mercredi 12 novembre 2008

WAFANYABIASHARA WA MAFUTA WAFUNGUA VITUOVYAO KWA KUHOFIA HATUWA YA SERIKALI

Serikali iliazimia kupunguza bei ya mafuta aina ya essence hadi 1700, huku bei ya mafuta aina ya mazout ikipungua hadi 1500. hali hii ilipelekea hata bei ya usafiri mjinikati kupungua hadi 240, wakati hapo awali ilikuwa kwenye 280. kilicho dhihirika baada ya hatuwa hiyo ya serikali ni kufungwa kwa vituo vya mafuta, wamiliki wa vituo hivyo walidai kuwa watafilisika iwapo watauza mafuta wanayo kwa bei mpya wanayo. Uhaba wa mafuta ukadhihirika mjini kote. Lita moja ua mafuta kwenye masoko ya magendo, ilifikia hadi franka elfu nne. shirika la wanunuzi ABUCO lilitowa taarifa ambamo lililaani vikali hali hiyo na kuitolea mwito serikali wa kuitaka ichukuwe hatuwa za kisheria dhidi ya wafanyabiashara ya mafuta ambao ilisema taarifa hiyo ya ABUCO wamekaidi hatuwa ya serikali. Baada ya usumbufu mkubwa mjini Bujumbura wa kupata mafuta, hatimae serikali kupitia waziri wa baishara na viwanda bibi Euphrasie BIGIRIMANA iliazimia hatuwa za kisheria na kutishia kumtoza faini mfanya bishara yoyote yule ataekutwa kafunga kituo chake na ilihali mafuta anayo kama ilivyo dhihirika. hatuwa hiyo ni pamoja na kutozwa faini ya franka elf 50 hadi milioni 5 franka za Burundi na kifungo cha zaidi ya miaka miwilijela.

mercredi 15 octobre 2008

CHAMA KIKUU CHA UPINZANI NCHINI BURUNDI FRODEBU KIMEMTEUWA DOMITIEN NDAYIZEYE KUWA MTETEZI WAKE KWENYE UCHAGUZI WA MWAKA 2010.
Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi Sahwanya FRODEBU kimemteuwa rais wa zamani wa Burundi Domitien NDAYIZEYE kusimama kwenye uchaguzi wa 2010 utaofanyika nchini Burundi.
katika uchguzi wa wajumbe wa kamati tendaji uliofanyika jumapili octoba 12.2008 uliojumuisha wajumbe 268, Domitien NDAYIZEYE lichaguliwa kwa asilimia 86.5 ya kura dhidi ya wagombea wengine wawili Pierre Claver NAHIMANA na Rose NDUWAYO. Baada ya kuteuliwa kwake, rais huyo wa zamani aliviambia vyombo vya habari kuwa, alikuwa ametangaza kuachana na siasa baada ya kuondoka kwenye utawala mwaka 2005, na kufungwa kwake kwenye jela kuu la Mpimba mwaka 2006, sasa amerejea kwenye uwanja wa siasa ili kupambana na rais alieko madarakani wakati huu. FRODEBU ni chama cha kwanza cha upinzani kutangaza rasmi mgombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Domitien NDAYIZEYE aliiongoza Burundi tangu mwaka 2003 hadi Agosti 2005 wakati wa awamu ya pili ya kipindi cha mpito, kipindi ambacho kilihitimshwa kwa uchaguzu uliopelekea chama CNDD-FDD kunyakuwa ushindi.

PALIPEHUTU/FNL YAPINGA KATAKATA KUBADILI JINA

katika mkutano uliitishwa na katibu mkuu wa palipehutu FNL Jonas NSHIMIRIMANA jumanne 14 octoba, aliwaambia waandishi habari kuwa kamwe Palipehutu FNL haitothubutu kubadili jina hilo, na kwamba iwapo watafanya hivyo, basi watakuwa wamekwenda kinyume na mkataba, kwa kuwa mikataba yote waliosaini na serikali ya Burundi walitumia jina hilo Palipehutu/FNL na itakuwa ni kuvunja mkataba wakati ambapo hawana nia ya kuvunja mkataba huo. Seriklai ya Burundi imelipa sharti kundi hilo kubadili jina kabla ya kukubaliwa rasmi kama chama cha kisiasa, kwa kuwa kama inavyo sema taarifa ya serikali ni kinyume cha katiba ya Burndi iwapo kitasainiwa chama chenye jina la kikabila. Licha ya kukwama kwa mazungumzo ya palipehutu/FNL na serikali ya Burundi, Jonas NSHIMIRIMANA amesema kuwa majadiliano yataendelea hadi pale serikali itaitambua Palipehutu/FNL kama chama rasmi cha kisiasa. Katibu mkuu wa Palipehutu FNL ametumia fursa hiyo kukanusha habari kwamba kuna mzozo wa ndani katika kundi hilo la palipehutu FNL ambapo mwenyekiti wa kundi hilo Agathon RWASA na msemaji wa palipehutu FNL Pasteru HABIMANA hawapatani na kwamba kila mmoja anafuyawafuasi wake. Kiongozi huyo amekanusha habari hizo na kusema kuwa huo ni uzushi mtupu.
MIAKA 3 IMEMALIZIKA CHAMA CNDD-FDD KIWA KWENYE UTAWALA NCHINI BURUNDI
Chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimeazimisha myaka 3 Jumapili tarehe 12 Octoba 2008 kikiwa kwenye usukani wa kuiongoza Burundi. sherehe rasmi za siku kuu hiyi zimefanyika katika Mkoa wa Gitega Kaskazini mwa Burundi. Wafuasi wa chama hicho kutoka katika kila mikoa ya Burundi walimiminika kwa wingi kuhudhuria sherehe hizo. Wajumbe wa vyama vingine vya upinzani walialikwa kwenye sherehe hizo. chama kinacho tawala nchini Jamuhuri ya Kimokrasia ya Congo PPRD kiliwatuma wajumbe wake kushiriki kwenye sherehe hizo ambazo zilionekana kufana kiasi fulani. halaiki ya watu walimiminika kwenye uwanja wa mpira wa miguu Mkoani Gitega huku wakivalia sare za chama CNDD-FDD. Akiwahutubia wafuasi wake mwenyekiti wa chama CNDD-FDD Jéremie NGENDAKUMANA alisema kuwa siku hiyo ni siku ya furaha kwa kila mwananchi na hasa wanachama wa CNDD-FDD kwa kuwa ni mara ya kwanza utawala uliochaguliwa katika misingi ya kidemokrasia unafanya zaidi ya miezi 3 madarakani. aliwaambia wafuasi wa chama kuwa wavivu hawana nafasi katika chama, nakwamba lazima watumike kwa bidii katika kuendeleza mipango ya nchi. miaka mitatu hii imemalizika wazazi wanajinfua bila malipo, huku watoto wakisoma bila kutowa hata mea na hata watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 wanatibiwa bila malipo. Jéremie NGENDAKUMANA amewapa kasopo wafuasi wa upinzani ambao wamekuwa wakiimba uchaguzi wakati huu na ilihali kumesalia muda wa miaka 2 wa utawala wa chama hicho kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi. Upande wake rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA ambae ni mfuasi wa chama hicho, alisema kuwa miaka 3 kwenye utawala ni midogo kwa kuwa safari bado ingali ndefu; lakinihata hivo lazima ashukuriwe Mungu. Rais NKURUNZIZA amewatahadharisha wale wote ambao alisema wamekuwa wakimuwekea vizingiti na mitego katika utawala wake, na kwamba wafahamu kuwa wakiendelea kutezga mitego hiyo basi watajikuta wao ndio ambao wameanguka wa kwanza ndani yake. sherehe hizo zlihitimishwa kwa kutowa zawadi kwa walioendesha kzi zao vizuri katika kipindi chote hiki. Miongoni mwa waliopewa zawadi ni Rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA alievalishwa midali, huku wengine kama seneta Muhamed Rukara, Gervais RUFYIKIRI na Pie NTAVYOHANYUMA wakipewa picha zinazo maanisha kuwa wameshukuriwa na chama katika kazi zao.

jeudi 9 octobre 2008

HATUWA KADHAA ZACHUKULIWA ILI KUWALINDIA USALAMA MA ALBINOS
Viongozi waliokuwa wkikutana mjini Ruyigi juzi jumanne na jumatano katika mkutano na wa wakilishi wa ma zeruzeru,hatimae wameazimia hatuwa za muda ili kuwalindia uslama mazeuzeru ambao wanakabiliwa na uslama mdogo Mkoani Ruyigi na hata Mikoa mingine mathalan Cankuzo. Kwa mujibu wa kiongozi wa shirika la ma albinos nchini nchini Burundi Kazungu Kassim, amesema kwamba miongoni mwa hatuwa zilizo chukuliwa ni kuwapatishia nyumba mojawapo katika tarafa ya Ruyigi ambako watalindiwa usalama zaidi. Kiongozi huyo aliwatolea mwito ma albinos popote pale walipo kutosita kujisalimisha kwenye makao makuu ya tarafa pindi tu watapojihisi kuwa usalama wao upo hatarini. Kiongozi huyo aliendelea kusema, wakati huu wanahitaji misaada ya kukidhi mahitaji ya ma albinos hao ambao wamekusanywa pamoja. Kiasi ma albinos 48 ndio ambao wanahesabiwa kueshi katika Mkoa huo wa Ruyigi. Kwa sasa wamekwisha kusanyika ma albinos zaidi ya 10 kwenye nyumba hiyo iliochukuliwa kama kituo cha kuwahifadhi ma albinos.

JOSE CAMELEONE AVUNJIKA MIGUU BAADA YA KUOTA AKITEMBEA.

Mwanamuzki huyo wa Uganda alikuwa nchini Tanzania kwa mianajili ya tamasha mbalimbali alijurusha toka kwenye ghorofa ya tatu kwenye Hoteli ya Impala mjini Arusha. duru kutoka Arusha zaarifu kuwa mwanamuziki huyo aliingia kupumzika muda mchache akitokea kuendesha Show, na ndipo akaota kuwa yuko anatembea, baadae akaanguka kwenye ghorofa hiyo. baadae alipelekwa haraka Hospitalini. lakini kabla hajaanza kupata matibabu mkewe alikuja na ndege kutoka Kampala hadi kwenye Hospitali hiyo na kumpeleka Uganda kwenye hospitali mojawa kuu nchini hapo ambako anaendelea kupata matibabu.

VYAMA VYA KISIASA NCHINI BURUNDI VYA IFASIRI HATUWA YA KUZUIA MIKUTANO YA HADHARA KUWA IMEPITWA NA WAKATI
Waziri wa mambo ya ndani na maendeleo ya vijiji Venant Kamana alitangaza kwamba hakuna mikutano yoyote ile aidha maadamano yoyote ya vyama vya kisiasa ya hadhara yatakubaliwa tena kuendeshwa holela bila kuwa na kibali rasmi, na kwamba siku za maadamano ni jumamosi na jumapili. Maandamano aidha mikutano uya siku ya jumamosi yatakubaliwa kuazishwa saa tano hadi saa kumi na mbili jioni, na siku ya jumapili ni kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Kama alivyo kazia tangazo lake hilo waziri wa mambo ya ndani amesema kuwa hii ni kuepusha vurugu ambazo zaweza kujitokeza katika siku zijazo kutokana na mikutano ya vyama vya kisiasa. Mkurugenzi mkuu kwenye wizaraTérence Mbonabuca, upande wake alisema kuwa hatuwa hiyo ilichukuliwa baada ya kujadiliana na viongozi mbalimbali wa vyama vya kisiasa. hatuwa hii imepokelewa kwa shingo upande na vyama vya kisiasa. Mwenyekiti wa chama SAHWANYA FRODEBU Léonce NGENDAKUMANA amesema kwamba hatuwa hiyo anayo jaribu kuchukuwa waziri wa mambo ya ndani na maendeleo ya vijiji ni ya zamani wakati ambapo Burundi ilikuwa ndio bado inaingiza mguu katika mfumo wa kidemokrasia ambapo serikali ya zama hizo iliamuru kupinga maandamano na mikutano ya vyama vya kisiasa lakini wakati huu Burundi imepiga hatuwa kubwa, hakuna budi kuendelea mbele kuliko kurejea nyuma, na kwamba hakuna sheria ya kiwaziri ambayo yaweza kufuta sheria ya katiba aidha sheria kuhusu vyama vya kisiasa. Léonce NGENDAKUMANA ameendelea kusema kua iwapo waziri wa mambo ya ndani ameona umuhimu wa kubadili badhi ya sheria ni kusukuma mapendekezo yake bungeni ili yajadiliwe. Kiongozi huyo amesema chama FRODEBU kitapinga hatuwa zozote zile za kuzuia mikutana na maadamano ya vyama visivyo unga mkono chama kilicho madarakani. maoni kama hayo yalitolewa pia na msemaji wa chama CNDD Francois BIZIMANA
WAFUNGWA ZAIDI YA 15 WAJERUHIWA KATIKA JELA KUU LA MPIMBA MJINI BUJUMBURA
Katika uchunguzi ulioendeshwa kwenye jela kuu la Mpimba baada ya kutokea vurugu siku ya jumapili ambapo risase na hata bomu zilisikika jelani hapo, wafungwa wa tano wamegunduliwa kuhusika na vurugu hizo pia na kukutwa na shughuli za kutengeneza noti za magendo katika jela hilo la Mpimba. Duru kutoka kwenye jela kuu la Mpimba zimearifu kuwa kiini cha vurugu hizo ni mfungwa ambae aliagiza simu 4 za mkononi kwa mtu ambae aliekuwa amekwenda kumuona nduguye, baada ya kumpa pesa, na kuondoka ndipo akagunduwa kwamba noti zile alizo pewa sio noti halali, akamuwa kuzirudisha huko Mpimba. Alietowa pesa hizo akakana kurejesha simu, baadae ndipo wenzake walimuunga mkono na kuanzisha vurugu. Lakini hata hivo duru zaidi zimesema kuwa kiini cha vurugu hizo ni mzozo uliotokea bainaya wafungwa wakati wa kugawa simu za mkononi na pesa walizo zipata kutokana na suhghuli zao hizo za utengenezajiwa noti bandia. Polisi ililazimika kuingilia kati kwa kuvurumisha risase hewani kama zilivyo endelea kuarifu duru kutoka katika jela kuu hilo la Mpimba. Wafungwa zaidi ya 15 walijeruhiwa katika tukio hilo mmoja akiwa katika hali mbaya.
SERIKALI YA BURUNDI YAANDAA MABADILIKO KATIKA UTOWAJO MISHAHARA

Serikali ya Burundi imo mbioni kuandaa mradi mpya utaopelekea wafanyakazi wake kusalia nhini Burundi badala ya kufikiria kwenda ugenini aidha kutumikia mashirika ya wahisani ambayo hutowa donge nono zaidi kulikoni hapa nchini. Hii inatokana hasa na mshara mfinyu wanao pewa wafanyakazi wa serikali. Hayo yamefahamishwa na Pierre NTIRABAMPA Mkurugenzi mkuu kwenye wizara ya kazi wakati akiyajibu maswali ya waandishi habari katika kipindi mojawapo kilichokuwa kikitasmini hali halisi ya mfanyakazi wa serikali na jinsi gani ya kuboresha kazi na kupelekea mfanyakazi wa serikali apate nafuu katika utekelezwaji wa kazi zake. Kipindi hicho kilikuwa kimeandaliwa na muungano wa mashirika yanayo tetea haki za wafanyakazi COSYBU.

dimanche 5 octobre 2008

USALAMA

WALINZI 3 WA SHIRIKA LA KK SECURITY WATIWA MBARONI KWA KUSHUKIWA KUHUSI NA WIZI WA PIKIPIKI 4 MKOANI RUTANA.

Polisi ya usalama wa raia Mkoani Rutana ilifaulu kukamata pikipiki 4 mpya katika usiku wa kuamkia ijumaa, zilizo ibiwa katika usiku huo kwenye shirika la GTZ Mkoani Rutana. Watu 3 wa shirika la Ulinzi la KK Security na mhusika wa shuhuli za kunyunyuzia maji bustani katika shirika la GTZ wamewekwa mbaroni kwa kushukiwa kuhusika na wizi wa pikipiki hizo mpya ambazo zilikamatwa kwa mchango mkubwa wa raia Mkoani hapo. Kama alivyo fahamisha afisaa wa polisi ya usalama Mkoani Rutana Sylvestre NZOHABONAYO, waliipokea simu kutoka kwa raia ambae aliwafahamisha kuona hali ya sintofahamu ambapo pikipiki mpya zinasukumwa usiku wa saa nne unusu, zikitokea kwenye makao makuuya shirika la GTZ Mkoani Rutana zikielekezwa katika kata ya Birongozi. Kiongozi huyo aliamuru kikoso chake kuripoti haraka, wezi hao walifaulu kitimka baada ya kuwaona askari polisi. Baadae polisi walipojielekeza kwenye shirika hilo la GTZ, ndipo walinzi wakajaribu kutimka bila mafaanikio, kwa kuwa, polisi ilikuwa imetanda eneo zima la shirika hilo. Baada ya kuendesha msako zaidi ndipo iligunduliwa pikipiki nyingine ambayo ilikuwa kweye kituo cha mafuta mkoani hapo, huku kukiwa na lori aina ya Fuso ambayo ilikuwa ikisubiri kusafirisha pikipiki hizo hadi nchini TZ. Kiongozi wa walinzi hao, alijaribu kuwatetea wafanyakazi wake bila mafaanikio kwa kuwa, imedhihirika kwamba nae huenda anahusika kwa vile, kama wanavyo sema walinzi hao walilazimishwa kufungua milango na watu 6 wenye silaha. Lakini hata hivo, haieleweki kwanini hawakufahamisha idara za uslama mapema na ilihali uwezo walikuwa nao, huku pia wakijaribu kutimka wakati walipowaona polisi wa uslama wa raia, kwa nini watimke. Uchunguzi unaendelea huku pikipiki hizo zikipelekwa kwenye idara ya polisi.

jeudi 2 octobre 2008

SHEREHE ZA ID-IL FITRI ZAFANYIKA VEMA LICHA YA SERIKALI KUTOKUWEPO
Kama ilivyokuwa kawaida kila mwaka, jamii ya waislam nchini Burundi COMIBU huitolea serikali taarifa katika maadhimisho ya siku kuu ya Idil Fitri inayo maanisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. hata hivo kumekuwa na mtafaraku kila mwaka inapo wadia kufungua mwezi ambapo inafikia waislam kufunga siku 30 ao 29, hili linaeleweka, lakinikwa sasa kumekuwemo na mambo ya siasa ndani yake. waislam walifurika kwa wingi kuendesha ibada yao ya sala ya laidi kama ilivyokuwa kawaida. jumuia ya waislam nchini Burundi COMIBU iliwatangazia waislam viwanja maalum ambavyo vitaendeshewa ibada na ma shekh ambao wataendesha ibada hiyo. inakubalika wazi kwamba sherehe rasmi hufanyika kila mwaka Mtaani Jabe, eneo kubwa linalo kusanyikia waumini wengi. mwaka huu kama ilivyo staajabisha wengi sherehe rasmi ziligeuzwa na kupelekewa kwingine. serikali ilimtuma muwakilishi wake huko kwingine. hili halikupelekea sherehe kutofana, badala yake sherehe kwenye uwanja wa idi zilipendeza kiasi kwamba Cheikh Issa Salum BAGORIBARIRA alikuwa ameandaa hutba yake fupi yenye kujawa na ujumbe mzito, ilimalizika huku waumini wakihitaji aendelee. Waumini wa kiislam wamepinga kuendesha malumbano kutokana na hilo kwa kuwa kama walivyo ieleza blogi hii, wanayo matatizoi mengine ndani ya jamii ambayo yawakabili, na kuzidi kuwa hilo ni lidogo, kwa kuwa Uislam ulikuwepo tangu kabla ya utawala uliopo, na Uislam utasalia ulipo huku utawala uliopo ukitoweka.

jeudi 25 septembre 2008

WARUNDI 20 WALIOFUKUZWA NCHINI TANZANIA WAWASILI MKOANI RUTANA KUSINI MWA BURUNDI


Raia takriban 20 waliofukuzwa nchini Tanzania, wamewasili jana jumatano asubuhi tarehe 24/9/2008 katika mkoa wa Rutana kusini mwa Burundi bada ya kutembea kwa mguu kwa muda wa siku 15. Raia hao wengi wao ni watoto na wanawake waliokuwa wakiishi nchini Tanzania tangu mwaka 1995 katika kijiji cha Bukiriro wilaya ya Ngara Mkoani Kagera. Raia hao walifukuzwa nchini Tanzania tangu tarehe 9 mwezi wa 9 na wamedai kuwa wazaliwa wa mikoa ya Cibitoke na Ngozi na kwamba walifurushwa na watu wa jamii ya wanangambo waliowapora mali na vitu vyao.
Shughuli za ujenzi wa soko la Buyenzi zimekamilika. kinacho salia ni shirika la mamlaka ya maji na umeme REGIDESO paomja na manispaa ya jiji la Bujumbura kushughulikia maswala ya umeme na maji katika soko hilo muhimu kwa uchumi wa nchi. hayo yamethibitishwa na Anatole MPERAMIHIGO ambae alikuwa akisimamia shughuli za ujenzi wa soko hilo. Lakini hata hivo kumekuwa na uvumi kwamba shughuli za ujenzi wa soko hilo la Ruvumera zilikamilika tangu kitambo, uzinduzi rasmi unacheleweshwa kutokana na hali ya viongozi wa kuu serikali kujipa viwanja zaidi ya vitano kila mmoja ambapo waliokutwa katika soko hilo kabla hata halijakarabatiwa huenda wakakosa viwanja.
MSEMAJI WA PALIPEHUTU/FNL ATHIBITISHA KWAMBA WANAO MA AFISAWA WA KIJESHI KATIKA KUNDI LAO.

Akizungumza na redio Burundi jumatano hii tarehe 24/9/2008, msemaji wa palipehutu/FNL Pasteur HABIMANA amesema kuwa katika idadi walioitowa ya jeshi lao wanao ma afisa wakuu wa jeshi, ambao hawahitaji mafunzo ya kuwa ma afisa. hayo ni baada ya serikali ya Burundi kutowa taarifa ambamo iliwataka vijana kujiunga na chuo kikuu cha kijeshi ISCAM wakiwemo vijana kutoka kundi hilo la palipehutu/FNL. msemaji huyo wa FNL alisema kuwa majadiliano baina ya seriklai ya Burundi na kundi hilo yaendelea vema licha ya kasoro kadhaa ambazo zimekuwa zikijitokeza. miongonimwa kasoro hizo amesema Pasteur HABIMANA ni kuitwa kwa kundi lao palipehutu/FNL. amezidikuwa haoni pengamizi popote lilipokwa kuwa kila wanapo itishwa katika mikutano aidha kongamano lolote huitwa kama palipehutu FNL, alisema na hata wakati wa mechi baina ya wanajeshi wa Burundi na wapiganaji wa kundi lao waliitwa kuwa wapiganaji wa palipehutu FNL.

mercredi 3 septembre 2008

POLISI YA USALAMA WA RAIA YAMMALIZIA MAISHA JAMBAZI BAADA YA KUWAPORA HABIRIA KWENYE BARABARA ITOKAYO BUJUMBURA KUELEKEA GATUMBA
Majambazi wenye silaha waliendesha mtego siku ya jumamosi tarehe 30/8/2008, kwenye barabara itokayo mjini Bujumbura kuelekea tarafani Gatumba. basi moja la habaria lilianguka kwenye mtego huo. habiria waliokuwemo ndani ya basi hilo waliporwa pesa, simu za mkononi na vitu mbalimbali vya thamani waliokuwa navyo. baada ya shambulio hilo, jeshi la taifa eneo hilo liliingia kati na kumuua jambazi mmoja ambae alikuwa amevalia sare za jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hata hivo raia wa Gatumba waliokuja kushuhudia tukio hilo walithibitisha kwamba jambazi huyo alieuliwa ni mkaazi wa kata ya Gatumba. mnamo siku zote hizi za nyuma kumekuwa na hujuma mbalimbali ambazi zimekuwa zikiendeshwa na majambazi wenye silaha katika barabara tofauti zinazo toka mjini Bujumbura kuelekea mikoani.

lundi 18 août 2008



MAZUNGUMZO YA VYAMA VYA KISIASA YAZINDULIWA MKOANI GITEGA

Bujumbura le 18/8/2008. Kumeanzishwa hii leo Mkoani Gitega mazungumzo yanayo jumuisha wawakilishi wa vyama vya kisiasa vilivyo sajiliwa kisheria hapa nchini, ili kujadili kwa pamoja kuhusu maswala mahimu yanayo ikumba Burundi wakati huu. Mwenyekiti wa chama UPRONA Aloys Rubuka ameomba chama kilichoko madarakani na viongozi mbalimbali waonyeshe utashi wa kutaka kuheshimisha maazimio yanayo chukuliwa katika mijadala tofauti na kwamba ni lazima chama madarakani kielewe vema madhumuni ya mazungumzo hayo, kinyume na hivo majadiliano hayo yatakuwa kama kuongeza mzigo juu ya ungine, amesema hayo mwenyekiti wa chama UPRONA Aloys Rubuka. Upande wake mwenyekiti wa chama Sahwanya FRODEBU Léonce NGENDAKUMANA amesema kuwa katika mazungumzo hayo watasisitiza kuhusu kutatua matatizo yalioko nchini ambayo yaweza kuwa pengamizi kwa majadiliano hayo. Amesema miongoni ni pamoja na swala la usalama kuhusu mkataba na uheshimishwaji wa kusitisha vita baina ya serikali na Palipehutu FNL, maswala ya Utawala bora na matumizi ya pesa ya serikali kwa mantiki binafsi. Léonce NGENDAKUMA amesema watasisitiza ili maswala hayo yagusiwe, badala yake amesema mazungumzo hayo yatakuwa ni nyongezo isiokuwa na faida. Amemalizia kusema mchango wa chama FRODEBU utakuwa ni uleule ambao FRODEBU imekuwa ikiutoa kila mara inapo pata fursa ya kujadiliana.
Ama kuhusu Upande wa chama madarakani CNDD-FDD msemaji wake Onesime NDUWIMANA amesema kuwa chama chake kitashiriki kikamilifu katika mazungumzo hayo kwa njia ya kudumisha amani na utulivu jote nchini na wala chama CNDD-FDD hakiwezi kamwe kutia pengamizi lolote katika mazungumzo hayo.


WAKATI SENSA YA WANANCHI NA MAKAAZI YAARIFiWA KUFANYIKA VEMA KOTE NCHINI MKOANI MURAMVYA KUNA KASORO

Bujumbura le 18/8/2008.
Sensa ya wananchi na makaazi iliozinduliwa juzi jumamoso yaendelea kufanyika barabara kote nchini. Wale ambao wataopinga kufanya sensa hiyo wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria iliosainiwa Septemba 25 mwaka jana. Amesema hayo Térence MBONABUCA afisa msimamizi wa sensa hiyo. Wakati hayo yakiarifiwa Mkoani Muramvya kuna mwalimu mmoja ajulikanae kwa jina la Jonas NIZIGIYIMANA ambae amekuwa akiendesha shughuli za kuwahamasisha wananchi wasusie sensa ya wananchi na makaazi. Habari zaidi kutoka mkoani hapo zarifu kuwa mwalimu huyo alianza shughuli hizo mapema, pindi tu alipo kataliwa kuorodheshwa kwenye idadi ya watao endesha sensa baada ya kwamba alishindwa mtihani. Upande wa ofisi inayo husika na sensa mkoani hapo Muramvya waarifu kuwa mtu huyo hakuwa na alama za kumuwezesha kuendesha sens ya wananchi na makaazi. Wananchi wa eneo hilo wameonekana kutii wito wa mwalimu huyo, baada ya wengi kutojibu maswala kadhaa muhimu wanayo ulizwa na ma afisa wanaoendesha Sensa. Wakati huo huo Mratibu wa Sensa ya wananchi na makaazi katika mkoa wa kusini mwa nchi wa Makamba Dominique NIYONDIKO amesema kuskitishwa kuona hadi sasa kunabaadhi ya wananchi ambao hawajatambua vema umuhimu wa sensa. kuna watu ambao wamekuwa wakitapakaza fikira potovu eti kwamba majumba yaliopakwa chaki wakati wa kuandika namba ndio, ambayo yamo mbioni kubomolewa, huku waumini wa baadhi ya madini ya kikristo wakiarifu kuwa hayo yanayo fanyika ni kinyume na neno la Yesu Christo. Mratibu huyo wa maswala ya sena mkoani hapo amewatolea mwito viongozi wa ngazi za china, kuwahamasisha wananchi vya kutosha ili waitikie kwa wingi sensa hiyo muhimu kwa nchi na wananchi.

POLISI YA BURUNDI YATAKA KUJUWA IDADI RASMI YA JESHI LA POLISI.

Bujumbura le 18/8/2008.Wakati kunafanyika hapa nchini ,kama ulivosikia , sensa ya kujua idadi kamili ya wakaazi wa Burundi wakati huu,polisi nao wameanzisha sensa ya kuitambua idadi rasmi ya jeshi la polisi nchini hapa. Mbali na maswali kadhaa watakayoyajibu , polisi watatakiwa kueleza wanatokea kabila gani ili kujaaribu kuweka usawa kwenye uwakilishi wa makabila katika taasisi hiyo ya usalama wa taifa. Sensa hiyo itashuhudia pia uanzishwaji wa vyombo vya kukagua polisi katika vitua mbalimbali. Kama alivyo fahamisha msemaji wa jeshi la polisi Pierre Chanel Ntarabaganyi kuna umuhimu mkubwa sana wa kujuwa idadi rasmi ya polisi na tabaka zao ili kuheshimisha mikataba inayo agiza asilimia 50 kwa wahutu na asilimia 50 kwa watutsi

JESHI LA TAIFA LA ANDAA MIJALA NA RAIA

Bujumbura le 18/8/2008.Katika hali ya kudumisha nidhwamu jeshini, pamoja na kudumisha uhusiano bora ulioko baina ya wanajeshi na raia, wizara ya ulinzi imeanzisha mijadala tofauti wakishiriki wawakilishi wa mashirika ya kiraia na wananchi wa kawaida. Kama alivyo fahamisha kanali Mponimba Athanase ambae aliendesha mjadala, mazunzungumzo hayo yanamadhumuni ya kuwafahamisha wananchi kuhusu juhudi zinazo fanywa katika mageuzi ya jeshi la taifa, juhudi ambazo zinaelekea ku vifanya vikosi vya taifa viwajibike barabara na jinsi gani ya kueshi na raia. Amesema afisa huyo kwamba jeshi la tumikia raia, na wananchi ndio ambao watowa uwezo kwa jeshi kwa hiyo, amesema ni lazima wananchi watambuwe vema janayo jiri jeshini. lakini hata hivo kumekuwa na maswala ambayo mtu aweza kujiuliza, hadi muda wote huu inamaanisha kwamba idadi ya polisi hawakujulikana?

mercredi 16 juillet 2008

PALIPEHUTU/FNL WAPEWA CHAKULA KWA MARA NYINGINE TENA.


Bujumbura le 14/7/2008. Shughuli za kuwapa chakula wapiganaji wa palipehutu/FNL zimeanzishwa tena jumatatu hii. Hayo yamefahamishwa na msemaji wa kundi hilo Pasteur HABIMANA. Akizungumza katika mahojiano kupitia njia ya simu kwenye redio Burundi, Pasteur HABIMANA alisema kuwa muakilishi wa msuluhishi nchini Burundi Kingslay Mamaboulo alishindwa kuzibiti hali ya mambo wakati alipo safiri muakilishi maalum wa umoja wa Afrika nchini Burundi Mamadou Ba na kutofahamisha mapema kwamba chakula kiliopo kimekwisha. Kusitishwa kwa shughuli hizo kulipelekea wapiganaji wa palipehutu/FNL kuingia ndani ya majumba ya raia na kupora chakula. Msemaji wa palipehutu/FNL ameitolea mwito jamii ya kimataifa kuongeza idadi ya chakula wanacho pewa wapiganaji wa kundi hilo wakati huu. Kama alivyo fahamisha, kila mpiganaji hupewa chakula mara moja kwa siku, sawa na kilo 4 kwa wiki.



WATUHUMIWA 6 WA MAUAJI YA DACTARI KASSY MANLAN WAACHIWA HURU.


Bujumbura le 14/7/2008 Watuhumiwa 6 wa mauaji ya aliekuwa muakilishi mkaazi wa shirika la afya ulimwenguni nchini Burundi, Dactari Kassy Manlan, wameachiwa huru. Korti kuu ya sheria iliamuru watuhumiwa hao wafunguliwe tangu juni 12, baada ya kufungwa kwenye jela kuu la Mpimba tangu Novemba 2003. watuhumiwa hao 6 ambao ni pamoja na Gerard ntunzwenayo, Emile Manisha, Aloys Bizimana, Japhet Ndayegamiye, Expert Bihumugani na Athanase Bizindavyi, wamebaini kuridhishwa na kufunguliwa kwao. hata hivo Pierre Claver Mponimba kiongozi wa shirika linalo tetea haki za wafungwa amesema kwamba kufunguliwa kwa watuhumiwa hao ni pigo kubwa kwa vyombo vya sheria nchini Burundi, kiongozi huyo amebaini kuwa kesi hiyo lazima ifikie kileleni na wahusika lazima watambulike. Jamii ya warundi wanajiuliza wakati huu kuhusu hatma ya kesi hiyo baada ya watuhumiwa hao kukutwa bila hatia. Upande wake Wakili Marc BIRIHANYUMA amesema kusikitishwa kuona vyombo vya dola na vile vya sheria vimeshindwa kuendesha uchunguzi kama ipasavyo kuhusu kifo cha hayati Kassy Manlan ili warundi na jamii ya kimataifa watambuwe ukweli zaidi kuhusu kifo hicho ambacho kina tatanisha. Inavyo dhihirika wakati huu, utafkiri kwamba hayati Manlan alijiua mwenyewe na baadae kenda kujitupa katika ziwa tanganyika, amesema hayo mwanasheria huyo.
KIONGOZI ZAMANI WA SHULE LA GATABO MKOANI MURAMVYA AUAWA NA MTU ALIE VALIA SARE ZA KIJESHI.

kiongozi zamani wa shule la upili la tarafa ya GATABO Jean Claude NSHIMIRIMANA ameuawa katika usiku wa jumatatu kuamkia jumanne nyumbani kwake na mtu aliekuwa amevalia sare za kijeshi ambae hadi sasa hajatambulika. Mauaji hayo yametokea katika kata ya Kigwati inayo patikana mjini kati Muramvya. Kwa mujibu wa Muandishi habari wa kituo cha kutawanyia habari Mkoani Muramvya ABP, Philippe SENDAZIRASA, hayati huyo aliuawa muda mfupi wakati aliporejea nyumbani kwake, ghafla amimuona muhalifu anaingia ndani na ambae alimfahamisha kuwa amekuja kummalizia maisha, papo hapo alichomoa bunduki aliokuwa nayo aiana ya bastola na kumpiga risase 3 kichwani. Hayati Jean Claude NSHIMIRIMANA hadi sasa alikuwa mwalimu kwenye shule la upili la Shombo katika tarafa ya Muramvya.


ALAIN MUGABARABONA KIONGOZI ZAMANI WA FNL/ICANZO KAITOROKA NCHI.

Mugabarabona mwenyekiti zamani wa chama cha FNL/ICANZO ambae alikatiwa kifungo cha miaka 20 jela kutokana na shutma za kutaka kuipiduwa serikali ya Burundi asadikiwa kuitoroka nchi katika mazingira ambayo yanatatanisha. Kutoroka kwa Dk Alain Mugabarabona hakuthibitishwi wala kukanushwa na mkurugenzi mkuu wa jela kuu la Mpimba Afisa Victor Segasago, kwa kuwa mfungwa huyo alikuwa amepewa ruhusu ya kuzuru nyumbani kwake ili kutatua matatizo yaliokuwa yakiripotiwa katika familia yake. Kama alivyo fahamisha afisa huyo, Kibali cha kutoka jela kilikuwa kimetolewa na mkurugenzi mkuu wa magereza Anaclet Gasamirwa, ilikuwa tarehe 17 juni iliopita. Kuliko kurejea katika jela kuu la Mpimba, Alain Mugabarabona alipewa kibali kingine cha siku 15 na mkurugenzi huyo wa magereza Anaclet Gasamirwa kama inavyo agizwa na sheria za mambo ya ndani za magereza. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa Mpimba Alain Mugabarabona anatakiwa kurejea katika jela kuu la Mpimba leo saa kumi na moja majira ya hapa nyumbani. Iwapo hatorudi shutuma zote atazibeba yule ambae aliemuwekea dhamana nae si mwengine ni wakili wake Jean Bosco Nyakiki, ambapo mkurugenzi mkuu wa jela kuu la Mpimba alionyesha faili alizo saini wakili nyakiki. Itafahamika kuwa muda wote aliopewa kibali cha kutoka nnje ya jela kuu la Mpimba Dk Alain Mugabarabona hakuwa na walinzi. Mtu mwingine ambae anasadikiwa kuwa kaitoroka nchi ni Gérard NGENDABANKA aliwahi kuwa hakimu mkuu wa jamuhuri, ambae inasadikiwa kuwa anatambuwa mengi zaidi kuhusu kifo cha hayati Dk Kassy Manlan muakilishi mkaazi wa shirika la Afya ulimwenguni OMS alieuliwa nchini hapa mwaka 2001. Washukiwa wa mauji hayo waliachiwa huru kwa kukutwa bila hatia.

mercredi 9 juillet 2008

BUJUMBURA LE 9.7.08. SERIKALI YA BURUNDI YA WAASA WAPIGANAJI WA PALIPEHUTU/FNL KUMALIZA HARAKA MPANGO WA KUWAKUSANYA WAPIGANAJI WAKE KWENYE VITUO TEUL

Serikali ya Burundi kupitia msemaji wake bibi Hafsa MOSSI akiwa pia waziri wa habari na ushirikiano wa bunge la Burundi, imetangaza kuhusu msimamo wa Palipehutu/FNL

HABARI ZA SIASA

Bujumbura le 8.7.08. LICHA YA MATATIZO YA UKOSEFU WA LISHE YA KUTOSHA WAPIGANAJI WA PALIPEHUTU/FNL WASEMA KU GANGA NJAA.
Wapiganaji wa palipehutu/FNL walioko katika kituo teule cha huko Mkoani Bubanza tarafani Rugazi, wanakabiliwa na matatizo ya uhaba wa chakula. Kama tulivyo shuhudia Kwenye eneo hilo liliotengwa kuwapokea wapiganaji wa kundi la palipehutu/FNL la hapo Rugazi, ni kwenye umbali za kilomita zaidi ya 20 hivi ukitokea katika kijiji cha Muzinda. Kambi hiyo yawajumuisha wapiganaji 155 ambao wanalindwa na askari wa Afrika kusini. Ukifika eneo hilo utawakuta wapiganaji wa palipehutu FNL wamo ndani yake, waki randa randa bila kuwa na lolote la kufanya huku wengine wakifua nguo zao wengine wakicheza kisoro. Wapiganaji hao hawana silaha, lakini kiasii ya wengi wanavalia sare za kijeshi. Kila anae taka kutoka nnje ya kambi hiyo hupewa kibali na kiongozi wa wapiganaji kambini humo. Duru kutoka kambini hapo zaarifu kuwa wanayo matatizo ya kupata lishe ya kutosha, wapiganaji hao hupewa chakula mara moja kwa siku yaani kwa wiki kila mmoja hupewa kilo 4 za chakula ambazo imeendelea kuarifuduru hiyo kiasi hicho hakitoshi hata kidogo lakini hata hivo wanavumilia. Duru hiyo imeeeleza pia matatizo ya ukosefu wa madawa, yale wanao pewa ni ya kutibu vidonda ambavyo wakati huu vita ilisimama hakuna wanaouumia. Mbali kidogo na eneo hilo kama kilometa 15 ukielekea katika msitu wa Kibira katika mlima wa Kibuye, kuna kambi nyingine ya wapiganaji ambayo ilitengwa ya wale ambao wanajiandaa kuelekea katika kambi iitwayo ya Cantonnement iwapo majadiliano yataendelea vizuri. Ukifika eneo hilo utawakuta wapiganaji wengi kwenye barabara ya mlima huo na hata juu ya mlima utakuta tujumba twa misonge ambato wameanza kujenga, hii ni baada ya kukumbwa na matatizo ya kunyeshewa na mvua kubwa zilizo nyesha wiki iliopita ilioharibu vitu walivyokuwa navyo kama vile unga. Wengi wao wanazo silaha mikononi. Wapiganaji hao wanaskitishwa kuona hawajapewa maturubai hadi sasa, wanashinda na jua lao, mvua yao. Wamearifu kwamba pindi walipokuwa msituni walijitegemea kwa kila kitu, lakini wakati huu katika hali ya kuheshimisha majadiliano wanakubali kuvumilia hali hiyo, kwa kuwa wamearifu hawajafikia kuishi maisha mazuri, bado wanaendesha maisha waliokuwa nayo wakati wa mapambano. Hata hivo wamesema kuwa na wasiwasi kutokana na matamshi ya wanasiasa. Wananchi wa maeneo hayo wamearifu kueshi vizuri na wapiganaji hao licha ya kujitokeza mara kadhaa vitendo ambavyo wamesema imekua vigumu kuthibitisha kwamba ni wapiganaji hao ndio wanaohusika ao la. Wananchi wa maeneo hayo wanafurahishwa na hatua ambayo imekwisha pigwa na hivo wametolea mwito wanasiasa kuendeleza mazungumzo ili kufikia kikomo cha mazungumzo katika hali ya muafaka. Wapiganaji hao wameomba wapewa vifaa mahitajio muhimu kama vile chakula cha kutosha na madawa kwa kuwa iwapo itafikia wasitishe kuwapa chakula silaha bado wanazo na hazijaziba, wataendelea kueshi kama walivyokuwa wakieshi wakati wa mapambano.
BIOGRAPHIE
NDUWIMANA Didier A.k.a Sugu Jay Tishio, ni kijana ambae ndoto yake wakati huu inaonekana ku shamiri kiasi fulani, hii ni baada tu ya kufanyakazi yake vizuri na kazi hiyo kupokelewa vema na mashabiki wa muziki nchini Burundi. Sugu Jay Tishio ni kijana wa 4 katika familia ya watoto wa 7. Amezaliwa Octoba 13 mwaka 1985 mjini Bujumbura.
Ni yatima aliwapoteza wazazi wake wapendwa, mama yake tarehe 6/02/2000. Na baba yake 7/08/2001. Shule ya msingi alisoma Ngagara Q3, Vita ilipozuka nchini Burundi alisimamisha, baadae akaendelesha kwenye shule la msingi la barabara ya 8 Buyenzi maharufu jumuia. amakuhusu Secondari, alisoma kwenye shule la kiufundi la Lycée Technique St-luc ambapo alipata shahada ya A2 kwenye kitivo cha fundi waya wa magari ama (electromecanique) ilikuwa mwaka 2005. Muziki alianza toka utotoni kwani anaamini kuwa kipaji mtu huzaliwa nacho.
katika mwaka 1992, alikuwa akirudilia nyimbo zilizopendwa hasa za christophe matata wa nchini Burundi na Wenge Musica kundi ambalo lilikuwa likipga fora nchini Zaire zamani ambayo ni RDCongo kwa sasa. Majirani walimpenda sana hapo ndipo wazazi wake walimjulisha kitu ambacho hawezi sahau, walimueleza kwamba toka angali mdogo sana alikuwa na tabiya yakuomba kila kitu akiimba asa alipokuwa akihisi njaa. Aliendelea kutunga nyimbo zake.
2001 alianzicha kikundi chake (To Be One) ambapo walikuwa wakitumiya Instrumental za inje, waliweza kuuzuria tamasha mbali mbali moja yazo ni shindano liloandaliwa na ASIYA HEMEDI wa RTNB, Ata hivo alikuwa ajaupa mziki muda mwingi kwa mama alikuwa anapenda masomo sana .
2004, ndipo alirekodi nyimbo yake yakwanza (I wanna Live With U) ambayo ili mpa kutambulika kote inchini na kupata mialiko inje na ndani ya nchi akatowa zingine nyimbo.2006, alialikwa kwenye show Kigali, akapabaki myezi 6 ili aitambulishe kazi yake vizuri. Kule alitowa NDABATASHA ikapata tunzo la mziki bora ,shindano liloandiliwa na Radio Flash FM Rwanda, akapta mashabiki wengi rwanda na burundi.
Aliporudi Burundi, wa Kaunda kundi kwajina la OGOPA BAND akiwa na wenzake,Guyrap,s na Mss G Flow.waliweza kuanda show kubwa tarehe 6.12.2006,ila kundi ilo alikuweza kuendelea.
Ndipo compun ya TOP IKOH ikatambuwa kipaji chake ikaamuwa ku msapoti ili waufanye mziki kazi.Ndipo alipoitowa MAISHA KAMA GAME ambayo ikatambulisha ALBUM yake ya nyimbo 10 zifwatazo :
1 .I wonna live with u ft Rick Dogg,Mss G Flow prod Jeremie.
2 .Kama unanipenda prod Jeremie.
3.Maisha kama game prod Ado,Bochum,Alex.
4.Kisa dem ft Fizzo prod Dr Jack F2K Rwanda.
5.Nzirinda prod Ado alpha record.
6.Ndabatasha Remix prod Dr Jack Rwanda.
7.Iwacu ni heza remix prod Dr Jack F2K Rwanda.
8.Amidah ft Dr Cloud prod Dr Jack F2K RWANDA,
9. BORA UNGEACHA Prod Dr Jack F2K Rwanda.
10. Kisa dem Part 2.
Kinyume na nyimbo zake alishirikishwa na wasani wengi inje na ndani ya inchi. Baadhi yazo ni maisha ya ghetto pamoja na Mr. Fanu wa congo Uvira, Inyange na Master SMG wa rwanda, Ili hit sana Kigali, Umenitoka na Public Familly wa Bubanza, Ubudodi na Didier wa Rwanda, Bomba Style na EA Boyz wa Rwanda, Twende beach na OZB wa Bongo. Ono omwana na Cool Man wa kampala.
Aliweza kuhuzuriya Show nyingi (saga plage, la pirogue, muse vivant (Akabirya talent show walo udhuriya wanajuwa ilikuwaje sugu jay alipo paa jukwani) , centre culturel francais, odeon palace) inje ya inchi (ruhengeri, kigali na universty ya butare rwanda) na Uvira. Na pote aliintangaza inchi yake Burundi vizuri.

habari

Hii ni moja miongoni mwa sehemu ambayo utakuta habari kutoka nchini Burundi katika lugha ya kiswahili,na hata habari kutoka ukanda mzima wa maziwa makuu. waweza pia kuchangia huku ukiwa mtaarabu kati ya yale ambayo labda waona kwamba waweza kutowa muelekeo zaidi.