vendredi 30 juillet 2010

WAOKOAJI NCHINI DRC, WAENDELEA NA SHUGHULI ZA UOKOZI

Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta manusura wa ajali ya boti iliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo watu 140 walikufa baada ya boti hiyo iliyobeba abiria kuzidi uwezo wake na kupinduka katika mto. Boti hiyo iliyokuwa na wafanyakazi na abiria wapatao mia mbili inaaminika kugonga kingo za mchanga au mwamba, Jumatano katika maunganiko ya mto Congo, katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo. Baada ya miongo kadhaa ya migogoro, Kongo ina barabara chache au huduma za reli, hali inayosababisha wengi kusafiri kwenye boti hizo zilizojaa pumoni. Mwezi Novemba iliyopita takriban watu 73 walifariki dunia baada ya boti kuzama kwenye ziwa, pia katika jimbo la Bandundu. Ajali iliyotokea hivi karibuni ilitokea siku ya Jumatano. Boti hiyo ilikuwa ikibeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu, mji mkuu katika jimbo hilo. Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo ameliambia shirika la habari la Reuters, " Boti hiyo ilijaa pumoni na haikuweza kuhimili kupita kwenye dhoruba hiyo."

jeudi 29 juillet 2010

VIONGOZI WA TARAFA WATEULIWA

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewateuwa alhamisi hii Julay 29-2010 viongozi wapya wa tarafa mbalimbali zinazo unda mikoa ua Burundi. Hata hivyo baadhi ya tarafa hazikupata viongozi wapya kwani kumekuwa na utata kuhusu uteuzi wa viongozi wa tarafa kuhusiana na tarafa ambazo madiwani kutoka muungano wa vyama kwa ajili ya demokrasia ADC-IKIBIRI walinyakua ushindi lakini baadae kukana kukaa barazani. Mathalan katika baadhi ya Mikoa ya Bujumubura vijijini jumla ya Tarafa 11, tarafa 4 pekee ndizo zimepata viongozi. Katika Manispaa ya jiji la Bujumbura tarafa 3 pekee jumla ya 13 ndizo zimewapata viongozi wapya ikiwa ni pamoja na Kamenge Buterere na Rohero. Mkoani Bururi tarafa 3 ndizo zimewapata viongozi ikiwa ni pamoja na Matana,Vyanda na Rutovu jumla ya tarafa 9. jumla ya tarafa 129, wameteuliwa viongozi 106.

WYCLIF JEAN APANIA KUGOMBEA URAIS NCHINI HAITI


Familia ya mwanamuziki aliyezaliwa Haiti imesema Wyclef Jean anafikiria kugombea urais nchini humo. Lakini nyota huyo wa kundi la Fugees, ambaye aliteuliwa kama balozi wa nchi hiyo mwaka 2006, hajaamua bado kama agombee nafasi hiyo ya miaka mitano.
Haiti ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi mwezi Januari iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 250,000. Taarifa kutoka familia yake ilisema Wyclef "anajali" sana maslahi ya kwao. Taarifa hiyo ilitolewa baada ya kuwepo uvumi huko Haiti kuwa Wyclef anajiandaa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Wagombea wana nafasi ya kujiandikisha mpaka ifikapo Agosti 7. Ilisema: " Namna Wyclef anavyojali maslahi ya kwao hauna mipaka kabisa na ataendelea kuisaidia nchi yake bila kujali kama yeye ni sehemu ya serikali. "Kwa wakati huu, Wyclef Jean hajatangaza nia yake ya kugombea Urais Haiti. Iwapo, na wakati, uamuzi utakapochukuliwa, vyombo vya habari vitapewa taarifa haraka iwezekanavyo."
Rais aliye madarakani kwa sasa Rene Preval anazuiwa na katiba kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine. Wyclef, anayeishi New York, ni mwanzilishi wa wakfu wa kusaidia binadamu ya Yele Haiti, na amechangia kwa kiasi kikubwa katika kutoa misaada tangu kutokea kwa tetemeko hilo la ardhi. Mwanamuziki huyo na mzalishaji wa muziki, anayejulikana zaidi sasa kwa kushirikiana na mwanamuziki nyota wa miondoko ya Pop kutoka Colombia Shakira, anajulikana sana Haiti ambapo nusu ya watu wote nchini humo wana umri wa miaka 21.

MKUTANO WA NCHI WANACHAMA WA CEPGL WAANZA MJINI GISENYI

mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama wa jumuia ya nchi za maziwa makuuCEPGL ambazo ni Rwanda, Burundi, na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wanakutana mjini Gisenyi nchi Rwanda tangu alhamis hii Julay 29.2010 kwenye makao makuu ya CEPGL. Mawaziri hao watajadili kuhusu juhudu za kuimarisha shirika la CEPGL. kwenye ajenda ya mkutano watagusia pia kuhusu swala la wanachama kulipia malimbikizo ya michango yo kwenye shirika hilo.

mercredi 28 juillet 2010

CHAMA CHA CNDD FDD CHAIBUKA MSHINDI WA VITI 32 HUKU UPRONA IKIPATA VITI 2


Kulingana na matokeo ya muda yaliotolewa kupitia muungano wa vyombo vya habari nchini Burundi chama tawala cha CNDD FDD cha rais waé sasa Pierre Nkurunziza kimejipatia viti 32 katika baraza la seneti huku chama UPRONA kikipata viti 2. viti hivyo 2 vyama chama UPRONA vilipatika kimoja kutoka Mkoani Bururi huku kingine kutoka jijini Bujumbura ambapo inasemekana kuwa kulikuwa na maelewano baina ya wagombea wa CNDD FDD na UPRONA. juhudu za maelewano hazikufua dafu huko Mkoani Mwaro ambapo wagombea waliochaguliwa ni kutoka chama CNDD FDD. vyama kutoka muungano wa vyama kwa ajili ya demokrasia ADC IKIBIRI havikushiriki uchaguzi tangu pale vilipo lalamikia tume huru inayo anda uchaguzi kuvuta matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa baraza la madiwani, wajumbe ambao ndio wanaowachaguwa wanaseneti kiulingana na katiba ya Burundi. katiba ya Burundi inaamuru kuwashirika watu kutoka kabila la watwa, hivyo watwa 3 wanalazimika kuteuliwa pamoja pia na ma rais wa zamani wa Burundi.

WATU 152 WAMEUAWA KATIKA AJALI YA NDEGE NCHINI PAKISTAN

Ndege hiyo, iliyokuwa katika safari kutoka Karachi kwenda Islamabad inaendeshwa na kampuni Hapakuwa na taarifa za awali kubaini chanzo cha ajali. Ingawa imeelezwa eneo hilo lilikuwa limetandwa na ukungu.
Televisheni za Pakistan zilionyesha picha za mabaki ya ndege yakiwaka moto, huku helikopta za uokoaji zikiranda juu.binafsi ya Airblue, ilianguka kwenye vilima vilivyoko kaskazini mwa jiji wakati ikijiandaa kutua.Airblue ndiyo kampuni kubwa zaidi ya ndege binafsi, miongoni mwa mashirika yaliyoibuka nchini Pakistan katika miaka ya karibuni.



Kampuni hiyo na idara ya usimamizi wa safari za anga hawadhani ndege hiyo ilikutwa na matatizo ya kiufundi wakati ikiondoka Karachi.
Wanasema hapakuwa na dalili za hitilafu ya kiufundi katika mawasiliano kati ya rubani na mnara wa kuongozea ndege wa Karachi.
Hata hivyo, maafisa wa uwanja wa ndege waliieleza BBC kuwa ndege mbili zilizokuwa zitue kwenye mji huo mkuu zilikataliwa kabla ya ajali hiyo ya Airblue, katika ajali kubwa zaidi ya ndege kuwahi kutokea nchini Pakistan.
Ingawa sekta ya safari za anga imekuwa kwa kasi, wakosoaji wanasema viwango vimekuwa chini na haviendani na ukuaji wa huduma.
Marubani hulalamika wanalazimishwa kuruka kwa saa za ziada, jambo linalosababisha uchovu, ingawa mashirika ya ndege yanakana madai hayo.mtiaz Elahi, mwenyekiti wa Capital Development Authority, mamlaka inashughulikia dharura, alisema ajali hiyo "inavunja moyo".
"Ni janga kubwa, na ninaweza kuthibitisha kwa uchungu kwamba hapakuwa na watu waliosalimika," alilieleza shirika la habari la Associated Press.
Ndege hiyo, inayosemekana kuwa ni muundo wa Airbus A321 ikiwa na abiria 146 na wafanyakazi sita ndani yake, inaaminika kuwa iliondoka Karachi saa mbili kasorobo asubuhi majira ya huko.Awali, Wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan, ilisema watu wasiopungua watano walikuwa wamenusurika kifo na kupelekwa hospitalini, lakini maafisa wa maeneo hayo baadaye walisema taarifa hizo hazikuwa sahihi.
Televisheni za maeneo hayo zilionyesha vipande vya mabati na chuma vikining'inia kutoka juu ya miti na kutapakaa ardhini.Kifaa cha kutunza kumbukumbu za safari kimekwishapatikana.
Maafisa wanasema waokoaji waliokuwa wakitafuta watu walionusurika, walikuwa wakitumia mikono mitupu kufukua mabaki hayo. Eneo la ajali lililoko kwenye mlima mkali, halifikiki kwa barabara.

mardi 27 juillet 2010

TUME HURU INAYO ANDAA UCHAGUZI NCHINI BURUNDI CENI YATANGAZA MATOKEO RASMI YA UCHAGUZI WA WABUNGE

BUJUMBURA LE 27.7.2010: Tume huru inayo andaa uchaguzi nchini Burundi CENI imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika siku ya ijumaa iliopita julay 23 mwaka 2010. Matokeo hayo yabaini kuwa chama cha CNDD FDD kimepata viti 81 bungeni huku chama UPRONA kikipata wabunge 17 na chama FRODEBU NYAKURI kikiridhika na wabunge 5. imesalia kuwateuwa wabunge 3 kutoka kabila la watwa wataotoka katika Mikoa ya Cibitoke, Karusi na Mji mkuu Bujumbura. tume hiyo inayo simamia uchaguzi CENI imesema raia walioshiriki uchaguzi wa wabunge imefikia asilimia 66. Ucahguzi wa wanasneta watazamiwa kufanyika siku ya jumanne Julay 28 ambapo kila Mkoa utwakilisha wajumbe 2 kutoka makabila ya wahutu na watutsi. tume huru CENI imetangaza kwamba vyama vya CNDD FDD na UPRONA ndivyo vitavyo wania viti vya uanaseneti. hata hivyo katika baadhi ya Mikoa chama UPRONA kimeshindwa kuorodhesha wajumbe kutoka katika kabila la wahutu. katiba ya Burundi inaagiza kwamba ma rais wa zamani wanaingia barazani moja kwa moja wakimaliza uongozi wao. Domitien Ndayizeye, Jean Baptiste, Pierre Buyoya na Ndibantunganya Syvestre ma rais wa zamani tayari ni wanaseneti.

LEONARD NYANGOMA TAYARI AMEITOROKA NCHI KWA KUHOFIA USALAMA WAKE


BUJUMBURA:Mkuu wa chama cha CNDD Léonard Nyangoma akiwa pia msemaji wa muungano wa vyama kwa ajili ya demokrasia ADC IKIBIRI, vyama amvavyo vilivyo pinga matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa baraza la madiwani wa Mai 23, inasemeka kwamba tayari ameitoroka nchi sasa ni zaidi ya wiki. hii ni kutokana na hofu wa kutiwa nguvuni aidha kumaliziwa maisha zasema duru tofauti. Nyangoma ameitoroka nchi na kujificha kwa kuhofia maisha yake, amethibitisha hayo Alexis Sinduhije mkuu wa chama MSD kinacho jumuika katika muungano ADC IKIBIRI ambae aliliambia shirika la habari la ufaransa la AFP kwamba kiongozi huyo alionekana mara ya mwisho jijini Bujumbura Julay 20. Kiongozi huyo wa upinzani anashutumiwa na utawala baada ya kutowa tamko ambamo aliushutumu utawala kuhusika na mauaji huko Ruziba kwenye umbali wa kilometa 8 kusini mwa mji mkuu Bujumbura ambako ndege ya kijeshi na manuari vilitumiwa ilikuwasaka watu waliokuwa wamehusika katika mauaji ya wanamemba wa chama tawala CNDD FDD. waziri wa ulinzi aliomba afunguliwe mashtaka na polisi ilikuwa tayari kumtia nguvuni licha ya kinga ya muda alionayo kama mbunge.

mercredi 21 juillet 2010

WAZIRI WA ULINZI NCHINI BURUNDI AOMBA KESI UFUNGULIWE DHIDI YA MWANASIASA WA MRENGO WA UPINZANI LEONARD NYANGOMA

waziri wa ulinzi nchini Burundi meja jenerali Germain Niyoyankana ameitaka mahakama nchini humo kumfungulia kesi kiongozi wa upinzani wa chama CNDD bwana léonard Nyangoma kwa kile alicho kisema kiongozi huyo amekuwa akikashifu jeshi la Burundi. Hii ni baada ya kiongozi huyo wa mrengo wa upinzani kutowa matamshi kuhusu matukio ya ndege ya kijeshi iliovurumisha ma bomu na kuwamalizia maisha watu kadhaa. waziri wa ulinzi wa Burundi amesema mwanasiasa huyo alikuwa na malengo ya kuamsha hisia mbaya za wananchi hivo wakaidi serikali pindi alipo sema kwamba serikali ya Burundi yajihusisha na mauaji dhidi ya raia. Jeshi la burundi liliendesha siku za nyuma operesheni ya kuwasaka vijana waliosadikiwa kuhusika katika vitendo tofauti vya mauaji jijini Bujumbura vikiwemo vile vya ulipuaji ma bomu. Ndege za kijeshi na manuari ya kivita ilitumiwa ili kuwazuia vijana hao ambao inasadikiwa kuwa walikuwa na dhamira ya kutimkia nchini DRC wakipitia ndani ya ziwa Tanganyika. Hadi sasa haijulikani ni watu wangapi walioyapoteza maisha katika operesheni hiyo.

dimanche 18 juillet 2010

JEAN CLAUDE KAVUMBAGU MHARIRI WA GAZETI NET PRESS AKAMATWA NA KUTIWA NGUVUNI

Mhariri wa gazeti la Net Press Jean Claude KAVUMBAGU alikamatwa jana jumamosi july 17 na polisi ya taifa kwa tuhuma ya kwamba alichapisha katika gazeti lake taarifa inayosema kwamba jeshi la Burundi na polisi vimezamilia hasa katika uporaji na mauwaji dhidi ya wananchi kuliko kulinda nchi yao. Mwanahabari huyo alikamatwa akiwa ofisini mwake. Wakili wake mtetezi Gabriel SINARINZI akihojiwa kuhusu kukamatwa kwa mteja wake na muungano wa redio za nchini Burundi amefahamisha kwamba Jean Claude KAVUMBAGU amekamatwa kinyume cha sheria kwani alipelekwa moja kwa moja katika jela kuu la Mpimba wakati kesi yake ilikuwa bado haijakatwa. Itafahamika kwamba Jean Claude KAVUMBAGU alihojiwa kwa muda wa masaa mawili kabla ya kupelekwa mbaroni.