa wamekubaliana siku za nyuma. kiongozi huyo amesema kuwa kiwango cha dhamana kinacho takiwa kwa wagombe viti mbalimbali vya uchaguzi hakina sababu za kuwepo. upande wake mwenyekiti wa chama CNDDLéonard Nyangoma amesema ni aibukubwa sana kwa taifa la Burundi. upane wake amesema sheria hiyo ya uchaguzi inakuja kurejesha nyuma hatuwa za demokrasia nchini Burundi ukilinganisha na sheria.

BAADA YA MVUTANO WA SIKU NZIMA, HATIMAE WABUNGE WAMEPASISHA SHERIA ZA UCHAGUZI SAA TISA USIKU

BUJUMBURA le 11.9.2009:Hatimae wabunge nchuini Burundi wamepasisha muswada wa sheria uhusuo uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Tangu saa tatu asubuhi alhamis Septemba 2009, wabunge walitakiwa kujadili na kupasisha muswada wa sheria uhusuo sheria za uchaguzi nchini Burundi. Kutokana na utata uliokuwemo katika sheria hizo, ilikuwa vigumu kupatikana muafaka, hadi saa tisa usiku wa kuamlia ijumaa septemba 11, wabunge walifikia muafaka na kusaini sheria zihusuzo uchaguzi wa 2010. miongoni mwa walioafikiana ni pamoja na mpangilio wa uchaguzi utaoanzia kwa viongozi wa madiwani na baadae kufuatia uchaguzi wa rais, utaofuatiwa na na wa bunge na seneti na kuhitimishwa kwa ule wa viongozi wa ngazi za china. Ama kuhusu kadi ya uchaguzi, wanasiasa hao wameafiki kutumia kadi tofauti na vijisanduku 2. kimoja kitapokea kadi iliopiga kura na nyingine itayo tupwa katika kijisanduku maalum kitachokuwa kimeandaliwa. Ili kuepusha wizi na udanganyifu, kadi zote zitahesabiwa, zile zilizo chaguliwa na zile zilizo tupwa sehemu kutakokutikana na udanganyifu sehemu hiyi uchaguzi utafutwa na baadae kuandaliwe mwingine katika kipindi kisichozidi siku 5. kuhusiana na dhamana anayo takiwa kutowa mgombea kiti cha urais imesalia kuwa franka za Burundi millioni 15, pesa hizo zitarejeshwa iwapo mgombea hatofikisha asilimia 5 ya kura zitazopigwa nchi nzima. Mgombea kiti cha ubunge atalipa dhamana inyo lingana na franka za Burundi laki 5 huku , mgombea kiti cha uanaseneta akilipa franka za Burundi laki 4. Pesa hizo zitarejeshwa iwapo wagombea hao hawatofikisha asilimia 2 ya kura zitazopigwa kote nchini. Wabunge walikubaliana pia kuhusu kufutwa ubunge kwa mbunge ataekuwa amekitoroka chama chake na kujiunga na chama kingine swala ambalo lililo zusha utata, hatimae wabunge wamekubalina na swala hilo.

mercredi 9 septembre 2009

KUKOSEKANA KWA SHERIA JUU YA UCHAGUZI NCHINI BURUNDI KWA CHELEWESHA SHUGHULI ZA TUME HURU YA UCHAGUZI CENI.

Bunge nchini Burundi limeahirisha kwa mara ya tena kikao cha dharura kilichoititishwa na rais wa jamuhuri tangu jumatatu iliopita. Wabunge walitakiwa kujadili jumatano hii muswada wa sheria uhusuo sheria za uchaguzi wa 2010 unaosubiriwa na wengi nchini Burundi. Spika wa Bunge Pie Ntavyohanyuma ameskika akisema kuwa kuna umuhimu wa kuahirisha muswada huo wa sheria ukizingatia kuwa hakujapatikana muafaka kuhusu baadhi ya vipengee. Baadhi ya yanayo leta utata na kupelekea wanasiasa kutoelewana ni pamoja na orodha ya utaratibu mzima wa uchaguzi utavyo fanyika. Chama tawala CNDD-FDD kinataka uchaguzi uanzie juu, yaani uchaguzi wa rais, huku vyama vingine vikitupilia mbali pendekezo hilo. Pia, kadi ya uchaguzi, wanasiasa wanaomba iwe moja kwa vyama vyote vitavyo jikita katika mlolongo wa uchaguzi wakati ambapo chama tawala CNDD-FDD kikiomba pawepo na kadi tofauti kwa kila chama. Swala la dhamana pia linazusha utata ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2005 mgombea kiti cha urais alitakiwa kilipa franka za Burundi milioni 3, lakini mwaka huu wa 2010 mgombea kiti cha urais anatakiwa kulipa franka za Burundi milioni 15. Swala la msamaha wa muda uliotolewa miaka ya nyuma kwa viongozi waliohusika kwa njia moja ama nyingine na machafuko nchini Burundi linazuia pia tafrani. Kukosekana kwa sheria juu a uchaguzi kunachelewesha shughuli za tume ya uchguzi CENI kuanza kazi zake. Wabunge wamepanga kukutana tena alhamis septemba 10/9/2009 kujaribu kutafuta muafaka kuhusu sheria juu ya uchaguzi.

MAZOEZI YA PAMOJA YA KIJESHI YA NCHI ZA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI YA ZINDULIWA NCHINI TANZANIA

Rais wa Tanzania Jakaya Mrishio kikwete amezindua rasmi mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya nchi za jumiya ya Afrika mashariki huko Monduli, Mkoani Arusha jumanne 8.9.2009 asubuhi. Baadhi ya makamanda waandamizi wa majeshi ya nchi za Afrika Mashariki wanashiriki katika mazoezi hayo ya pamoja kutoka katika kilima cha Nodosoito huko monduli mkoani Arusha. Burundi, Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya ni nchi wanachama wa jumuia hiyo ya Afrika mashariki. Kama unavyo ona kwenye picha ma kamanada wa kijeshi kutoka nchi hizo wakimuonyesha rais Jakaya Mrisho Kikwete sehemu kutako endeshewa mafunzo hayo.

POLISI YA USALAMA WA RAIA HAIJA FAULU KUWAKAMATA MAJAMBAZI WALIOJARIBU KUMMALIZIA MAISHA MSANII JOHN CHRIS


Hadi sasa polisi haijafaulu kuwakamata watu waliojaribu kummalizia maisha msanii John Chris wakati wa likizo yake mjini Bujumbura. John Chris alinusurika katika tukio lililo endeshwa na watu ambao hawajajulikana katika usiku wa kuamkia jumanne Septemba Mosi mwaka huu. Kama alivyo eleza mwenyewe kwenye Vyombo vya habari Msani huyo mwenye asili ya Burundi ambae sasa anaishi Mjini Bruxels Ubelgiji alikuwa pamoja na familia katika sherehe za kuagana kwa kuwa alikuwa amehitimisha likizo yake mjini Bujumbura, wakati alipo toka akiwa na walinzi wake 2, alijieleza sehemu kujisaidia, alipo rudi ndipo akakuwa watu 2 waliokuwa na bastola tayari kuziweka kichwani kwa walinzi aho ambao walikuwa ni askari polisi waliovalia nguo za kiraia. Alipo fika nae akawekwa bastola kichwani na kuambiwa aondowe kila kilicho mfukoni mwake, hakusita kufanya hivo kama alivyo eleza. Lakini mmoja kati ya walinzi wake alijaribu kujiokowa kwa kuridi nyuma ili apate jinsi ya kutowa bastola ambayo aliokuwa nayo ili awashambulie majambazi hao, huku mwengine akimsukuma msanii huyo kama kumponyesha. Mmoja kati ya majambazi hao alirusha rusase zikampata mmoja kati ya walinzi kwenye mbavu. Majamabazi hao walitimka baada ya kuona kwamba mambo yamekuwa magumu. Askari polisi huyo afya yake sio mbaya anaendelea kupata matibabu kwenye Hospitali mojawapo jijini Bujumbura.