mercredi 17 juin 2009

RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA AREJEA NYUMBANI BAADA YA KUSHIRIKI MAMOBOLEZO YA KIFO CHA MAREHEMU OMAR BONGO ONDIMBA


Rais wa jamuhiri Pierre Nkurunziza amerejea nyumbani hii leo akitokea mjini Libreville nchini Gabon ambako alikuwa amekwenda kutowa heshimwa zake za mwisho kwa marehemu Elhadji Omar Bongo rais wa Gabon aliefariki huko Barcelona Hispania wiki zilizopita. Rais Nkurunziza kama vile ma rais wengine 15 wa bara la Afrika walishiriki jana katika shughuli za kuomboleza kifo cha rais huyo Mkongwe wa ma rais wa Afrika. Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa jijini Bujumbura rais Nkurunziza amesema nchi ya Gabon ilionyehsa utawala bora katika kipindi cha muda mrefu, hasa marehemu Omar Bongo Ondimba alisaidia sana katika kuyasogeza makundi yaliokuwa yakigomba nchini Burundi kwa kuwashawishi wakae kwenye meza ya majadiliano. Ameendelea kuwa mbali na Burundi Marehemu Omar Bongo Ondimba alichangia pia katika kusuluhisha mizozo mingi barani Afrika. Pierre Nkurunziza amesema kutokana na uongozi wake bora marehemu Bongo alipendwa sana na wananchi wake ambao wameshuhudiwa wakistika kifo cha rasi wao, hivo rais Omar Bongo atasalia kuwa mfano wa kuigwa na viongozi wa bara hili la Afrika.