dimanche 18 juillet 2010

JEAN CLAUDE KAVUMBAGU MHARIRI WA GAZETI NET PRESS AKAMATWA NA KUTIWA NGUVUNI

Mhariri wa gazeti la Net Press Jean Claude KAVUMBAGU alikamatwa jana jumamosi july 17 na polisi ya taifa kwa tuhuma ya kwamba alichapisha katika gazeti lake taarifa inayosema kwamba jeshi la Burundi na polisi vimezamilia hasa katika uporaji na mauwaji dhidi ya wananchi kuliko kulinda nchi yao. Mwanahabari huyo alikamatwa akiwa ofisini mwake. Wakili wake mtetezi Gabriel SINARINZI akihojiwa kuhusu kukamatwa kwa mteja wake na muungano wa redio za nchini Burundi amefahamisha kwamba Jean Claude KAVUMBAGU amekamatwa kinyume cha sheria kwani alipelekwa moja kwa moja katika jela kuu la Mpimba wakati kesi yake ilikuwa bado haijakatwa. Itafahamika kwamba Jean Claude KAVUMBAGU alihojiwa kwa muda wa masaa mawili kabla ya kupelekwa mbaroni.

Aucun commentaire: