Waziri wa mambo ya ndani amewapigia maarufu magavana kutoa ruhusa jumamosi wakati wa shughuli za usafi. Waziri Edouard Nduwimana ameiambia idhaa hii kwamba hatua yake imetokana na wananchi wengi kuomba ruhusa za udhuru wa kusafiri jumamossi na hivo shughuli za usafi kuonekana zikipuuziwa. Amewashauri wananchi hasa wasafiri badala ya kun’gan’gania kuomba ruhusa za jumamossi waandae mikakati ya safari zao mapema kuhakikisha kwamba wamefika katika maeneo wanakokwenda kabla au baada ya shughuli za usafi za jumamossi asubuhi. Aidha waziri huyo wa mambo ya ndani amesema kwamba iwapo udhuru wa kuomba idhni utaonekana una umuhimu mkubwa kama shughuli za musba au safari za ndege, basi wakuu wa mikoa watajadili hilo na kumpa ruhusa muhitaji.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire