
Baraza la Seneti limeidhisha majina yaliopendekezwa na rais wa jamuhuri Pierre Nkurunziza kwenye nyadhifa mbalimbali. Waziri wa ulinzi meja jenerali Germain Niyoyankana aliwasilisha kikaoni jina la Brigadia jenerali Ndegeya diomède ambae alipendekezwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwa kaimu mkuu wa majeshi ya Burundi. Brigadia jenerali Ndegeya Diomede aliidhinishwa kuwa kaimu mkuu wa majeshi ya Burundi. Upande mwigine, waziri wa mambo ya ndani Edourd Nduwimana aliwasilisha majina ya walipendekezwa na rais kuiwakilisha Burundi ugenini. Nibizi Isidore na Bashimiyubusa Denis kutoka chama FNL wamepasishwa kuiwakilisha Burundi ugenini. Elias Buregure wa chama CNDD-FDD ambae aliwahi kuwa mea wa jiji la Bujumbura kabla ya kuwa waziri mdogo wa kazi za serikali amekataliwa na wanaseneti kuiwakilisha Burundi ugenini kwa kushtumiwa katika kesi mbalimbali za ubadhilifu mali ya umma. kulingana na habari kutoka kwa wanaseneti Elias Buregure alijihusisha na rishwa katika utowaji viwanja vya ujenzi wakati alipokuwa waziri mdogo wa kazi za serikali ambae alipingana na waziri mkuu kwenye wizara hiyo katika kuchukuwa maamuzi. Baraza la seneti limeidhinisha pia majina ya ma gavana wa Mikoa ya Mwaro, Makamba na Cibitoke. Nahayo Fredine ataongoza Mkoa wa Mwaro ni kutoka chama FNL, Ntahitaja Térence ataongoza Mkoa wa Makamba ni kutoka chama CNDD–FDD, huku Bizimungu Simon akiidhishwa kuongoza Mkoa wa Cibitoke, akiwa ni mwanachama wa FNL.
