mercredi 15 octobre 2008

MIAKA 3 IMEMALIZIKA CHAMA CNDD-FDD KIWA KWENYE UTAWALA NCHINI BURUNDI
Chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimeazimisha myaka 3 Jumapili tarehe 12 Octoba 2008 kikiwa kwenye usukani wa kuiongoza Burundi. sherehe rasmi za siku kuu hiyi zimefanyika katika Mkoa wa Gitega Kaskazini mwa Burundi. Wafuasi wa chama hicho kutoka katika kila mikoa ya Burundi walimiminika kwa wingi kuhudhuria sherehe hizo. Wajumbe wa vyama vingine vya upinzani walialikwa kwenye sherehe hizo. chama kinacho tawala nchini Jamuhuri ya Kimokrasia ya Congo PPRD kiliwatuma wajumbe wake kushiriki kwenye sherehe hizo ambazo zilionekana kufana kiasi fulani. halaiki ya watu walimiminika kwenye uwanja wa mpira wa miguu Mkoani Gitega huku wakivalia sare za chama CNDD-FDD. Akiwahutubia wafuasi wake mwenyekiti wa chama CNDD-FDD Jéremie NGENDAKUMANA alisema kuwa siku hiyo ni siku ya furaha kwa kila mwananchi na hasa wanachama wa CNDD-FDD kwa kuwa ni mara ya kwanza utawala uliochaguliwa katika misingi ya kidemokrasia unafanya zaidi ya miezi 3 madarakani. aliwaambia wafuasi wa chama kuwa wavivu hawana nafasi katika chama, nakwamba lazima watumike kwa bidii katika kuendeleza mipango ya nchi. miaka mitatu hii imemalizika wazazi wanajinfua bila malipo, huku watoto wakisoma bila kutowa hata mea na hata watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 wanatibiwa bila malipo. Jéremie NGENDAKUMANA amewapa kasopo wafuasi wa upinzani ambao wamekuwa wakiimba uchaguzi wakati huu na ilihali kumesalia muda wa miaka 2 wa utawala wa chama hicho kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi. Upande wake rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA ambae ni mfuasi wa chama hicho, alisema kuwa miaka 3 kwenye utawala ni midogo kwa kuwa safari bado ingali ndefu; lakinihata hivo lazima ashukuriwe Mungu. Rais NKURUNZIZA amewatahadharisha wale wote ambao alisema wamekuwa wakimuwekea vizingiti na mitego katika utawala wake, na kwamba wafahamu kuwa wakiendelea kutezga mitego hiyo basi watajikuta wao ndio ambao wameanguka wa kwanza ndani yake. sherehe hizo zlihitimishwa kwa kutowa zawadi kwa walioendesha kzi zao vizuri katika kipindi chote hiki. Miongoni mwa waliopewa zawadi ni Rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA alievalishwa midali, huku wengine kama seneta Muhamed Rukara, Gervais RUFYIKIRI na Pie NTAVYOHANYUMA wakipewa picha zinazo maanisha kuwa wameshukuriwa na chama katika kazi zao.

Aucun commentaire: