mercredi 15 octobre 2008


PALIPEHUTU/FNL YAPINGA KATAKATA KUBADILI JINA

katika mkutano uliitishwa na katibu mkuu wa palipehutu FNL Jonas NSHIMIRIMANA jumanne 14 octoba, aliwaambia waandishi habari kuwa kamwe Palipehutu FNL haitothubutu kubadili jina hilo, na kwamba iwapo watafanya hivyo, basi watakuwa wamekwenda kinyume na mkataba, kwa kuwa mikataba yote waliosaini na serikali ya Burundi walitumia jina hilo Palipehutu/FNL na itakuwa ni kuvunja mkataba wakati ambapo hawana nia ya kuvunja mkataba huo. Seriklai ya Burundi imelipa sharti kundi hilo kubadili jina kabla ya kukubaliwa rasmi kama chama cha kisiasa, kwa kuwa kama inavyo sema taarifa ya serikali ni kinyume cha katiba ya Burndi iwapo kitasainiwa chama chenye jina la kikabila. Licha ya kukwama kwa mazungumzo ya palipehutu/FNL na serikali ya Burundi, Jonas NSHIMIRIMANA amesema kuwa majadiliano yataendelea hadi pale serikali itaitambua Palipehutu/FNL kama chama rasmi cha kisiasa. Katibu mkuu wa Palipehutu FNL ametumia fursa hiyo kukanusha habari kwamba kuna mzozo wa ndani katika kundi hilo la palipehutu FNL ambapo mwenyekiti wa kundi hilo Agathon RWASA na msemaji wa palipehutu FNL Pasteru HABIMANA hawapatani na kwamba kila mmoja anafuyawafuasi wake. Kiongozi huyo amekanusha habari hizo na kusema kuwa huo ni uzushi mtupu.

Aucun commentaire: