WARUNDI 20 WALIOFUKUZWA NCHINI TANZANIA WAWASILI MKOANI RUTANA KUSINI MWA BURUNDI
Raia takriban 20 waliofukuzwa nchini Tanzania, wamewasili jana jumatano asubuhi tarehe 24/9/2008 katika mkoa wa Rutana kusini mwa Burundi bada ya kutembea kwa mguu kwa muda wa siku 15. Raia hao wengi wao ni watoto na wanawake waliokuwa wakiishi nchini Tanzania tangu mwaka 1995 katika kijiji cha Bukiriro wilaya ya Ngara Mkoani Kagera. Raia hao walifukuzwa nchini Tanzania tangu tarehe 9 mwezi wa 9 na wamedai kuwa wazaliwa wa mikoa ya Cibitoke na Ngozi na kwamba walifurushwa na watu wa jamii ya wanangambo waliowapora mali na vitu vyao.