mercredi 16 juillet 2008

PALIPEHUTU/FNL WAPEWA CHAKULA KWA MARA NYINGINE TENA.


Bujumbura le 14/7/2008. Shughuli za kuwapa chakula wapiganaji wa palipehutu/FNL zimeanzishwa tena jumatatu hii. Hayo yamefahamishwa na msemaji wa kundi hilo Pasteur HABIMANA. Akizungumza katika mahojiano kupitia njia ya simu kwenye redio Burundi, Pasteur HABIMANA alisema kuwa muakilishi wa msuluhishi nchini Burundi Kingslay Mamaboulo alishindwa kuzibiti hali ya mambo wakati alipo safiri muakilishi maalum wa umoja wa Afrika nchini Burundi Mamadou Ba na kutofahamisha mapema kwamba chakula kiliopo kimekwisha. Kusitishwa kwa shughuli hizo kulipelekea wapiganaji wa palipehutu/FNL kuingia ndani ya majumba ya raia na kupora chakula. Msemaji wa palipehutu/FNL ameitolea mwito jamii ya kimataifa kuongeza idadi ya chakula wanacho pewa wapiganaji wa kundi hilo wakati huu. Kama alivyo fahamisha, kila mpiganaji hupewa chakula mara moja kwa siku, sawa na kilo 4 kwa wiki.



WATUHUMIWA 6 WA MAUAJI YA DACTARI KASSY MANLAN WAACHIWA HURU.


Bujumbura le 14/7/2008 Watuhumiwa 6 wa mauaji ya aliekuwa muakilishi mkaazi wa shirika la afya ulimwenguni nchini Burundi, Dactari Kassy Manlan, wameachiwa huru. Korti kuu ya sheria iliamuru watuhumiwa hao wafunguliwe tangu juni 12, baada ya kufungwa kwenye jela kuu la Mpimba tangu Novemba 2003. watuhumiwa hao 6 ambao ni pamoja na Gerard ntunzwenayo, Emile Manisha, Aloys Bizimana, Japhet Ndayegamiye, Expert Bihumugani na Athanase Bizindavyi, wamebaini kuridhishwa na kufunguliwa kwao. hata hivo Pierre Claver Mponimba kiongozi wa shirika linalo tetea haki za wafungwa amesema kwamba kufunguliwa kwa watuhumiwa hao ni pigo kubwa kwa vyombo vya sheria nchini Burundi, kiongozi huyo amebaini kuwa kesi hiyo lazima ifikie kileleni na wahusika lazima watambulike. Jamii ya warundi wanajiuliza wakati huu kuhusu hatma ya kesi hiyo baada ya watuhumiwa hao kukutwa bila hatia. Upande wake Wakili Marc BIRIHANYUMA amesema kusikitishwa kuona vyombo vya dola na vile vya sheria vimeshindwa kuendesha uchunguzi kama ipasavyo kuhusu kifo cha hayati Kassy Manlan ili warundi na jamii ya kimataifa watambuwe ukweli zaidi kuhusu kifo hicho ambacho kina tatanisha. Inavyo dhihirika wakati huu, utafkiri kwamba hayati Manlan alijiua mwenyewe na baadae kenda kujitupa katika ziwa tanganyika, amesema hayo mwanasheria huyo.
KIONGOZI ZAMANI WA SHULE LA GATABO MKOANI MURAMVYA AUAWA NA MTU ALIE VALIA SARE ZA KIJESHI.

kiongozi zamani wa shule la upili la tarafa ya GATABO Jean Claude NSHIMIRIMANA ameuawa katika usiku wa jumatatu kuamkia jumanne nyumbani kwake na mtu aliekuwa amevalia sare za kijeshi ambae hadi sasa hajatambulika. Mauaji hayo yametokea katika kata ya Kigwati inayo patikana mjini kati Muramvya. Kwa mujibu wa Muandishi habari wa kituo cha kutawanyia habari Mkoani Muramvya ABP, Philippe SENDAZIRASA, hayati huyo aliuawa muda mfupi wakati aliporejea nyumbani kwake, ghafla amimuona muhalifu anaingia ndani na ambae alimfahamisha kuwa amekuja kummalizia maisha, papo hapo alichomoa bunduki aliokuwa nayo aiana ya bastola na kumpiga risase 3 kichwani. Hayati Jean Claude NSHIMIRIMANA hadi sasa alikuwa mwalimu kwenye shule la upili la Shombo katika tarafa ya Muramvya.


ALAIN MUGABARABONA KIONGOZI ZAMANI WA FNL/ICANZO KAITOROKA NCHI.

Mugabarabona mwenyekiti zamani wa chama cha FNL/ICANZO ambae alikatiwa kifungo cha miaka 20 jela kutokana na shutma za kutaka kuipiduwa serikali ya Burundi asadikiwa kuitoroka nchi katika mazingira ambayo yanatatanisha. Kutoroka kwa Dk Alain Mugabarabona hakuthibitishwi wala kukanushwa na mkurugenzi mkuu wa jela kuu la Mpimba Afisa Victor Segasago, kwa kuwa mfungwa huyo alikuwa amepewa ruhusu ya kuzuru nyumbani kwake ili kutatua matatizo yaliokuwa yakiripotiwa katika familia yake. Kama alivyo fahamisha afisa huyo, Kibali cha kutoka jela kilikuwa kimetolewa na mkurugenzi mkuu wa magereza Anaclet Gasamirwa, ilikuwa tarehe 17 juni iliopita. Kuliko kurejea katika jela kuu la Mpimba, Alain Mugabarabona alipewa kibali kingine cha siku 15 na mkurugenzi huyo wa magereza Anaclet Gasamirwa kama inavyo agizwa na sheria za mambo ya ndani za magereza. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa Mpimba Alain Mugabarabona anatakiwa kurejea katika jela kuu la Mpimba leo saa kumi na moja majira ya hapa nyumbani. Iwapo hatorudi shutuma zote atazibeba yule ambae aliemuwekea dhamana nae si mwengine ni wakili wake Jean Bosco Nyakiki, ambapo mkurugenzi mkuu wa jela kuu la Mpimba alionyesha faili alizo saini wakili nyakiki. Itafahamika kuwa muda wote aliopewa kibali cha kutoka nnje ya jela kuu la Mpimba Dk Alain Mugabarabona hakuwa na walinzi. Mtu mwingine ambae anasadikiwa kuwa kaitoroka nchi ni Gérard NGENDABANKA aliwahi kuwa hakimu mkuu wa jamuhuri, ambae inasadikiwa kuwa anatambuwa mengi zaidi kuhusu kifo cha hayati Dk Kassy Manlan muakilishi mkaazi wa shirika la Afya ulimwenguni OMS alieuliwa nchini hapa mwaka 2001. Washukiwa wa mauji hayo waliachiwa huru kwa kukutwa bila hatia.

mercredi 9 juillet 2008

BUJUMBURA LE 9.7.08. SERIKALI YA BURUNDI YA WAASA WAPIGANAJI WA PALIPEHUTU/FNL KUMALIZA HARAKA MPANGO WA KUWAKUSANYA WAPIGANAJI WAKE KWENYE VITUO TEUL

Serikali ya Burundi kupitia msemaji wake bibi Hafsa MOSSI akiwa pia waziri wa habari na ushirikiano wa bunge la Burundi, imetangaza kuhusu msimamo wa Palipehutu/FNL

HABARI ZA SIASA

Bujumbura le 8.7.08. LICHA YA MATATIZO YA UKOSEFU WA LISHE YA KUTOSHA WAPIGANAJI WA PALIPEHUTU/FNL WASEMA KU GANGA NJAA.
Wapiganaji wa palipehutu/FNL walioko katika kituo teule cha huko Mkoani Bubanza tarafani Rugazi, wanakabiliwa na matatizo ya uhaba wa chakula. Kama tulivyo shuhudia Kwenye eneo hilo liliotengwa kuwapokea wapiganaji wa kundi la palipehutu/FNL la hapo Rugazi, ni kwenye umbali za kilomita zaidi ya 20 hivi ukitokea katika kijiji cha Muzinda. Kambi hiyo yawajumuisha wapiganaji 155 ambao wanalindwa na askari wa Afrika kusini. Ukifika eneo hilo utawakuta wapiganaji wa palipehutu FNL wamo ndani yake, waki randa randa bila kuwa na lolote la kufanya huku wengine wakifua nguo zao wengine wakicheza kisoro. Wapiganaji hao hawana silaha, lakini kiasii ya wengi wanavalia sare za kijeshi. Kila anae taka kutoka nnje ya kambi hiyo hupewa kibali na kiongozi wa wapiganaji kambini humo. Duru kutoka kambini hapo zaarifu kuwa wanayo matatizo ya kupata lishe ya kutosha, wapiganaji hao hupewa chakula mara moja kwa siku yaani kwa wiki kila mmoja hupewa kilo 4 za chakula ambazo imeendelea kuarifuduru hiyo kiasi hicho hakitoshi hata kidogo lakini hata hivo wanavumilia. Duru hiyo imeeeleza pia matatizo ya ukosefu wa madawa, yale wanao pewa ni ya kutibu vidonda ambavyo wakati huu vita ilisimama hakuna wanaouumia. Mbali kidogo na eneo hilo kama kilometa 15 ukielekea katika msitu wa Kibira katika mlima wa Kibuye, kuna kambi nyingine ya wapiganaji ambayo ilitengwa ya wale ambao wanajiandaa kuelekea katika kambi iitwayo ya Cantonnement iwapo majadiliano yataendelea vizuri. Ukifika eneo hilo utawakuta wapiganaji wengi kwenye barabara ya mlima huo na hata juu ya mlima utakuta tujumba twa misonge ambato wameanza kujenga, hii ni baada ya kukumbwa na matatizo ya kunyeshewa na mvua kubwa zilizo nyesha wiki iliopita ilioharibu vitu walivyokuwa navyo kama vile unga. Wengi wao wanazo silaha mikononi. Wapiganaji hao wanaskitishwa kuona hawajapewa maturubai hadi sasa, wanashinda na jua lao, mvua yao. Wamearifu kwamba pindi walipokuwa msituni walijitegemea kwa kila kitu, lakini wakati huu katika hali ya kuheshimisha majadiliano wanakubali kuvumilia hali hiyo, kwa kuwa wamearifu hawajafikia kuishi maisha mazuri, bado wanaendesha maisha waliokuwa nayo wakati wa mapambano. Hata hivo wamesema kuwa na wasiwasi kutokana na matamshi ya wanasiasa. Wananchi wa maeneo hayo wamearifu kueshi vizuri na wapiganaji hao licha ya kujitokeza mara kadhaa vitendo ambavyo wamesema imekua vigumu kuthibitisha kwamba ni wapiganaji hao ndio wanaohusika ao la. Wananchi wa maeneo hayo wanafurahishwa na hatua ambayo imekwisha pigwa na hivo wametolea mwito wanasiasa kuendeleza mazungumzo ili kufikia kikomo cha mazungumzo katika hali ya muafaka. Wapiganaji hao wameomba wapewa vifaa mahitajio muhimu kama vile chakula cha kutosha na madawa kwa kuwa iwapo itafikia wasitishe kuwapa chakula silaha bado wanazo na hazijaziba, wataendelea kueshi kama walivyokuwa wakieshi wakati wa mapambano.
BIOGRAPHIE
NDUWIMANA Didier A.k.a Sugu Jay Tishio, ni kijana ambae ndoto yake wakati huu inaonekana ku shamiri kiasi fulani, hii ni baada tu ya kufanyakazi yake vizuri na kazi hiyo kupokelewa vema na mashabiki wa muziki nchini Burundi. Sugu Jay Tishio ni kijana wa 4 katika familia ya watoto wa 7. Amezaliwa Octoba 13 mwaka 1985 mjini Bujumbura.
Ni yatima aliwapoteza wazazi wake wapendwa, mama yake tarehe 6/02/2000. Na baba yake 7/08/2001. Shule ya msingi alisoma Ngagara Q3, Vita ilipozuka nchini Burundi alisimamisha, baadae akaendelesha kwenye shule la msingi la barabara ya 8 Buyenzi maharufu jumuia. amakuhusu Secondari, alisoma kwenye shule la kiufundi la Lycée Technique St-luc ambapo alipata shahada ya A2 kwenye kitivo cha fundi waya wa magari ama (electromecanique) ilikuwa mwaka 2005. Muziki alianza toka utotoni kwani anaamini kuwa kipaji mtu huzaliwa nacho.
katika mwaka 1992, alikuwa akirudilia nyimbo zilizopendwa hasa za christophe matata wa nchini Burundi na Wenge Musica kundi ambalo lilikuwa likipga fora nchini Zaire zamani ambayo ni RDCongo kwa sasa. Majirani walimpenda sana hapo ndipo wazazi wake walimjulisha kitu ambacho hawezi sahau, walimueleza kwamba toka angali mdogo sana alikuwa na tabiya yakuomba kila kitu akiimba asa alipokuwa akihisi njaa. Aliendelea kutunga nyimbo zake.
2001 alianzicha kikundi chake (To Be One) ambapo walikuwa wakitumiya Instrumental za inje, waliweza kuuzuria tamasha mbali mbali moja yazo ni shindano liloandaliwa na ASIYA HEMEDI wa RTNB, Ata hivo alikuwa ajaupa mziki muda mwingi kwa mama alikuwa anapenda masomo sana .
2004, ndipo alirekodi nyimbo yake yakwanza (I wanna Live With U) ambayo ili mpa kutambulika kote inchini na kupata mialiko inje na ndani ya nchi akatowa zingine nyimbo.2006, alialikwa kwenye show Kigali, akapabaki myezi 6 ili aitambulishe kazi yake vizuri. Kule alitowa NDABATASHA ikapata tunzo la mziki bora ,shindano liloandiliwa na Radio Flash FM Rwanda, akapta mashabiki wengi rwanda na burundi.
Aliporudi Burundi, wa Kaunda kundi kwajina la OGOPA BAND akiwa na wenzake,Guyrap,s na Mss G Flow.waliweza kuanda show kubwa tarehe 6.12.2006,ila kundi ilo alikuweza kuendelea.
Ndipo compun ya TOP IKOH ikatambuwa kipaji chake ikaamuwa ku msapoti ili waufanye mziki kazi.Ndipo alipoitowa MAISHA KAMA GAME ambayo ikatambulisha ALBUM yake ya nyimbo 10 zifwatazo :
1 .I wonna live with u ft Rick Dogg,Mss G Flow prod Jeremie.
2 .Kama unanipenda prod Jeremie.
3.Maisha kama game prod Ado,Bochum,Alex.
4.Kisa dem ft Fizzo prod Dr Jack F2K Rwanda.
5.Nzirinda prod Ado alpha record.
6.Ndabatasha Remix prod Dr Jack Rwanda.
7.Iwacu ni heza remix prod Dr Jack F2K Rwanda.
8.Amidah ft Dr Cloud prod Dr Jack F2K RWANDA,
9. BORA UNGEACHA Prod Dr Jack F2K Rwanda.
10. Kisa dem Part 2.
Kinyume na nyimbo zake alishirikishwa na wasani wengi inje na ndani ya inchi. Baadhi yazo ni maisha ya ghetto pamoja na Mr. Fanu wa congo Uvira, Inyange na Master SMG wa rwanda, Ili hit sana Kigali, Umenitoka na Public Familly wa Bubanza, Ubudodi na Didier wa Rwanda, Bomba Style na EA Boyz wa Rwanda, Twende beach na OZB wa Bongo. Ono omwana na Cool Man wa kampala.
Aliweza kuhuzuriya Show nyingi (saga plage, la pirogue, muse vivant (Akabirya talent show walo udhuriya wanajuwa ilikuwaje sugu jay alipo paa jukwani) , centre culturel francais, odeon palace) inje ya inchi (ruhengeri, kigali na universty ya butare rwanda) na Uvira. Na pote aliintangaza inchi yake Burundi vizuri.

habari

Hii ni moja miongoni mwa sehemu ambayo utakuta habari kutoka nchini Burundi katika lugha ya kiswahili,na hata habari kutoka ukanda mzima wa maziwa makuu. waweza pia kuchangia huku ukiwa mtaarabu kati ya yale ambayo labda waona kwamba waweza kutowa muelekeo zaidi.