mercredi 15 octobre 2008

CHAMA KIKUU CHA UPINZANI NCHINI BURUNDI FRODEBU KIMEMTEUWA DOMITIEN NDAYIZEYE KUWA MTETEZI WAKE KWENYE UCHAGUZI WA MWAKA 2010.
Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi Sahwanya FRODEBU kimemteuwa rais wa zamani wa Burundi Domitien NDAYIZEYE kusimama kwenye uchaguzi wa 2010 utaofanyika nchini Burundi.
katika uchguzi wa wajumbe wa kamati tendaji uliofanyika jumapili octoba 12.2008 uliojumuisha wajumbe 268, Domitien NDAYIZEYE lichaguliwa kwa asilimia 86.5 ya kura dhidi ya wagombea wengine wawili Pierre Claver NAHIMANA na Rose NDUWAYO. Baada ya kuteuliwa kwake, rais huyo wa zamani aliviambia vyombo vya habari kuwa, alikuwa ametangaza kuachana na siasa baada ya kuondoka kwenye utawala mwaka 2005, na kufungwa kwake kwenye jela kuu la Mpimba mwaka 2006, sasa amerejea kwenye uwanja wa siasa ili kupambana na rais alieko madarakani wakati huu. FRODEBU ni chama cha kwanza cha upinzani kutangaza rasmi mgombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Domitien NDAYIZEYE aliiongoza Burundi tangu mwaka 2003 hadi Agosti 2005 wakati wa awamu ya pili ya kipindi cha mpito, kipindi ambacho kilihitimshwa kwa uchaguzu uliopelekea chama CNDD-FDD kunyakuwa ushindi.

PALIPEHUTU/FNL YAPINGA KATAKATA KUBADILI JINA

katika mkutano uliitishwa na katibu mkuu wa palipehutu FNL Jonas NSHIMIRIMANA jumanne 14 octoba, aliwaambia waandishi habari kuwa kamwe Palipehutu FNL haitothubutu kubadili jina hilo, na kwamba iwapo watafanya hivyo, basi watakuwa wamekwenda kinyume na mkataba, kwa kuwa mikataba yote waliosaini na serikali ya Burundi walitumia jina hilo Palipehutu/FNL na itakuwa ni kuvunja mkataba wakati ambapo hawana nia ya kuvunja mkataba huo. Seriklai ya Burundi imelipa sharti kundi hilo kubadili jina kabla ya kukubaliwa rasmi kama chama cha kisiasa, kwa kuwa kama inavyo sema taarifa ya serikali ni kinyume cha katiba ya Burndi iwapo kitasainiwa chama chenye jina la kikabila. Licha ya kukwama kwa mazungumzo ya palipehutu/FNL na serikali ya Burundi, Jonas NSHIMIRIMANA amesema kuwa majadiliano yataendelea hadi pale serikali itaitambua Palipehutu/FNL kama chama rasmi cha kisiasa. Katibu mkuu wa Palipehutu FNL ametumia fursa hiyo kukanusha habari kwamba kuna mzozo wa ndani katika kundi hilo la palipehutu FNL ambapo mwenyekiti wa kundi hilo Agathon RWASA na msemaji wa palipehutu FNL Pasteru HABIMANA hawapatani na kwamba kila mmoja anafuyawafuasi wake. Kiongozi huyo amekanusha habari hizo na kusema kuwa huo ni uzushi mtupu.
MIAKA 3 IMEMALIZIKA CHAMA CNDD-FDD KIWA KWENYE UTAWALA NCHINI BURUNDI
Chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimeazimisha myaka 3 Jumapili tarehe 12 Octoba 2008 kikiwa kwenye usukani wa kuiongoza Burundi. sherehe rasmi za siku kuu hiyi zimefanyika katika Mkoa wa Gitega Kaskazini mwa Burundi. Wafuasi wa chama hicho kutoka katika kila mikoa ya Burundi walimiminika kwa wingi kuhudhuria sherehe hizo. Wajumbe wa vyama vingine vya upinzani walialikwa kwenye sherehe hizo. chama kinacho tawala nchini Jamuhuri ya Kimokrasia ya Congo PPRD kiliwatuma wajumbe wake kushiriki kwenye sherehe hizo ambazo zilionekana kufana kiasi fulani. halaiki ya watu walimiminika kwenye uwanja wa mpira wa miguu Mkoani Gitega huku wakivalia sare za chama CNDD-FDD. Akiwahutubia wafuasi wake mwenyekiti wa chama CNDD-FDD Jéremie NGENDAKUMANA alisema kuwa siku hiyo ni siku ya furaha kwa kila mwananchi na hasa wanachama wa CNDD-FDD kwa kuwa ni mara ya kwanza utawala uliochaguliwa katika misingi ya kidemokrasia unafanya zaidi ya miezi 3 madarakani. aliwaambia wafuasi wa chama kuwa wavivu hawana nafasi katika chama, nakwamba lazima watumike kwa bidii katika kuendeleza mipango ya nchi. miaka mitatu hii imemalizika wazazi wanajinfua bila malipo, huku watoto wakisoma bila kutowa hata mea na hata watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 wanatibiwa bila malipo. Jéremie NGENDAKUMANA amewapa kasopo wafuasi wa upinzani ambao wamekuwa wakiimba uchaguzi wakati huu na ilihali kumesalia muda wa miaka 2 wa utawala wa chama hicho kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi. Upande wake rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA ambae ni mfuasi wa chama hicho, alisema kuwa miaka 3 kwenye utawala ni midogo kwa kuwa safari bado ingali ndefu; lakinihata hivo lazima ashukuriwe Mungu. Rais NKURUNZIZA amewatahadharisha wale wote ambao alisema wamekuwa wakimuwekea vizingiti na mitego katika utawala wake, na kwamba wafahamu kuwa wakiendelea kutezga mitego hiyo basi watajikuta wao ndio ambao wameanguka wa kwanza ndani yake. sherehe hizo zlihitimishwa kwa kutowa zawadi kwa walioendesha kzi zao vizuri katika kipindi chote hiki. Miongoni mwa waliopewa zawadi ni Rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA alievalishwa midali, huku wengine kama seneta Muhamed Rukara, Gervais RUFYIKIRI na Pie NTAVYOHANYUMA wakipewa picha zinazo maanisha kuwa wameshukuriwa na chama katika kazi zao.

jeudi 9 octobre 2008

HATUWA KADHAA ZACHUKULIWA ILI KUWALINDIA USALAMA MA ALBINOS
Viongozi waliokuwa wkikutana mjini Ruyigi juzi jumanne na jumatano katika mkutano na wa wakilishi wa ma zeruzeru,hatimae wameazimia hatuwa za muda ili kuwalindia uslama mazeuzeru ambao wanakabiliwa na uslama mdogo Mkoani Ruyigi na hata Mikoa mingine mathalan Cankuzo. Kwa mujibu wa kiongozi wa shirika la ma albinos nchini nchini Burundi Kazungu Kassim, amesema kwamba miongoni mwa hatuwa zilizo chukuliwa ni kuwapatishia nyumba mojawapo katika tarafa ya Ruyigi ambako watalindiwa usalama zaidi. Kiongozi huyo aliwatolea mwito ma albinos popote pale walipo kutosita kujisalimisha kwenye makao makuu ya tarafa pindi tu watapojihisi kuwa usalama wao upo hatarini. Kiongozi huyo aliendelea kusema, wakati huu wanahitaji misaada ya kukidhi mahitaji ya ma albinos hao ambao wamekusanywa pamoja. Kiasi ma albinos 48 ndio ambao wanahesabiwa kueshi katika Mkoa huo wa Ruyigi. Kwa sasa wamekwisha kusanyika ma albinos zaidi ya 10 kwenye nyumba hiyo iliochukuliwa kama kituo cha kuwahifadhi ma albinos.

JOSE CAMELEONE AVUNJIKA MIGUU BAADA YA KUOTA AKITEMBEA.

Mwanamuzki huyo wa Uganda alikuwa nchini Tanzania kwa mianajili ya tamasha mbalimbali alijurusha toka kwenye ghorofa ya tatu kwenye Hoteli ya Impala mjini Arusha. duru kutoka Arusha zaarifu kuwa mwanamuziki huyo aliingia kupumzika muda mchache akitokea kuendesha Show, na ndipo akaota kuwa yuko anatembea, baadae akaanguka kwenye ghorofa hiyo. baadae alipelekwa haraka Hospitalini. lakini kabla hajaanza kupata matibabu mkewe alikuja na ndege kutoka Kampala hadi kwenye Hospitali hiyo na kumpeleka Uganda kwenye hospitali mojawa kuu nchini hapo ambako anaendelea kupata matibabu.

VYAMA VYA KISIASA NCHINI BURUNDI VYA IFASIRI HATUWA YA KUZUIA MIKUTANO YA HADHARA KUWA IMEPITWA NA WAKATI
Waziri wa mambo ya ndani na maendeleo ya vijiji Venant Kamana alitangaza kwamba hakuna mikutano yoyote ile aidha maadamano yoyote ya vyama vya kisiasa ya hadhara yatakubaliwa tena kuendeshwa holela bila kuwa na kibali rasmi, na kwamba siku za maadamano ni jumamosi na jumapili. Maandamano aidha mikutano uya siku ya jumamosi yatakubaliwa kuazishwa saa tano hadi saa kumi na mbili jioni, na siku ya jumapili ni kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Kama alivyo kazia tangazo lake hilo waziri wa mambo ya ndani amesema kuwa hii ni kuepusha vurugu ambazo zaweza kujitokeza katika siku zijazo kutokana na mikutano ya vyama vya kisiasa. Mkurugenzi mkuu kwenye wizaraTérence Mbonabuca, upande wake alisema kuwa hatuwa hiyo ilichukuliwa baada ya kujadiliana na viongozi mbalimbali wa vyama vya kisiasa. hatuwa hii imepokelewa kwa shingo upande na vyama vya kisiasa. Mwenyekiti wa chama SAHWANYA FRODEBU Léonce NGENDAKUMANA amesema kwamba hatuwa hiyo anayo jaribu kuchukuwa waziri wa mambo ya ndani na maendeleo ya vijiji ni ya zamani wakati ambapo Burundi ilikuwa ndio bado inaingiza mguu katika mfumo wa kidemokrasia ambapo serikali ya zama hizo iliamuru kupinga maandamano na mikutano ya vyama vya kisiasa lakini wakati huu Burundi imepiga hatuwa kubwa, hakuna budi kuendelea mbele kuliko kurejea nyuma, na kwamba hakuna sheria ya kiwaziri ambayo yaweza kufuta sheria ya katiba aidha sheria kuhusu vyama vya kisiasa. Léonce NGENDAKUMANA ameendelea kusema kua iwapo waziri wa mambo ya ndani ameona umuhimu wa kubadili badhi ya sheria ni kusukuma mapendekezo yake bungeni ili yajadiliwe. Kiongozi huyo amesema chama FRODEBU kitapinga hatuwa zozote zile za kuzuia mikutana na maadamano ya vyama visivyo unga mkono chama kilicho madarakani. maoni kama hayo yalitolewa pia na msemaji wa chama CNDD Francois BIZIMANA
WAFUNGWA ZAIDI YA 15 WAJERUHIWA KATIKA JELA KUU LA MPIMBA MJINI BUJUMBURA
Katika uchunguzi ulioendeshwa kwenye jela kuu la Mpimba baada ya kutokea vurugu siku ya jumapili ambapo risase na hata bomu zilisikika jelani hapo, wafungwa wa tano wamegunduliwa kuhusika na vurugu hizo pia na kukutwa na shughuli za kutengeneza noti za magendo katika jela hilo la Mpimba. Duru kutoka kwenye jela kuu la Mpimba zimearifu kuwa kiini cha vurugu hizo ni mfungwa ambae aliagiza simu 4 za mkononi kwa mtu ambae aliekuwa amekwenda kumuona nduguye, baada ya kumpa pesa, na kuondoka ndipo akagunduwa kwamba noti zile alizo pewa sio noti halali, akamuwa kuzirudisha huko Mpimba. Alietowa pesa hizo akakana kurejesha simu, baadae ndipo wenzake walimuunga mkono na kuanzisha vurugu. Lakini hata hivo duru zaidi zimesema kuwa kiini cha vurugu hizo ni mzozo uliotokea bainaya wafungwa wakati wa kugawa simu za mkononi na pesa walizo zipata kutokana na suhghuli zao hizo za utengenezajiwa noti bandia. Polisi ililazimika kuingilia kati kwa kuvurumisha risase hewani kama zilivyo endelea kuarifu duru kutoka katika jela kuu hilo la Mpimba. Wafungwa zaidi ya 15 walijeruhiwa katika tukio hilo mmoja akiwa katika hali mbaya.
SERIKALI YA BURUNDI YAANDAA MABADILIKO KATIKA UTOWAJO MISHAHARA

Serikali ya Burundi imo mbioni kuandaa mradi mpya utaopelekea wafanyakazi wake kusalia nhini Burundi badala ya kufikiria kwenda ugenini aidha kutumikia mashirika ya wahisani ambayo hutowa donge nono zaidi kulikoni hapa nchini. Hii inatokana hasa na mshara mfinyu wanao pewa wafanyakazi wa serikali. Hayo yamefahamishwa na Pierre NTIRABAMPA Mkurugenzi mkuu kwenye wizara ya kazi wakati akiyajibu maswali ya waandishi habari katika kipindi mojawapo kilichokuwa kikitasmini hali halisi ya mfanyakazi wa serikali na jinsi gani ya kuboresha kazi na kupelekea mfanyakazi wa serikali apate nafuu katika utekelezwaji wa kazi zake. Kipindi hicho kilikuwa kimeandaliwa na muungano wa mashirika yanayo tetea haki za wafanyakazi COSYBU.

dimanche 5 octobre 2008

USALAMA

WALINZI 3 WA SHIRIKA LA KK SECURITY WATIWA MBARONI KWA KUSHUKIWA KUHUSI NA WIZI WA PIKIPIKI 4 MKOANI RUTANA.

Polisi ya usalama wa raia Mkoani Rutana ilifaulu kukamata pikipiki 4 mpya katika usiku wa kuamkia ijumaa, zilizo ibiwa katika usiku huo kwenye shirika la GTZ Mkoani Rutana. Watu 3 wa shirika la Ulinzi la KK Security na mhusika wa shuhuli za kunyunyuzia maji bustani katika shirika la GTZ wamewekwa mbaroni kwa kushukiwa kuhusika na wizi wa pikipiki hizo mpya ambazo zilikamatwa kwa mchango mkubwa wa raia Mkoani hapo. Kama alivyo fahamisha afisaa wa polisi ya usalama Mkoani Rutana Sylvestre NZOHABONAYO, waliipokea simu kutoka kwa raia ambae aliwafahamisha kuona hali ya sintofahamu ambapo pikipiki mpya zinasukumwa usiku wa saa nne unusu, zikitokea kwenye makao makuuya shirika la GTZ Mkoani Rutana zikielekezwa katika kata ya Birongozi. Kiongozi huyo aliamuru kikoso chake kuripoti haraka, wezi hao walifaulu kitimka baada ya kuwaona askari polisi. Baadae polisi walipojielekeza kwenye shirika hilo la GTZ, ndipo walinzi wakajaribu kutimka bila mafaanikio, kwa kuwa, polisi ilikuwa imetanda eneo zima la shirika hilo. Baada ya kuendesha msako zaidi ndipo iligunduliwa pikipiki nyingine ambayo ilikuwa kweye kituo cha mafuta mkoani hapo, huku kukiwa na lori aina ya Fuso ambayo ilikuwa ikisubiri kusafirisha pikipiki hizo hadi nchini TZ. Kiongozi wa walinzi hao, alijaribu kuwatetea wafanyakazi wake bila mafaanikio kwa kuwa, imedhihirika kwamba nae huenda anahusika kwa vile, kama wanavyo sema walinzi hao walilazimishwa kufungua milango na watu 6 wenye silaha. Lakini hata hivo, haieleweki kwanini hawakufahamisha idara za uslama mapema na ilihali uwezo walikuwa nao, huku pia wakijaribu kutimka wakati walipowaona polisi wa uslama wa raia, kwa nini watimke. Uchunguzi unaendelea huku pikipiki hizo zikipelekwa kwenye idara ya polisi.

jeudi 2 octobre 2008

SHEREHE ZA ID-IL FITRI ZAFANYIKA VEMA LICHA YA SERIKALI KUTOKUWEPO
Kama ilivyokuwa kawaida kila mwaka, jamii ya waislam nchini Burundi COMIBU huitolea serikali taarifa katika maadhimisho ya siku kuu ya Idil Fitri inayo maanisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. hata hivo kumekuwa na mtafaraku kila mwaka inapo wadia kufungua mwezi ambapo inafikia waislam kufunga siku 30 ao 29, hili linaeleweka, lakinikwa sasa kumekuwemo na mambo ya siasa ndani yake. waislam walifurika kwa wingi kuendesha ibada yao ya sala ya laidi kama ilivyokuwa kawaida. jumuia ya waislam nchini Burundi COMIBU iliwatangazia waislam viwanja maalum ambavyo vitaendeshewa ibada na ma shekh ambao wataendesha ibada hiyo. inakubalika wazi kwamba sherehe rasmi hufanyika kila mwaka Mtaani Jabe, eneo kubwa linalo kusanyikia waumini wengi. mwaka huu kama ilivyo staajabisha wengi sherehe rasmi ziligeuzwa na kupelekewa kwingine. serikali ilimtuma muwakilishi wake huko kwingine. hili halikupelekea sherehe kutofana, badala yake sherehe kwenye uwanja wa idi zilipendeza kiasi kwamba Cheikh Issa Salum BAGORIBARIRA alikuwa ameandaa hutba yake fupi yenye kujawa na ujumbe mzito, ilimalizika huku waumini wakihitaji aendelee. Waumini wa kiislam wamepinga kuendesha malumbano kutokana na hilo kwa kuwa kama walivyo ieleza blogi hii, wanayo matatizoi mengine ndani ya jamii ambayo yawakabili, na kuzidi kuwa hilo ni lidogo, kwa kuwa Uislam ulikuwepo tangu kabla ya utawala uliopo, na Uislam utasalia ulipo huku utawala uliopo ukitoweka.