mercredi 16 juillet 2008

KIONGOZI ZAMANI WA SHULE LA GATABO MKOANI MURAMVYA AUAWA NA MTU ALIE VALIA SARE ZA KIJESHI.

kiongozi zamani wa shule la upili la tarafa ya GATABO Jean Claude NSHIMIRIMANA ameuawa katika usiku wa jumatatu kuamkia jumanne nyumbani kwake na mtu aliekuwa amevalia sare za kijeshi ambae hadi sasa hajatambulika. Mauaji hayo yametokea katika kata ya Kigwati inayo patikana mjini kati Muramvya. Kwa mujibu wa Muandishi habari wa kituo cha kutawanyia habari Mkoani Muramvya ABP, Philippe SENDAZIRASA, hayati huyo aliuawa muda mfupi wakati aliporejea nyumbani kwake, ghafla amimuona muhalifu anaingia ndani na ambae alimfahamisha kuwa amekuja kummalizia maisha, papo hapo alichomoa bunduki aliokuwa nayo aiana ya bastola na kumpiga risase 3 kichwani. Hayati Jean Claude NSHIMIRIMANA hadi sasa alikuwa mwalimu kwenye shule la upili la Shombo katika tarafa ya Muramvya.


ALAIN MUGABARABONA KIONGOZI ZAMANI WA FNL/ICANZO KAITOROKA NCHI.

Mugabarabona mwenyekiti zamani wa chama cha FNL/ICANZO ambae alikatiwa kifungo cha miaka 20 jela kutokana na shutma za kutaka kuipiduwa serikali ya Burundi asadikiwa kuitoroka nchi katika mazingira ambayo yanatatanisha. Kutoroka kwa Dk Alain Mugabarabona hakuthibitishwi wala kukanushwa na mkurugenzi mkuu wa jela kuu la Mpimba Afisa Victor Segasago, kwa kuwa mfungwa huyo alikuwa amepewa ruhusu ya kuzuru nyumbani kwake ili kutatua matatizo yaliokuwa yakiripotiwa katika familia yake. Kama alivyo fahamisha afisa huyo, Kibali cha kutoka jela kilikuwa kimetolewa na mkurugenzi mkuu wa magereza Anaclet Gasamirwa, ilikuwa tarehe 17 juni iliopita. Kuliko kurejea katika jela kuu la Mpimba, Alain Mugabarabona alipewa kibali kingine cha siku 15 na mkurugenzi huyo wa magereza Anaclet Gasamirwa kama inavyo agizwa na sheria za mambo ya ndani za magereza. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa Mpimba Alain Mugabarabona anatakiwa kurejea katika jela kuu la Mpimba leo saa kumi na moja majira ya hapa nyumbani. Iwapo hatorudi shutuma zote atazibeba yule ambae aliemuwekea dhamana nae si mwengine ni wakili wake Jean Bosco Nyakiki, ambapo mkurugenzi mkuu wa jela kuu la Mpimba alionyesha faili alizo saini wakili nyakiki. Itafahamika kuwa muda wote aliopewa kibali cha kutoka nnje ya jela kuu la Mpimba Dk Alain Mugabarabona hakuwa na walinzi. Mtu mwingine ambae anasadikiwa kuwa kaitoroka nchi ni Gérard NGENDABANKA aliwahi kuwa hakimu mkuu wa jamuhuri, ambae inasadikiwa kuwa anatambuwa mengi zaidi kuhusu kifo cha hayati Dk Kassy Manlan muakilishi mkaazi wa shirika la Afya ulimwenguni OMS alieuliwa nchini hapa mwaka 2001. Washukiwa wa mauji hayo waliachiwa huru kwa kukutwa bila hatia.

Aucun commentaire: