mercredi 9 juillet 2008

HABARI ZA SIASA

Bujumbura le 8.7.08. LICHA YA MATATIZO YA UKOSEFU WA LISHE YA KUTOSHA WAPIGANAJI WA PALIPEHUTU/FNL WASEMA KU GANGA NJAA.
Wapiganaji wa palipehutu/FNL walioko katika kituo teule cha huko Mkoani Bubanza tarafani Rugazi, wanakabiliwa na matatizo ya uhaba wa chakula. Kama tulivyo shuhudia Kwenye eneo hilo liliotengwa kuwapokea wapiganaji wa kundi la palipehutu/FNL la hapo Rugazi, ni kwenye umbali za kilomita zaidi ya 20 hivi ukitokea katika kijiji cha Muzinda. Kambi hiyo yawajumuisha wapiganaji 155 ambao wanalindwa na askari wa Afrika kusini. Ukifika eneo hilo utawakuta wapiganaji wa palipehutu FNL wamo ndani yake, waki randa randa bila kuwa na lolote la kufanya huku wengine wakifua nguo zao wengine wakicheza kisoro. Wapiganaji hao hawana silaha, lakini kiasii ya wengi wanavalia sare za kijeshi. Kila anae taka kutoka nnje ya kambi hiyo hupewa kibali na kiongozi wa wapiganaji kambini humo. Duru kutoka kambini hapo zaarifu kuwa wanayo matatizo ya kupata lishe ya kutosha, wapiganaji hao hupewa chakula mara moja kwa siku yaani kwa wiki kila mmoja hupewa kilo 4 za chakula ambazo imeendelea kuarifuduru hiyo kiasi hicho hakitoshi hata kidogo lakini hata hivo wanavumilia. Duru hiyo imeeeleza pia matatizo ya ukosefu wa madawa, yale wanao pewa ni ya kutibu vidonda ambavyo wakati huu vita ilisimama hakuna wanaouumia. Mbali kidogo na eneo hilo kama kilometa 15 ukielekea katika msitu wa Kibira katika mlima wa Kibuye, kuna kambi nyingine ya wapiganaji ambayo ilitengwa ya wale ambao wanajiandaa kuelekea katika kambi iitwayo ya Cantonnement iwapo majadiliano yataendelea vizuri. Ukifika eneo hilo utawakuta wapiganaji wengi kwenye barabara ya mlima huo na hata juu ya mlima utakuta tujumba twa misonge ambato wameanza kujenga, hii ni baada ya kukumbwa na matatizo ya kunyeshewa na mvua kubwa zilizo nyesha wiki iliopita ilioharibu vitu walivyokuwa navyo kama vile unga. Wengi wao wanazo silaha mikononi. Wapiganaji hao wanaskitishwa kuona hawajapewa maturubai hadi sasa, wanashinda na jua lao, mvua yao. Wamearifu kwamba pindi walipokuwa msituni walijitegemea kwa kila kitu, lakini wakati huu katika hali ya kuheshimisha majadiliano wanakubali kuvumilia hali hiyo, kwa kuwa wamearifu hawajafikia kuishi maisha mazuri, bado wanaendesha maisha waliokuwa nayo wakati wa mapambano. Hata hivo wamesema kuwa na wasiwasi kutokana na matamshi ya wanasiasa. Wananchi wa maeneo hayo wamearifu kueshi vizuri na wapiganaji hao licha ya kujitokeza mara kadhaa vitendo ambavyo wamesema imekua vigumu kuthibitisha kwamba ni wapiganaji hao ndio wanaohusika ao la. Wananchi wa maeneo hayo wanafurahishwa na hatua ambayo imekwisha pigwa na hivo wametolea mwito wanasiasa kuendeleza mazungumzo ili kufikia kikomo cha mazungumzo katika hali ya muafaka. Wapiganaji hao wameomba wapewa vifaa mahitajio muhimu kama vile chakula cha kutosha na madawa kwa kuwa iwapo itafikia wasitishe kuwapa chakula silaha bado wanazo na hazijaziba, wataendelea kueshi kama walivyokuwa wakieshi wakati wa mapambano.

Aucun commentaire: