mardi 21 avril 2009

VITISHO DHIDI YA MWENYEKITI WA SHIRIKA LA KIRAIA LA OLUCOME NCHINI BURUNDI.

Gabriel Rufyiri mkuu wa shirika linalo jihusisha na upigaji vita rushwa na uporaji mali ya umma nchini Burundi OLUCOME ameviambia vyombo vya habari nchini Burundi kwamba siku zote hizi za nyuma amekuwa akipokea simu za watu asio wafahamu ambao wamekuwa wakimtisha na kumtia hofu. Kiongozi huyo amesema tayari amefikisha ripoti kwa hakimu mkuu wa jamuhuri jijini Bujumbura, hadi sasa amesema hajapata jibu lolote. Upande wa polisi kupitia msemaji wake Chanel Ntarabaganyi ameomba Rufyiri atowe namba za simu wanazo tumia watu hao wanaomtia hofu ili waendeshe uchunguzi. Kuhusu uchunguzi wa mauaji ya kifo cha aliekuwa naibu kiongozi wa shirika la OLUCOME Ernest MANIRUMVA alieuawa kikatili siku zilizopita na watu siojulikana bado, msemaji wa jeshi la Polisi nchini Burundi Pierre Chanel NTARABAGANYI amesema kuwa hadi sasa tume ya uchunguzi ilioundwa inaendeleza shughuli zake, na tayari imeomba msaada wa kikosi cha polisi kutoka ugenini itayo saidia katika kuendesha uchunguzi wakitumia ujuzi wa hali ya juu.

Aucun commentaire: