CHAMA KIKUU CHA UPINZANI NCHINI BURUNDI FRODEBU KIMEMTEUWA DOMITIEN NDAYIZEYE KUWA MTETEZI WAKE KWENYE UCHAGUZI WA MWAKA 2010. Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi Sahwanya FRODEBU kimemteuwa rais wa zamani wa Burundi Domitien NDAYIZEYE kusimama kwenye uchaguzi wa 2010 utaofanyika nchini Burundi.
katika uchguzi wa wajumbe wa kamati tendaji uliofanyika jumapili octoba 12.2008 uliojumuisha wajumbe 268, Domitien NDAYIZEYE lichaguliwa kwa asilimia 86.5 ya kura dhidi ya wagombea wengine wawili Pierre Claver NAHIMANA na Rose NDUWAYO. Baada ya kuteuliwa kwake, rais huyo wa zamani aliviambia vyombo vya habari kuwa, alikuwa ametangaza kuachana na siasa baada ya kuondoka kwenye utawala mwaka 2005, na kufungwa kwake kwenye jela kuu la Mpimba mwaka 2006, sasa amerejea kwenye uwanja wa siasa ili kupambana na rais alieko madarakani wakati huu. FRODEBU ni chama cha kwanza cha upinzani kutangaza rasmi mgombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Domitien NDAYIZEYE aliiongoza Burundi tangu mwaka 2003 hadi Agosti 2005 wakati wa awamu ya pili ya kipindi cha mpito, kipindi ambacho kilihitimshwa kwa uchaguzu uliopelekea chama CNDD-FDD kunyakuwa ushindi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire