vendredi 17 avril 2009

WANASENETI WA BURUNDI WAYAKATAA MAJINA KADHAA YALIOPENDEKEZWA NA RAIS KWENYE NYADHIFA TOFAUTI KARENGA RAMADHAN AKIWEMO.


Baraza la seneti nchini Burundi limejadili alhamisi hii April 16 majina ya watu waliopendekezwa na rais wa jamuhuri ya Burundi kwenye nyadhifa mbalimbali , ikiwa ni kwenye uongozi wa Mikoa kadhaa ya Burundi, aidha uwakilishi wa Burundi ugenini pomoja na kwenye uongozi wa jeshi la taifa.
Waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana alikuwa amewasilisha majina ya watu waliopendekezwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuongoza mikoa ya Makamba, Ruyigi na Kayanza.
Reverien Ndikuriyo alikuwa amependekezwa kuongoza Mkoa wa Makamba.
Fenele Nduwimana alipendekezwa kuongoza Mkoa wa Kayanza.na Syriaque Nshimirimana alipendekezwa kuwa gavana wa Mkoa wa Ruyigi. Majina ya waliopendekezwa kuwa wanabalozi wa Burundi ugenini ni , ni pamoja na Karenga Ramadhani aliewahi kuwa mkuu wa itifaki kwenye ofisi ya rais wa jamuhuri kabla ya kuwa waziri wa habari na msemaji wa serikali na hatimaye waziri anaye husika na uhusiano wa kikanda.
Mwingine ni Angel Niyuhire ambaye ni mbunge kutoka chama Uprona pamoja na Gahutu zacharie. Wakati huo waziri wa ulinzi meja jenerali Jermain Niyoyankana aliwasilisha majina ya Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye ni Naibu mkuu wa majeshi, alipendekezwa kuwa mkuu wa majeshi ya Burundi kuchukuwa nafasi ya Brigadia jeneral Samuel Gahiro alieteuliwa ku afisa wa kijeshi kwenye ubalozi wa Burundi mjini Tripoli. Mwingine ni meja jenerali Niyoyunguruza Juvenal aliependekezwa kuwa kaimi mkuu wa majeshi.
Miongoni mwa majina hayo, Juvenal Niyoyunguruza amekataliwa na wanaseneti kuwa naibu mkuu wa majeshi wakimtuhumu ya kwamba hayati Melchior Ndadaye rais wa kwanza wa Burundi kuchaguliwa chini misingi ya kidemokrasia aliuawa katika kambi ambayo alikuwa kamanda bila kuzuia mauaji hayo. Mwingine aliekataliwa ni Karenga Ramadhani, kuiwakilisha Burundi ugenini wanaseneti wakimtuhumu kwa matamshi aliyoyatowa wakati alipokuwa waziri wa habari na msemaji wa serikali kuhusu mkasa wa mauzo ya ndege ya rais Falcon 50, Naye Reverien Ndikuriyo amekataliwa kuongoza Mkoa wa Makamba baada ya jina lake kutajwa katika mkasa wa shirika la IDC lililo walaghai wananchi katika mikoa na kuwapora pesa .

Aucun commentaire: