Gabriel Rufyiri mkuu wa shirika linalo jihusisha na upigaji vita rushwa na uporaji mali ya umma nchini Burundi OLUCOME ameviambia vyombo vya habari nchini Burundi kwamba siku zote hizi za nyuma amekuwa akipokea simu za watu asio wafahamu ambao wamekuwa wakimtisha na kumtia hofu. Kiongozi huyo amesema tayari amefikisha ripoti kwa hakimu mkuu wa jamuhuri jijini Bujumbura, hadi sasa amesema hajapata jibu lolote. Upande wa polisi kupitia msemaji wake Chanel Ntarabaganyi ameomba Rufyiri atowe namba za simu wanazo tumia watu hao wanaomtia hofu ili waendeshe uchunguzi. Kuhusu uchunguzi wa mauaji ya kifo cha aliekuwa naibu kiongozi wa shirika la OLUCOME Ernest MANIRUMVA alieuawa kikatili siku zilizopita na watu siojulikana bado, msemaji wa jeshi la Polisi nchini Burundi Pierre Chanel NTARABAGANYI amesema kuwa hadi sasa tume ya uchunguzi ilioundwa inaendeleza shughuli zake, na tayari imeomba msaada wa kikosi cha polisi kutoka ugenini itayo saidia katika kuendesha uchunguzi wakitumia ujuzi wa hali ya juu.mardi 21 avril 2009
VITISHO DHIDI YA MWENYEKITI WA SHIRIKA LA KIRAIA LA OLUCOME NCHINI BURUNDI.
Gabriel Rufyiri mkuu wa shirika linalo jihusisha na upigaji vita rushwa na uporaji mali ya umma nchini Burundi OLUCOME ameviambia vyombo vya habari nchini Burundi kwamba siku zote hizi za nyuma amekuwa akipokea simu za watu asio wafahamu ambao wamekuwa wakimtisha na kumtia hofu. Kiongozi huyo amesema tayari amefikisha ripoti kwa hakimu mkuu wa jamuhuri jijini Bujumbura, hadi sasa amesema hajapata jibu lolote. Upande wa polisi kupitia msemaji wake Chanel Ntarabaganyi ameomba Rufyiri atowe namba za simu wanazo tumia watu hao wanaomtia hofu ili waendeshe uchunguzi. Kuhusu uchunguzi wa mauaji ya kifo cha aliekuwa naibu kiongozi wa shirika la OLUCOME Ernest MANIRUMVA alieuawa kikatili siku zilizopita na watu siojulikana bado, msemaji wa jeshi la Polisi nchini Burundi Pierre Chanel NTARABAGANYI amesema kuwa hadi sasa tume ya uchunguzi ilioundwa inaendeleza shughuli zake, na tayari imeomba msaada wa kikosi cha polisi kutoka ugenini itayo saidia katika kuendesha uchunguzi wakitumia ujuzi wa hali ya juu.lundi 20 avril 2009
SAMAHANI NDUGU WASOMAJI
Tuna tanguliza samahani kwa wapenzi wetu wasomaji wa blog hii kwa habari tulioindika kuhusu kufunguwa mashtaka kwa kiongozi zamani wa uasi nchini DRC Laurent Nkunda ambapo tulisema kuwa ni kiongozi wa kundi la FDLR, tulijidanganya kidogo, Laurent Nkunda hakuwa kiongozi wa FDLR bali alikuwa kiongozi zamani wa kundi la CNDP. natumaikuwa tumesameheka
samedi 18 avril 2009
KIONGOZI ZAMANI WA KUNDI LA UASI LA FDLR LAURENT NKUNDA AIFUNGULIA MASHTAKA SERIKALI YA RWANDA

Kiongozi wa waasi wa FDLR aliyekamatwa nchini Rwanda Laurent Nkunda ameishtaki serikali ya Rwanda kwa kumzuilia kinyume cha sheria. Katibu wa Idara ya habari ya Rais nchini Rwanda Yoland Makolo amesema kuwa, kesi ya Jenerali Nkunda dhidi ya serikali ya Kigali imesikizwa ijumaa April 17 lakini akasita kueleza uamuzi uliotolewa. Makolo ameongeza kuwa, Nkunda atarejeshwa nchini Congo anakotakiwa kujibu mashtaka ya ubakaji, utekaji nyara, kuwashirikisha watoto wadogo vitani pamoja na jinai zinginezo. Jenerali nkunda yuko chini ya kifungo cha nyumbani tangu mwezi Januari mwaka huu anakozuiliwa na serikali ya Rwanda. Mataifa ya Congo na Rwanda yamekuwa yakinyoosheana kidole cha lawama kuhusiana na suala la waasi lakini kuzuiliwa kwa Nkunda na serikali ya Rais Paul Kagame wa Rwanda ni dhihirisho tosha kuwa nchi hizo mbili ziko tayari kubadilisha mkondo wa uhusiano wao, wamesema weledi wa mambo.
BDI-MWENYEKITI WA FNL AGATHON RWASA AREJEA KATIKA MAISHA YA KIRAIA.

Kiongozi wa kundi la uasi zamani la FNL Agathon Rwasa amerejeshwa katika maisha ya kiraia jumamosi hii April 18.2009. Shughuli rasmi zimefanyika katika kambi walimo kusanywa wapiganaji wa FNL ya Rubira. Hii ikiwa ni iashara ya kwamba amani nchini Burundi inapiga hatuwa ya kuridhisha.
Msuluhishi katika mgogoro wa FNL na serikali ya Burundi Charles Nquakula aliteuwa tume iitwayo Task Team ambayo yatakiwa kuharakisha utekelezwaji kivitendo makubaliano ya FNL na serikali ya Burundi, tume hiyo ilipanga kwamba Tarehe 21 mwezi April watarejeshwa katika maisha ya kiraia wapiganaji wa FNL na ndipo chama hicho kitasajilia rasmi kuwa chama cha kisiasa nchini Burundi ambacho kitakuwa cha 42. tarehe 22 mwezi April ndipo yataanza mafunzo ya kuwanoa bongo wapiganaji zamani wataojiunga na jeshi la taifa wapatao 2100, mafunzo ambayo yamepangwa kufanyika Mkoani Bururi huku wale wataojiunga na jeshi la paolisi wapatao 1400 wakipewa mafunzo katika vituo vya Gatumba na Rubira huko Mkoani Bubanza. Hata hivo wanajeshi wapatao 390 wakiwemo wanajeshi wa taifa na wa FNL ndio ambao watalinda usalama wa vituo mbalimbali baada ya wanajaeshi wa Umoja wa Afrika kurejea nyumbani kwao. Askari hao wataendesha shughuli hizo baada ya mafunzo ya myezi 6. wapiganaji elf 10 na wanawake 100 watapewa viinuwa mgongo na badae warejea nyumbani kwao ambapo watasaidiwa katika miradi yao ya kujiendeleza. Watoto 340 watatenganishwa na wengine wapiganaji. Ifikapo juni 30 ndio itakuwa tarehe ya mwisho, mwisho kabisa wa shughuli za kuwarejesha katika maisha ya kiraia wapiganaji zamani wa FNL. Serikali ya Burundi imetakiwa kuwaacha huri wafungwa wa FNL ambao hadi sasa wapmesalia katika jela mbalimbali. Kuhusu nyadhifa 32 zilizo takiwa kutolewa na serikali, rais wa jamuhuri Pierre Nkurunziza na mwenyekiti wa FNL tayari waliteuwa tume ambayo inafuatilia kwa karibu swala hilo na kulitafutia ufumbuzi.
vendredi 17 avril 2009
WANASENETI WA BURUNDI WAYAKATAA MAJINA KADHAA YALIOPENDEKEZWA NA RAIS KWENYE NYADHIFA TOFAUTI KARENGA RAMADHAN AKIWEMO.

Baraza la seneti nchini Burundi limejadili alhamisi hii April 16 majina ya watu waliopendekezwa na rais wa jamuhuri ya Burundi kwenye nyadhifa mbalimbali , ikiwa ni kwenye uongozi wa Mikoa kadhaa ya Burundi, aidha uwakilishi wa Burundi ugenini pomoja na kwenye uongozi wa jeshi la taifa.
Waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana alikuwa amewasilisha majina ya watu waliopendekezwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuongoza mikoa ya Makamba, Ruyigi na Kayanza.
Reverien Ndikuriyo alikuwa amependekezwa kuongoza Mkoa wa Makamba.
Fenele Nduwimana alipendekezwa kuongoza Mkoa wa Kayanza.na Syriaque Nshimirimana alipendekezwa kuwa gavana wa Mkoa wa Ruyigi. Majina ya waliopendekezwa kuwa wanabalozi wa Burundi ugenini ni , ni pamoja na Karenga Ramadhani aliewahi kuwa mkuu wa itifaki kwenye ofisi ya rais wa jamuhuri kabla ya kuwa waziri wa habari na msemaji wa serikali na hatimaye waziri anaye husika na uhusiano wa kikanda.
Mwingine ni Angel Niyuhire ambaye ni mbunge kutoka chama Uprona pamoja na Gahutu zacharie. Wakati huo waziri wa ulinzi meja jenerali Jermain Niyoyankana aliwasilisha majina ya Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye ni Naibu mkuu wa majeshi, alipendekezwa kuwa mkuu wa majeshi ya Burundi kuchukuwa nafasi ya Brigadia jeneral Samuel Gahiro alieteuliwa ku afisa wa kijeshi kwenye ubalozi wa Burundi mjini Tripoli. Mwingine ni meja jenerali Niyoyunguruza Juvenal aliependekezwa kuwa kaimi mkuu wa majeshi.
Miongoni mwa majina hayo, Juvenal Niyoyunguruza amekataliwa na wanaseneti kuwa naibu mkuu wa majeshi wakimtuhumu ya kwamba hayati Melchior Ndadaye rais wa kwanza wa Burundi kuchaguliwa chini misingi ya kidemokrasia aliuawa katika kambi ambayo alikuwa kamanda bila kuzuia mauaji hayo. Mwingine aliekataliwa ni Karenga Ramadhani, kuiwakilisha Burundi ugenini wanaseneti wakimtuhumu kwa matamshi aliyoyatowa wakati alipokuwa waziri wa habari na msemaji wa serikali kuhusu mkasa wa mauzo ya ndege ya rais Falcon 50, Naye Reverien Ndikuriyo amekataliwa kuongoza Mkoa wa Makamba baada ya jina lake kutajwa katika mkasa wa shirika la IDC lililo walaghai wananchi katika mikoa na kuwapora pesa .

vendredi 3 avril 2009
Waliomuua Lucky Dube wafungwa maisha

Jaji wa Afrika Kusini amewahukumu watu watatu kifungo cha maisha jela baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua mwanamuziki maarufu wa reggae Lucky Dube mwaka 2007. Lucky Dube aliyekuwa na umri wa miaka 43, alipigwa risasi na watu hao watatu katika jaribio la kumuibia gari lake katika kitongoji kimoja cha mjini Johannesburg, tukio lililoleta hofu kwa taifa hilo. Jamaa wa Lucky Dube walitokwa machozi na baadae wakashangilia baada ya kutolewa hukumu hiyo. wanamuziki pamoja na mashabiki walikusanyika nje ya mahakama hiyo kuonesha mshikamano wao. Mahakama hiyo ilielezwa kuwa washtakiwa hao watatu, walifikiria mtu waliyekuwa wakimpora gari alikuwa raia wa Nigeria na kamwe hawakufahamu waliyemuua alikuwa Lucky Dube hadi waliposoma magazetini siku iliyofuatatu hao watatu. Moja ya mabango nje ya mahakama hiyo lilikuwa likisomeka "Lucky Dube hafanani na Mnigeria; bali yeye ni Mwafrika." Mahakama hiyo pia imewahukumu Sifiso Mhlanga, Julius Gxowa, na Mbuti Mabe kifungo cha miaka 15 kila mmoja kwa kufanya jaribio la kupora gari la Lucky Dube.
Inscription à :
Articles (Atom)