samedi 18 avril 2009

BDI-MWENYEKITI WA FNL AGATHON RWASA AREJEA KATIKA MAISHA YA KIRAIA.



Kiongozi wa kundi la uasi zamani la FNL Agathon Rwasa amerejeshwa katika maisha ya kiraia jumamosi hii April 18.2009. Shughuli rasmi zimefanyika katika kambi walimo kusanywa wapiganaji wa FNL ya Rubira. Hii ikiwa ni iashara ya kwamba amani nchini Burundi inapiga hatuwa ya kuridhisha.

Msuluhishi katika mgogoro wa FNL na serikali ya Burundi Charles Nquakula aliteuwa tume iitwayo Task Team ambayo yatakiwa kuharakisha utekelezwaji kivitendo makubaliano ya FNL na serikali ya Burundi, tume hiyo ilipanga kwamba Tarehe 21 mwezi April watarejeshwa katika maisha ya kiraia wapiganaji wa FNL na ndipo chama hicho kitasajilia rasmi kuwa chama cha kisiasa nchini Burundi ambacho kitakuwa cha 42. tarehe 22 mwezi April ndipo yataanza mafunzo ya kuwanoa bongo wapiganaji zamani wataojiunga na jeshi la taifa wapatao 2100, mafunzo ambayo yamepangwa kufanyika Mkoani Bururi huku wale wataojiunga na jeshi la paolisi wapatao 1400 wakipewa mafunzo katika vituo vya Gatumba na Rubira huko Mkoani Bubanza. Hata hivo wanajeshi wapatao 390 wakiwemo wanajeshi wa taifa na wa FNL ndio ambao watalinda usalama wa vituo mbalimbali baada ya wanajaeshi wa Umoja wa Afrika kurejea nyumbani kwao. Askari hao wataendesha shughuli hizo baada ya mafunzo ya myezi 6. wapiganaji elf 10 na wanawake 100 watapewa viinuwa mgongo na badae warejea nyumbani kwao ambapo watasaidiwa katika miradi yao ya kujiendeleza. Watoto 340 watatenganishwa na wengine wapiganaji. Ifikapo juni 30 ndio itakuwa tarehe ya mwisho, mwisho kabisa wa shughuli za kuwarejesha katika maisha ya kiraia wapiganaji zamani wa FNL. Serikali ya Burundi imetakiwa kuwaacha huri wafungwa wa FNL ambao hadi sasa wapmesalia katika jela mbalimbali. Kuhusu nyadhifa 32 zilizo takiwa kutolewa na serikali, rais wa jamuhuri Pierre Nkurunziza na mwenyekiti wa FNL tayari waliteuwa tume ambayo inafuatilia kwa karibu swala hilo na kulitafutia ufumbuzi.

Aucun commentaire: