jeudi 25 mars 2010

SILAHA ZILIZOMO MIKONONI MWA RAIA ZAENDELEA KUMALIZA MAISHA YA WANANCHI

Watu 3 wameuawa Mkoani Kirundo katika kijiji cha Renga zone ya Mukerwa tarafa ya Busoni katika usiku wa kuamkia alhamisi hii saa tatu na robo pindi majambazi waliokuwa na silaha walipo vamia familia moja. Miongoni mwa hayati hao ni baba na mkewe pamoja na mama yake. Katika tukio hilo dada wa hayati huyo alijeruhiwa.

Usalama mdogo umeripotiwa pia katika kijiji cha Migera Mkoani Nyabihanga. Watu wzenye silaha waliivamia nyumba ya mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la Ntabahungu Gaspard. Baada ya kuwajeruhi watu 2 na risase wahalifu hao ndipo walianza kuwapora watu simu za mkononi, redio na pesa ambazo haijulikani idadi yake. Katika usiku huohuo mwananchi Nkurunziza Evariste wa kijiji cha Bugera tarafani Ndava alipigwa risase na wahalifu magotini na baadae wakatimka.

mardi 9 mars 2010

MGOMO WA WAALIMU WAINGIA KATIKA SIKU YAKE YA PILI

BUJUMBURA:Mgomo wa waalimu wa shule za serikali kuisusia kazi leo umeingia katika siku ya pili.Shule nyingi zinazo patikana katika manispaa ya jij la Bujumbura zimefunga milango yake. Baadhi ya shule hata hivo hapa Mjini Bujumbura kama shule la kinama la msingi la kinama ya pili ni waalimu wachache pekee wanaofanya kazi. Hali kadhalika mgomo wa waalimu unatikisa shule za mikoani.Lakini tunaarifiwa kwamba Shule la kipili la mtakatifu Therese mkoani Gitega wanaofanya kazi ni waalimu wa kigeni.
Wakati huo huo Muungano mpya wa vyama vya waalimu katika shule za msingi SEEPBU unasema licha ya kwamba hawakujiunga na mgomo hata hivo wanaungana na madai ya waalimu ya masalia ya fedha katika upangiliaji upya wa vyeo vya waalimu.
Hata hivo mkuu wa chama hicho cha waaalimu SEEPBU Victor Nbabaniwe anasema wanatofautiana na wenzao kuhusu utaratibu wa kudai haki.Anasema inafaa kutumia majadiliano na serikali badala ya kuweka mgomo mbele. Hata hivo ameiomba serikali kuweka kwenye vitendo ahadi za waaalimu.

VIONGOZI WA MKOA WA KAYANZA WAMEPIGA MARUFUKU WAGENI KUINGIA NA WANAFUNZI KUTOKA KATIKA SHULE LA KIPILI LA KAYANZA

BUJUMBURA:Wakuu wa mkoa wa Kayanza wamechukua hatua kali za kiusalama katika shule la kipili la Kayanza baada ya kuripotiwa hali ya mtafaruku baina ya wanafunzi ,kukiwa ba chuki za chini kwa chini za kikabila na kisiasa.
Hatua hizo ni pamoja na kupiga marufuku nenda-rudi za wanafunzi,kupokea wageni shuleni hapo aidha kuondoka nje ya shule.Pia matumizi ya simu za mkononi yamepigwa marufuku.
Kwa mujibu wa muandishi wa habari wa radio Burundi mkoani hapo, Gavana na mkuu wa tarafa ya Mkoa wa Kayanza pamoja na wakuu wa usalama walikuwa jumatatu hii shuleni hapo kutuliza nyoyo wanafunzi na kuwaasa kujiepusha na hisia zote za mtengano zinazoweza kutishia usalama wa shule na wanafunzi
Mkoani Gitega nako tunaarifiwa kwamba wakuu wa shule la kipili la Notre Dame de la Sagesse maarufu CND wamechukua hatua ya kuwafuta wanafunzi sita wakituhumiwa kwamba wamekuwa wanawashawishi wanafunzi shuleni hapo wasitumie chakula cha maharagwe ambayo yanadaiwa kwamba sio mazuri.