MAZUNGUMZO YA VYAMA VYA KISIASA YAZINDULIWA MKOANI GITEGA
Bujumbura le 18/8/2008. Kumeanzishwa hii leo Mkoani Gitega mazungumzo yanayo jumuisha wawakilishi wa vyama vya kisiasa vilivyo sajiliwa kisheria hapa nchini, ili kujadili kwa pamoja kuhusu maswala mahimu yanayo ikumba Burundi wakati huu. Mwenyekiti wa chama UPRONA Aloys Rubuka ameomba chama kilichoko madarakani na viongozi mbalimbali waonyeshe utashi wa kutaka kuheshimisha maazimio yanayo chukuliwa katika mijadala tofauti na kwamba ni lazima chama madarakani kielewe vema madhumuni ya mazungumzo hayo, kinyume na hivo majadiliano hayo yatakuwa kama kuongeza mzigo juu ya ungine, amesema hayo mwenyekiti wa chama UPRONA Aloys Rubuka. Upande wake mwenyekiti wa chama Sahwanya FRODEBU Léonce NGENDAKUMANA amesema kuwa katika mazungumzo hayo watasisitiza kuhusu kutatua matatizo yalioko nchini ambayo yaweza kuwa pengamizi kwa majadiliano hayo. Amesema miongoni ni pamoja na swala la usalama kuhusu mkataba na uheshimishwaji wa kusitisha vita baina ya serikali na Palipehutu FNL, maswala ya Utawala bora na matumizi ya pesa ya serikali kwa mantiki binafsi. Léonce NGENDAKUMA amesema watasisitiza ili maswala hayo yagusiwe, badala yake amesema mazungumzo hayo yatakuwa ni nyongezo isiokuwa na faida. Amemalizia kusema mchango wa chama FRODEBU utakuwa ni uleule ambao FRODEBU imekuwa ikiutoa kila mara inapo pata fursa ya kujadiliana.
Ama kuhusu Upande wa chama madarakani CNDD-FDD msemaji wake Onesime NDUWIMANA amesema kuwa chama chake kitashiriki kikamilifu katika mazungumzo hayo kwa njia ya kudumisha amani na utulivu jote nchini na wala chama CNDD-FDD hakiwezi kamwe kutia pengamizi lolote katika mazungumzo hayo.
WAKATI SENSA YA WANANCHI NA MAKAAZI YAARIFiWA KUFANYIKA VEMA KOTE NCHINI MKOANI MURAMVYA KUNA KASORO
Bujumbura le 18/8/2008. Sensa ya wananchi na makaazi iliozinduliwa juzi jumamoso yaendelea kufanyika barabara kote nchini. Wale ambao wataopinga kufanya sensa hiyo wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria iliosainiwa Septemba 25 mwaka jana. Amesema hayo Térence MBONABUCA afisa msimamizi wa sensa hiyo. Wakati hayo yakiarifiwa Mkoani Muramvya kuna mwalimu mmoja ajulikanae kwa jina la Jonas NIZIGIYIMANA ambae amekuwa akiendesha shughuli za kuwahamasisha wananchi wasusie sensa ya wananchi na makaazi. Habari zaidi kutoka mkoani hapo zarifu kuwa mwalimu huyo alianza shughuli hizo mapema, pindi tu alipo kataliwa kuorodheshwa kwenye idadi ya watao endesha sensa baada ya kwamba alishindwa mtihani. Upande wa ofisi inayo husika na sensa mkoani hapo Muramvya waarifu kuwa mtu huyo hakuwa na alama za kumuwezesha kuendesha sens ya wananchi na makaazi. Wananchi wa eneo hilo wameonekana kutii wito wa mwalimu huyo, baada ya wengi kutojibu maswala kadhaa muhimu wanayo ulizwa na ma afisa wanaoendesha Sensa. Wakati huo huo Mratibu wa Sensa ya wananchi na makaazi katika mkoa wa kusini mwa nchi wa Makamba Dominique NIYONDIKO amesema kuskitishwa kuona hadi sasa kunabaadhi ya wananchi ambao hawajatambua vema umuhimu wa sensa. kuna watu ambao wamekuwa wakitapakaza fikira potovu eti kwamba majumba yaliopakwa chaki wakati wa kuandika namba ndio, ambayo yamo mbioni kubomolewa, huku waumini wa baadhi ya madini ya kikristo wakiarifu kuwa hayo yanayo fanyika ni kinyume na neno la Yesu Christo. Mratibu huyo wa maswala ya sena mkoani hapo amewatolea mwito viongozi wa ngazi za china, kuwahamasisha wananchi vya kutosha ili waitikie kwa wingi sensa hiyo muhimu kwa nchi na wananchi.
POLISI YA BURUNDI YATAKA KUJUWA IDADI RASMI YA JESHI LA POLISI.
Bujumbura le 18/8/2008.Wakati kunafanyika hapa nchini ,kama ulivosikia , sensa ya kujua idadi kamili ya wakaazi wa Burundi wakati huu,polisi nao wameanzisha sensa ya kuitambua idadi rasmi ya jeshi la polisi nchini hapa. Mbali na maswali kadhaa watakayoyajibu , polisi watatakiwa kueleza wanatokea kabila gani ili kujaaribu kuweka usawa kwenye uwakilishi wa makabila katika taasisi hiyo ya usalama wa taifa. Sensa hiyo itashuhudia pia uanzishwaji wa vyombo vya kukagua polisi katika vitua mbalimbali. Kama alivyo fahamisha msemaji wa jeshi la polisi Pierre Chanel Ntarabaganyi kuna umuhimu mkubwa sana wa kujuwa idadi rasmi ya polisi na tabaka zao ili kuheshimisha mikataba inayo agiza asilimia 50 kwa wahutu na asilimia 50 kwa watutsi
JESHI LA TAIFA LA ANDAA MIJALA NA RAIA
Bujumbura le 18/8/2008.Katika hali ya kudumisha nidhwamu jeshini, pamoja na kudumisha uhusiano bora ulioko baina ya wanajeshi na raia, wizara ya ulinzi imeanzisha mijadala tofauti wakishiriki wawakilishi wa mashirika ya kiraia na wananchi wa kawaida. Kama alivyo fahamisha kanali Mponimba Athanase ambae aliendesha mjadala, mazunzungumzo hayo yanamadhumuni ya kuwafahamisha wananchi kuhusu juhudi zinazo fanywa katika mageuzi ya jeshi la taifa, juhudi ambazo zinaelekea ku vifanya vikosi vya taifa viwajibike barabara na jinsi gani ya kueshi na raia. Amesema afisa huyo kwamba jeshi la tumikia raia, na wananchi ndio ambao watowa uwezo kwa jeshi kwa hiyo, amesema ni lazima wananchi watambuwe vema janayo jiri jeshini. lakini hata hivo kumekuwa na maswala ambayo mtu aweza kujiuliza, hadi muda wote huu inamaanisha kwamba idadi ya polisi hawakujulikana?
1 commentaire:
kwa kweli hata mie nachoshwa sana kuona mna kawia kutupa habari
Enregistrer un commentaire