mercredi 12 novembre 2008

WAFANYABIASHARA WA MAFUTA WAFUNGUA VITUOVYAO KWA KUHOFIA HATUWA YA SERIKALI

Serikali iliazimia kupunguza bei ya mafuta aina ya essence hadi 1700, huku bei ya mafuta aina ya mazout ikipungua hadi 1500. hali hii ilipelekea hata bei ya usafiri mjinikati kupungua hadi 240, wakati hapo awali ilikuwa kwenye 280. kilicho dhihirika baada ya hatuwa hiyo ya serikali ni kufungwa kwa vituo vya mafuta, wamiliki wa vituo hivyo walidai kuwa watafilisika iwapo watauza mafuta wanayo kwa bei mpya wanayo. Uhaba wa mafuta ukadhihirika mjini kote. Lita moja ua mafuta kwenye masoko ya magendo, ilifikia hadi franka elfu nne. shirika la wanunuzi ABUCO lilitowa taarifa ambamo lililaani vikali hali hiyo na kuitolea mwito serikali wa kuitaka ichukuwe hatuwa za kisheria dhidi ya wafanyabiashara ya mafuta ambao ilisema taarifa hiyo ya ABUCO wamekaidi hatuwa ya serikali. Baada ya usumbufu mkubwa mjini Bujumbura wa kupata mafuta, hatimae serikali kupitia waziri wa baishara na viwanda bibi Euphrasie BIGIRIMANA iliazimia hatuwa za kisheria na kutishia kumtoza faini mfanya bishara yoyote yule ataekutwa kafunga kituo chake na ilihali mafuta anayo kama ilivyo dhihirika. hatuwa hiyo ni pamoja na kutozwa faini ya franka elf 50 hadi milioni 5 franka za Burundi na kifungo cha zaidi ya miaka miwilijela.