
Kiongozi wa waasi wa FDLR aliyekamatwa nchini Rwanda Laurent Nkunda ameishtaki serikali ya Rwanda kwa kumzuilia kinyume cha sheria. Katibu wa Idara ya habari ya Rais nchini Rwanda Yoland Makolo amesema kuwa, kesi ya Jenerali Nkunda dhidi ya serikali ya Kigali imesikizwa ijumaa April 17 lakini akasita kueleza uamuzi uliotolewa. Makolo ameongeza kuwa, Nkunda atarejeshwa nchini Congo anakotakiwa kujibu mashtaka ya ubakaji, utekaji nyara, kuwashirikisha watoto wadogo vitani pamoja na jinai zinginezo. Jenerali nkunda yuko chini ya kifungo cha nyumbani tangu mwezi Januari mwaka huu anakozuiliwa na serikali ya Rwanda. Mataifa ya Congo na Rwanda yamekuwa yakinyoosheana kidole cha lawama kuhusiana na suala la waasi lakini kuzuiliwa kwa Nkunda na serikali ya Rais Paul Kagame wa Rwanda ni dhihirisho tosha kuwa nchi hizo mbili ziko tayari kubadilisha mkondo wa uhusiano wao, wamesema weledi wa mambo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire