Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta manusura wa ajali ya boti iliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo watu 140 walikufa baada ya boti hiyo iliyobeba abiria kuzidi uwezo wake na kupinduka katika mto. Boti hiyo iliyokuwa na wafanyakazi na abiria wapatao mia mbili inaaminika kugonga kingo za mchanga au mwamba, Jumatano katika maunganiko ya mto Congo, katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo. Baada ya miongo kadhaa ya migogoro, Kongo ina barabara chache au huduma za reli, hali inayosababisha wengi kusafiri kwenye boti hizo zilizojaa pumoni. Mwezi Novemba iliyopita takriban watu 73 walifariki dunia baada ya boti kuzama kwenye ziwa, pia katika jimbo la Bandundu. Ajali iliyotokea hivi karibuni ilitokea siku ya Jumatano. Boti hiyo ilikuwa ikibeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu, mji mkuu katika jimbo hilo. Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo ameliambia shirika la habari la Reuters, " Boti hiyo ilijaa pumoni na haikuweza kuhimili kupita kwenye dhoruba hiyo."vendredi 30 juillet 2010
WAOKOAJI NCHINI DRC, WAENDELEA NA SHUGHULI ZA UOKOZI
Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta manusura wa ajali ya boti iliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo watu 140 walikufa baada ya boti hiyo iliyobeba abiria kuzidi uwezo wake na kupinduka katika mto. Boti hiyo iliyokuwa na wafanyakazi na abiria wapatao mia mbili inaaminika kugonga kingo za mchanga au mwamba, Jumatano katika maunganiko ya mto Congo, katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo. Baada ya miongo kadhaa ya migogoro, Kongo ina barabara chache au huduma za reli, hali inayosababisha wengi kusafiri kwenye boti hizo zilizojaa pumoni. Mwezi Novemba iliyopita takriban watu 73 walifariki dunia baada ya boti kuzama kwenye ziwa, pia katika jimbo la Bandundu. Ajali iliyotokea hivi karibuni ilitokea siku ya Jumatano. Boti hiyo ilikuwa ikibeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu, mji mkuu katika jimbo hilo. Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo ameliambia shirika la habari la Reuters, " Boti hiyo ilijaa pumoni na haikuweza kuhimili kupita kwenye dhoruba hiyo."
Inscription à :
Publier les commentaires (Atom)
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire