
Kesi ya watu 11 wanaoshukiwa kuendesha mauaji ya Albinos ilisikilizwa jumanne na mahakama kuu ya mjini Ruyigi. Kulingana na muandishi habari wa kituo cha Burundi cha kutawanyia ABP habari Mkoani Ruyigi Maurice Bukuru, kesi hiyo ilianza kusikilizwa tangu saa nne mchana ambapo halaiki ya watu walikuwa wamemiminika mahakamani kusilikiza kesi hiyo. Awamu ya kwanza ya kesi hiyo iliwahusisha watu 8 walioshutumiwa kuwamalizia maisha binti mmoja albinos aliejulikana kwa jina la Harerimana Violette alieuawa Septemba 8 mwaka jana, pamoja na mtoto mwgine alieuawa katika kijiji cha Kinyinya na bwana mmoja albinos alieuawa Bweru. Washukiwa wengine wanashutumiwa kuhuika na jaribio la mauaji ya Albinos. Washukiwa hao walitajwa na wafungwa ambao walikatiwa kifungo cha maisha jela ambao wanazuiliwa katika jela kuu la Ruyigi. Wafungwa hao wanaozuiliwa jela walihusika na mauaji ya binti mmoja Albinos na kuuza viungo vya mwili mtu ajulikanae kwa jina Richard Adelin wa tarafa ya Cendajuru Mkoani Cankuzo ambae yuu huru hadi sasa. Katika kesi hiyo Nyabenda Elie maharufu Bihoro alikiri kuhusika katika mauaji hayo huku wengine wakikana kuhusika moja kwa moja. Hakimu mkuu wa jamuhuri Mkoani Ruyigi Nicodème Gahimbare aliwakamata kinaga ubaga mwezi march iliopita watu 11 wakiwa na viongo vya Albinos. Mkoa wa Ruyigi ndio ambao ulioorodhesha idadi kubwa ya mauaji ya Albinos waliouawa tangu kuanzishwa kwa visa vya mauaji ya Albinos vilivyo anzia nchini Tanzania na kutanda hadi nchini Burundi. Tangu kukamatwa kwa mtandao huo wa wahalivu wa mauaji ya Albinos Mkoani Ruyigi mwezi march hakuna kitendo kiovu kama hicho ambacho kimekwisha ripotiwa hadi leo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire