mercredi 9 septembre 2009

KUKOSEKANA KWA SHERIA JUU YA UCHAGUZI NCHINI BURUNDI KWA CHELEWESHA SHUGHULI ZA TUME HURU YA UCHAGUZI CENI.

Bunge nchini Burundi limeahirisha kwa mara ya tena kikao cha dharura kilichoititishwa na rais wa jamuhuri tangu jumatatu iliopita. Wabunge walitakiwa kujadili jumatano hii muswada wa sheria uhusuo sheria za uchaguzi wa 2010 unaosubiriwa na wengi nchini Burundi. Spika wa Bunge Pie Ntavyohanyuma ameskika akisema kuwa kuna umuhimu wa kuahirisha muswada huo wa sheria ukizingatia kuwa hakujapatikana muafaka kuhusu baadhi ya vipengee. Baadhi ya yanayo leta utata na kupelekea wanasiasa kutoelewana ni pamoja na orodha ya utaratibu mzima wa uchaguzi utavyo fanyika. Chama tawala CNDD-FDD kinataka uchaguzi uanzie juu, yaani uchaguzi wa rais, huku vyama vingine vikitupilia mbali pendekezo hilo. Pia, kadi ya uchaguzi, wanasiasa wanaomba iwe moja kwa vyama vyote vitavyo jikita katika mlolongo wa uchaguzi wakati ambapo chama tawala CNDD-FDD kikiomba pawepo na kadi tofauti kwa kila chama. Swala la dhamana pia linazusha utata ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2005 mgombea kiti cha urais alitakiwa kilipa franka za Burundi milioni 3, lakini mwaka huu wa 2010 mgombea kiti cha urais anatakiwa kulipa franka za Burundi milioni 15. Swala la msamaha wa muda uliotolewa miaka ya nyuma kwa viongozi waliohusika kwa njia moja ama nyingine na machafuko nchini Burundi linazuia pia tafrani. Kukosekana kwa sheria juu a uchaguzi kunachelewesha shughuli za tume ya uchguzi CENI kuanza kazi zake. Wabunge wamepanga kukutana tena alhamis septemba 10/9/2009 kujaribu kutafuta muafaka kuhusu sheria juu ya uchaguzi.

Aucun commentaire: